MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema anaandaa utaratibu ili wafanyabishara mbalimbali, wakiwamo wa baa waanze kufanya kazi kwa saa 24

mambo juu ya mambo
IMG-20181219-WA0003.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hili namuunga mkono, nachukia sana utaratibu wa kunipangia namna ya kutumia pesa zangu, mi ni mtu mzima, najua wakati gani wa kutafuta na wakati wa kula bata, nikeshe baa au nirudi mapema ni hiari yangu. Sipigi hodi kwa mtu kuomba mkate wa watoto wangu
 
Hahahahahahaaaaa, serikali inategemea wanadoa wafarakane ndipo wapate mapato!! Bado mwaka mmoja yatakuja mengine na kunauwezekano wa kuruhusu madanguro kwa kigezo cha mapato
 
View attachment 986471

Wakati akitangaza neema hiyo, Makonda pia ameeleza kushangazwa na utaratibu unaotumiwa na baadhi ya wamiliki wa nyumba za kulala wageni wa kudai vyeti vya ndoa, unaowafanya wakose mapato. Makonda aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na vyombo vya ulinzi na usalama, wakuu wa wilaya, makatibu tawala, maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa mkoa huo, kuhusu mkakati wa kukusanya mapato bila kuwabughudhi wafanyabishara.

“Maana ya Jiji la Dar es Salaam kuwa Jiji la kibishara ni pamoja na kuwawezesha wafanyabishara kufanya kazi kwa saa 24. Kwa sasa baa zinafunguliwa hadi saa sita usiku lakini mpango wetu zifunguliwe muda wote ili serikali ipate mapato,” alisema Makonda. Alisema endapo baa zitafanya kazi muda wote bila kuwapo na vurugu wala muziki unaosumbua majirani hiyo ni fursa kubwa ya kibiashara katika mkoa huo.

Polisi wamekuwa wakiwasumbua wafanyabishara kinyume cha taratibu zilizowekwa. “Kuna maofisa wa Jeshi la Polisi wanatumia jina la Mkuu wa Mkoa vibaya na kutumia jina langu ni kosa. Nawaomba maofisa mkapitie tena sheria ya hizi za baa, tulikubaliana mwisho iwe saa 8:00 usiku lakini kuna polisi wanatumia vibaya jina langu na kuwakamata watu ovyo kabla ya muda uliopangwa wakisingizia nimewatuma,” alisema Makonda.

Alisema wakati wa mkesha wa mwaka mpya katika moja ya baa Chang’ombe wilayani Temeke, maofisa wa polisi walikwenda kuvamia na kuwakamata watu ovyo wakati wakipiga muziki kinyume cha utaratibu. Aliwaagiza maofisa wa Jeshi la Polisi mkoani humo chini ya Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa, wapitie makubaliano waliyoweka kuwa wafanyabishara wafunge kamera na taa katika ofisi zao ili kufanya biashara muda wote. “Mfanyabishara afanye biashara muda wote.

Kama usalama upo na hapigi muziki unaosababisha usumbufu kwa wengine, kwanza ni vizuri kwa sababu ni ishara ya kuwapo kwa usalama,” alisema Makonda. Aidha, aliwaonya maofisa wa TRA na maofisa wa halmashauri wanaohusika na ukusanyaji kodi kuacha kuwaonea wafanyabishara lakini pia kuwapa elimu badala ya kuwafungia biashara zao.

Pia aliwataka maofisa wanaohusika kuwawezesha vijana kuchangamkia fursa mbalimbali ili vijana waweze kujiajiri na kukuza uchumi wa wakazi wa mkoa huo. Kuhusu watu kwenda kupumzika hotelini au nyumba ya kulala wageni, alisema suala la vyeti vya ndoa haliwahusu wamiliki wa nyumba hizo. “Kama mtu ameamua kuja kupumzika kwenye hoteli yako cheti cha ndoa cha kazi gani? Anakuja kupumzika na nani wewe hayakuhusu.

Watu waachwe wafanye mambo yao ilimradi wewe uingize mapato,” alisema. “Kwanza wanandoa wakigombana nayo ni fursa kwa serikali kwa sababu mmoja atakimbilia baa kupoteza mawazo na mwingine kwa sababu zake anazungusha raundi nyingi kwa watu waliopo baa. Hiyo ni fursa watatuingizia mapato,” alisema Makonda huku akicheka.
Majengo ya baa yamedoda ushuru majengo hora /property tax sheeda, barmaids wamerudi vijijini, wasambazaji kule, halmashari na trei hawakusanyi ,viwanda vya bia kule vya soda kule ajira kwa walinzi kule, wakulima wa ngano na shayiri hora. Wafugaji kuku na mbuzi hora, Bora tu tukae pamoja kwa tafakuri na muafaka.
 
View attachment 986471

Wakati akitangaza neema hiyo, Makonda pia ameeleza kushangazwa na utaratibu unaotumiwa na baadhi ya wamiliki wa nyumba za kulala wageni wa kudai vyeti vya ndoa, unaowafanya wakose mapato. Makonda aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na vyombo vya ulinzi na usalama, wakuu wa wilaya, makatibu tawala, maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa mkoa huo, kuhusu mkakati wa kukusanya mapato bila kuwabughudhi wafanyabishara.

“Maana ya Jiji la Dar es Salaam kuwa Jiji la kibishara ni pamoja na kuwawezesha wafanyabishara kufanya kazi kwa saa 24. Kwa sasa baa zinafunguliwa hadi saa sita usiku lakini mpango wetu zifunguliwe muda wote ili serikali ipate mapato,” alisema Makonda. Alisema endapo baa zitafanya kazi muda wote bila kuwapo na vurugu wala muziki unaosumbua majirani hiyo ni fursa kubwa ya kibiashara katika mkoa huo.

Polisi wamekuwa wakiwasumbua wafanyabishara kinyume cha taratibu zilizowekwa. “Kuna maofisa wa Jeshi la Polisi wanatumia jina la Mkuu wa Mkoa vibaya na kutumia jina langu ni kosa. Nawaomba maofisa mkapitie tena sheria ya hizi za baa, tulikubaliana mwisho iwe saa 8:00 usiku lakini kuna polisi wanatumia vibaya jina langu na kuwakamata watu ovyo kabla ya muda uliopangwa wakisingizia nimewatuma,” alisema Makonda.

Alisema wakati wa mkesha wa mwaka mpya katika moja ya baa Chang’ombe wilayani Temeke, maofisa wa polisi walikwenda kuvamia na kuwakamata watu ovyo wakati wakipiga muziki kinyume cha utaratibu. Aliwaagiza maofisa wa Jeshi la Polisi mkoani humo chini ya Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa, wapitie makubaliano waliyoweka kuwa wafanyabishara wafunge kamera na taa katika ofisi zao ili kufanya biashara muda wote. “Mfanyabishara afanye biashara muda wote.

Kama usalama upo na hapigi muziki unaosababisha usumbufu kwa wengine, kwanza ni vizuri kwa sababu ni ishara ya kuwapo kwa usalama,” alisema Makonda. Aidha, aliwaonya maofisa wa TRA na maofisa wa halmashauri wanaohusika na ukusanyaji kodi kuacha kuwaonea wafanyabishara lakini pia kuwapa elimu badala ya kuwafungia biashara zao.

Pia aliwataka maofisa wanaohusika kuwawezesha vijana kuchangamkia fursa mbalimbali ili vijana waweze kujiajiri na kukuza uchumi wa wakazi wa mkoa huo. Kuhusu watu kwenda kupumzika hotelini au nyumba ya kulala wageni, alisema suala la vyeti vya ndoa haliwahusu wamiliki wa nyumba hizo. “Kama mtu ameamua kuja kupumzika kwenye hoteli yako cheti cha ndoa cha kazi gani? Anakuja kupumzika na nani wewe hayakuhusu.

Watu waachwe wafanye mambo yao ilimradi wewe uingize mapato,” alisema. “Kwanza wanandoa wakigombana nayo ni fursa kwa serikali kwa sababu mmoja atakimbilia baa kupoteza mawazo na mwingine kwa sababu zake anazungusha raundi nyingi kwa watu waliopo baa. Hiyo ni fursa watatuingizia mapato,” alisema Makonda huku akicheka.
Kodi za vinywaji ziko chini by 60% kwa hiyo unjiuliza wakati wanafanya maamuzi haya hawakujua watakosa pesa, stupid decision from day one, mimi nafanya bandarini usiku, unanishika saa nne nakunywa bia ili nikalale, stupid
 
Dah! Ina maana baa za Dar zikiruhusiwa kufanya kazi saa 24, na za mikoani nazo zitaruhusiwa tu maana kuwa na double standard itakuwa ngumu. La sivyo itabidi utumbuzi ufanyike.
Shida ya muingiliano wa madaraka, makonda amechukua madaraka ya mawaziri wote, ardhi, ushoga nk, matatizo ndiyo hayo
 
Back
Top Bottom