Mkuu wa Mkoa wa Arusha MULONGO kutofika eneo lilipotokea mlipuko wa Bomu ni sahihi?

sokoinei

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,832
566
Tangia kutokea kwa mlipuko wa bomu hapo jana ktk mkutano wa kampeni wa chama cha Demokrasia na Maendeleo,na kupoteza maisha ya watu 3 huku zaidi ya 60 wakijeruhiwa vibaya,Mkuu wa mkoa Magesa Mulongo ambae ndie mwenyekiti wa ulinzi wa mkoa hakufika eneo la tukio hadi muda huu nikiwa hapa uwanja wa Soweto.

Mkuu wa mkoa akiongea na vyombo vya habari amesema kuwa anasikitika sana na anaona uchungu kwani ni takriban mwezi mmoja tangia litokee tukio lingine la Kulipuliwa kwa bomu ktk kanisa la Katoliki Olasiti tukio ambalo pia liliuwa watu watatu na wengine kujeruhiwa.

Siku ilipo tokea tukio la kulipuliwa kwa waumini wakiwa kanisani Mkuu wa mkoa alikua wa kwanza kufika eneo la tukio.kulikoni leo hii tukio kama hilo hilo limetokea na Mkuu wa Mkoa hakufika ktk eneo husika??
 
Anamuogopa sana Lema
 
unadhani hajui kama atazomewa na isitoshe anaweza kupewa kichapo

Mh! Hata mimi nilikuwa nasubiri kusikia msimamo wa awali wa serikali kupitia kwa Mkuu wa Mkoa.

Kama hajafika eneo la mlipuko wala kuwatembelea majeruhi hospitali inaacha maswali mengi ambayo hayana majibu!
 
Unafiki wa watawala wa tanzania,wana ubaguzi wa hali ya juu,ingekuwa ni msikitini na kanisani tukio hilo limetokea wote wangejikosha huko
 
Kama ni hivyo nazidi kuamini ktk kinachodaiwa ccm wapo nyuma la hili
 
Magessa Mulongo ni miongoni mwa Majanga makubwa tuliyonayo kama Taifa......
Akiongozwa na Jakaya Mrisho Kikwete kama Janga kuu kuliko majanga yote, sad to say!
 
Tunajua mkuu wa mkoa kuna watu hawapendi hata kuwasikia hasa wanafunzi wa vyuo na wanachadema aende akafanye nini
 
Anajua kinachoendelea huyo...anaweza kujichanganya akienda huko..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom