Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam nikuombe utoke ofisini kwani mtaani kunamomonyoka

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Mkuu wa Mkoa wa Dsm muda wakusoma majalada umekwisha, Toka nje utuambie upi msimamo wako kwenye mambo yafuatayo na Nini tufanye Kama wananchi?

1. Unajua Trafiki wamekuwa kero barabarani na kuifanya style ya makondakta kuzunguka nyuma ya gari nakuangusha buku buku kama mtindo halali na mfumo rasmi wa utoaji huduma? Tukiwarekodi nakurusha mtandaoni utatulinda au utawalinda?

2. Wamachinga tunawapenda ila mji umechafuka, je waendelee kuzagaa kila kona au unamkakati mzuri wakuwapanga na kuwawekea mazingira bora kwa wao kufanya biashara? Unakubalina na Hali ilivyo Sasa kwenye mitaa yetu?

3. Mvua zilinyesha japo siyo sana, je tuendelee na maandaki kwenye barabara za lami na za vumbi au Kuna utaratibu wakuvisukuma vyombo vilivyopo chini yako kuboresha miundo mbinu hii kwa wakati? Unasemaje, endapo tutakutumia picha mitandaoni kuhusu hali ya miundombinu tutakiwa tunakuchongea kwa maza tutakuwa tunakuahabarisha ujue Hali ilivyo? Tupe ruksa.

4. DAWASCO wamepewa fedha nyingi sana kusambaza maji, je unajua kwamba ubora wa kazi wanayofanya DAWASCO ni wa kiwango Cha chini sana na kiasi kikubwa Cha maji yanapotea njiani kutokana na mabombo kutokufukiwa vizuri na mengi kupitishwa maeneo yanapopita magari? Je unajua maji kuunganisha Hadi wananchi wachangishane kwa kisingizio kwamba mabomba na vifaa hakuna? Je unajua kwamba wafanyakazi wa DAWASCO wanafunga miundombinu chini ya kiwango ili wananchi wawaite wawape chochote kurekebisha miundombinu hiyo?

Je, unajua hadi Sasa hakuna magari na vituo vya kutoa msaada wa haraka( emergency) vilivyoanzishwa na DAWASCO Kama ilivyo Tanesco? Je unajua wahudumu wa kitengo Cha huduma kwa wateja DAWASCO wapo ofisini kupokea na kukata simu bila kuweka utaratibu wa ufuatiliaji wa Taarifa zinazowasilishwa kwao? Je unajua kwamba watu wanabambikiwa madeni ya maji? Toka ofisini baba utembee ujifunze tunavyoishi Jambo umejitapa wewe ni mtoto wa hapahapa town

5. Je, unajua huduma za afya zinatolewa kwa kila kitu kununua? Unajua mahospitalini private na government tunatibiwa si Kama walipa kodi bali wanyama? Unajua bima ya afya NHIF kwenye hospitali za umma inadharaulika na watumishi wa Umma? Unajua tunauziwa dawa?

Mzee Hali si shwari ujue,toka ofisini washtukize watumishi wako wamelala. Lakini tupe mchongo tutakufikishiaje ujumbe privately? Toka adharani tupe namba tukutupie wanaokudondosha ujadiliane nao ila usiwekeze kwenye utumbuaji maana yawezekana sisi tunaona awatimizi wajibu kimbe ninyi wakubwa ndo amtimizi wajibu kwa kuminya resources.

6. Mzee mkubwa unakubaliana na kinachoendelea stendi ya mabasi, hata Kama Mzee aliyetangulia alifungua milango yakujaza watu ndani mle lakini unao uwezo wakumshauri mama atengue kauli ile ili mpate muda wakuipanga vizuri stend ile. Kwa ufupi inachakaa kabla hata haijaanza kutumika kwa sababu ilizinduliwa kwa ahadi yakuwafurahisha wanyonge lakini wangepaswa kufurahi kwa utaratibu. Lile Ni lango la uchumi liboresheni nakulipangilia, Mzee hakuwa sahihi sana.

7. Hivi Mzee umewahi kuwasiliana na watu wa ardhi wakakuambia kiburi chakuwekea wananchi mawe kwenye mikondo ya maji na kuwapatia hati za makazi wanatoa wapi? Je mvua za mji huu ni ngeni kwako? Nikuombe utoe maelekezo, wananchi wote waliowekewa mawe kwenye mikondo ya maji hati zao za makazi ziangaliwe upya, mnawatia hasara wananchi, ushirikiano wa maafisa ardhi na vishoka unalitia Taifa hasara. Najua ujui ila nalileta mezani kwako.

Kwa ufupi nimeandika mwandiko mbaya ila moja Kati ya haya linaweza kukubakisha hapa mjini au likakuondoa hasa wapiga kura watakapoanza kunyanyua mabango.

TAADHARI: Usitoke ofisini kuja mtaani kwa stayle ya Makonda, toka ofisini jifunze,tafuta solution then tatua changamoto. Usijiingize kutweza utu wa watumishi wako. Shirikiana nao
 
Mwandiko wako umenikumbusha insha yangu niliandika nipo shule nikaipeleka kwa mkuu wa shule ikapitishwa na kuchapwa na mpiga chapa wa shule kisha ikabandikwa kwenye ubao wa matangazo. Ilikua ni insha ya mwaka..! Kila aliyeisoma alitamani na kufarijika, lakini ilikua ni changamoto kwa wahusika kuwajibika. Nakupongeza sana..!!
 

Hii habari imeenda shule na kwa kweli mhusika aipate haraka na kuanza kuifanyia kazi. Hapo pa Ardhi na DAWASCO ni shida. Hivi waziri Ardhi alivyokuwa moto vipi hatumsikii siku hizi?? Ama kweli wengi walikuwa bendera fuata upepo!
Stendi hii wasipojipanga upya muda utaongea.

Asante kwa kuyaleta hapa jukwaani.
Big up!.
 
Back
Top Bottom