Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam awajibishwe kwa hili!

Hivi ule ukaguzi wa nyumba kwa nyumba hapa Dar vipi?? Kwangu hawajafika..............
 
Hizi mada zingine ni chuki tu kwa Makonda.... Hivi foreni katika jiji la dar imeanza kipindi cha makonda? Mbona tangu kipindi cha hao kina kandoro foreni zilikuwepo!
Sisi tunasemea foleni na siyo hizo zako!!!!
 
Mkuu, kwani Dar hali ipoje sasa? Mie naona wanajitahidi sana kwa sasa. Foleni hakuna na wanajitahidi kuwa na bustani katikati ya barabara kuu
Yeye anachokijua ni shisha,unywaji pombe,magasho....

OVA
 
Jiji chaaaafuuu...machinga kila kona...watoto wa mtaani usiseme...miti iliyopandwa imenyauka...cha kushangaza miti iliyopandwa kipindi cha nyuma ilistawi...wamekata wameacha hiyo minazi yao ya kizungu iliyonyauka..
Kutwaaa kwenye media
 
Eti siro anapokea rushwa, hivi anao ushahidi wa hilo, siro akimpeleka mahakamani itakuwaje?
Sirro sio RPC kinondoni,huyo ni Kamishna wa hiyo kanda Ila RPC kinondoni ni SACP KAGANDA,sasa kwa kuwa kazoea kuropoka kama muimba taarabu,acha aendelee
 
Tatizo la wanaoteuliwa hawaelewi mipaka yao kiutendaji Kamishina Sirro kwa kawaida hawajibiki na RC yeye anawajibika moja kwa moja kwa IGP ni pamoja na RPC kiutendaji alipo pale kwa upande wa mkoa ni mshauri katika mambo ya usalama wa kanda kwa kamishina na RPC pia mambo ya utekelezaji yanatoka makao makuu kwa vile kwa misingi ya uteuzi huu wateuliwa hujiona miungu watu kea kukabidhiwa mkoa bila kuelewa mipaka yao ya kazi kuna siku mkuu wa mkoa ataoa amri hata kwa mkuu wa kikosi chochote cha mkoa wake kwa sababu wapo ndani ya mkoa
 
Naelekea kufikiri kuwa ktk kinachoitwa kamati ya ulinzi na usalama, Hali Si Sawia hata kdg. Kitendo cha
Mwenyekiti -Mkuu wa Mkoa, Kuwalalamikia hata kufikia hatua ya kuwaelekezea shutma wajumbe wa kamati yake -makamanda wa vikosi vya ulinzi na usalama ktk Mkoa wa Dar-es-Salaam, shutma za ''hongo'',...ya kuwa ''amewaagiza'' ila ''wanakigugumizi''kuchukua hatua Stahiki za kiutendaji!! Something is terribly WRONG people!!
1.Wamepanga na KUZUNGUMZA NDANI ya vikao imeshindikana....sasa majukwaani.
2.Ni mangapi yaliyopangwa yanaelekea kushindikana?.... Na kwanini?
3.Wana-Dar. na Wananchi kwa ujumla tuwaeleweje kiutendaji Kazi?? Usalama wetu uko Vipi?
4.Je? Ni Dar. Tu au hivi ndivyo hali ilivyo Hata ktk Mikoa yetu mingine Tanzania.... (migogoro ya ardhi ,sisi wakulima na wafugaji/mbuga zetu).

**My take: There's too much Egoism among leaders in this Government... Everybody wants to be seen to be doing something!!!... Otherwise kiongozi unaonekana huendi na kasi ''anayoitaka''Mheshimiwa Raisi. This is wrong!!
Mhe. Raisi viongozi wengi wanafanya Kazi kwa dhana ya woga....wakupendeze wewe zaidi..... Na ili uwasifie!!!!...na ktk dhana hii ya ''bora Punda afe lakini mzigo wa bwana ufike ''....wasaidizi hawa WATAKUANGUSHA MHE. RAISI.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Toa practical solution, vinginevyo you are part of the problem.

Kwanza ahamishe ofisi yake Ubungo atakuwa katikati ya wilaya zote. Halafu na ma DC wake nao watoke city centre. Mahakama zote ziwafuate wananchi waliko na sio kulundikana city centre. Wizara ya ardhi kwa vile inadeal na jiji 80% kulinganisha na nchi nzima nayo ifungue ofisi za kiutendaji kila kata na kule magogoni ibakie coordination tu. Akianza na hayo nafuu itapatikana kwa kuwa 60% ya waendao city centre kwa siku wanapelekwa na shida zao na sio ajira.
 
Huyu kiongozi ameshindwa kabisa kua mbunifu juu ya suala la foleni za magari katika jiji la Dar es salaam.
Tukisema kua huu mkoa ni mkubwa mno sio size yake tunaambiwa ni majungu, lakini mpaka sasa jiji liko shaghala baghala, parking zimezakaa kila kona ya jiji hovyo hovyo, jiji halina pa kupumulia. Mwanzo alikuja vizuri na wazo la kurasimisha maeneo ya maegesho yote ya magari jijini na gereji zote lakini kwa sasa sijui kapewa nini na matajiri!


Dar es salaam ilikua ya Makamba bhana, Dar ilikua ya mzee Kandoro bhana.Hawa ndio viongozi walioacha alama katika jiji la Dar, walikua wabunifu na wachapa kazi na sio hawa wanasiasa wanaojisifia muda wote.Mtu unaacha vipaumbele vya jiji unakimbilia upandaji miti inaingia akilini kweli? Miti ndio kero za wananchi wa Dar?

Huyu ndugu yangu tukubali kua kachemsha sana, size yake ilikua wilaya na sio jjiji, ona hali halisi ilivyo.

Hana ubunifu kwa sababu hana vyeti
 
Huyu Mkuu wa Mkoa Daudi Albert Bashite ni MHALIFU..
Huyu ni mwizi wa Cheti na jina la mtu (Paul Christian), huyu ni Mhalifu wa Taaluma.
Mh RC kumbe na mbwembwe zako zote zile kwanza Ulipata ZERO form4 then UKAIBA cheti cha mtu..
Unawapaka watu ukiwa jukwaani kumbe wewe una gaps kibao kwenye life yako.. SHAME kwako na kwa wanaokutukuza W. J. Malecela
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom