Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa ameshika mkasi baada ya kukata utepe katika uzunduzi wa barabara ya za Jiji la Arusha zinazoendelea kujengwa St.James na Mahakamani, jana Jijini Arusha.
Mbali na barabara, anazindua miradi mingi ya Maendeleo iliyobuniwa na kusimamiwa na Baraza la Halmashauri ya Jiji la Arusha linaloongozwa na CHADEMA wenye madiwani 32, mbunge 1 na CCM yenye diwani 1 tu.
Miradi hii imefanikishwa na Halmashauri ya Jiji inayoongozwa na CHADEMA katika mazingira ya hujuma toka kwa baadhi ya wateule wa Rais na wakati huo huo Serikali Kuu ikiwa imenyang'anya vyanzo baadhi vya mapato ya Jiji na kushindwa kurejesha fedha za maendeleo. Kwa mwaka huu wa fedha unaoisha, Jiji limepata pesa zisizozidi 9% ya kilichokuwakinahitajika.
Ni vyema sasa RC Gambo apitie miradi yote halafu arudi ofisini wajitathmin na nduguze kama vikwazo walivyokuwa wanaweka (bado havijaisha) kwa Madiwani na Meya wao kutofanikiwa kwasababutu ni CHADEMA vina tija kwa Taifa!? Ingekuwaje kama wangewaunga mkono kuletea maendeleo wananchi badala ya kuhujumiana!? Nadhani ataona umuhimu wa kupiga simu Ikulu ili fungu la Serikali Kuu lije kuleta maendeleo badala ya CHADEMA nimewashughulikiaje na Lema wao.
CCM oneni wivu mmependa sana na kutamani CHADEMA wafeli lakini imeshindikana!! Sasa lazima mpite kwenye mema ya CHADEMA kupigia picha.
MAENDELEO HAYANA ITIKADI
_____________
Pichani: Kulia kwake ni DC wa Arusha Mjini Daqarro, Naibu Meya wa Jiji viola Likcy, na Diwani wa Kataya Kaloleni Mzee Kessy aka Mzee wa Nukta.
Meya wa Jiji Mstahiki Kalisti Lazaro yuko ziarani nchini Ujerumani anakowakilisha nchi kwenye mkutano maalumu wa maendeleo na mazingira kwa majiji ya Afrika.