RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda ameagiza mambo matatu wakiwemo ombaomba wa mabarabarani, majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipokuwa na sehemu za kuegeshea magari na wamiliki wa bar kupiga muziki nje ya utaratibu wa vibali vyao.
Mkuu wa Mkoa ametoa siku sita mpaka April 18 ombaomba ndani ya Dar es salaam kuondoka mabarabarani.
Wamiliki wa majengo walipe faini na kuweka utaratibu wa magari wa kupaki wapi magari yao au kubomoa majengo yao.
Kuhusu wamiliki wa Bar mkuu wa mkoa amesema wamiliki wa bar wanaowapigia watu kelele wafuate sheria walizopewa kama ni mwisho saa sita kupiga muziki iwe hivyo na muziki huo upigwe kwenye maeneo husika.
Mtu ambaye anapiga muziki nje ya utaratibu wa kibali chake maana yake ajiandae kunyang’anywa leseni na kufutiwa kibali chake na faini hiyo atailipa mwenyewe.