Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, piga marufuku mabango ya Waganga wa Kienyeji yaliyojaa barabarani

was njombe

Member
Sep 8, 2020
6
9
Salam Abubakar Kunenge Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

Naomba upige marufuku mabango ya waganga wa kienyeji walio weka barabara na mitaani, hii ni hatari tena ni uchafu wa jiji letu katika ardhi hii ya Tanzania.

Sauti yako mheshimiwa itakuwa ujumbe wa baraka katika utumishi wako. Pili hawa watu wamesababisha umaskini na watu hawafanyi kazi.

Sauti yako kila mmoja mwenye nia njema atakuheshimu. Hadhi ya jiji letu inapotea kwa sababu ya hawa Waganga.
 
Kwakweli, hasa ya nguvu za kiume. Wanaume tumegeuzwa mtaji
 
Majuzi nilikuwa mkoa fulani nikakuta waganga wa jadi wote wameitwa kuelezwa kwamba wanatakiwa wajisajili na kulipa ada ya laki tatu kwa mwaka, wakawa wanajadiliana.

Mmoja wao akawa anawaambia tumpate mhusika ili tumfanyie mambo yetu halafu asahau kabisa hii issue, nikacheka sana mpaka wakanustukia.
 
Kuna yale ya kuwataka watu wajiunge na freemason ili wawe matajiri,Freemason gani hao wanatafuta wanachama wao kwa staili hiyo.Wanaidhalilisha jumuiya Freemason.Hao ni matapeli wanaotumia shida za watu kuwaghilibu
 
Vipi kuhusu Mabango Betting station,
Tatu mzuka,Biko,Bar,Pombe na Sigara Je?
Yaendelee kubaki?

Nafikiri yawe na msimamizi na mdhibiti,
Ili isiwe kila mahala pakueka.
 
Mkuu Iman ya mtu hiyo... watu kama yeriko wanaamin mizimu ya mbutu uko... ko unawakosea watu hawa
 
Back
Top Bottom