Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, ajutia kuwaweka ndani Watumishi wa Umma bila kuwasikiliza. Ataka Viongozi vijana wajisahihishe

Sevenjr

Member
Aug 3, 2018
32
127
Anaanza kwa kuelezea; "Mwaka 2012 niliteuliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mkuu wa Wilaya na kituo cha kuanzia kazi kilikuwa ni Korogwe.

Wakati huo nilikuwa Kijana zaidi ya sasa. Walimu ni watumishi ninao wapenda sana wakati wote wa Uongozi wangu. Wakati wote wa Uongozi wangu nimekuwa mtetezi wao.

Siku moja nikiwa Wilayani Korogwe nilielekeza niitiwe kikao cha Walimu wote ili niweze kusikiliza changamoto zao ili kwa ushirikiano pamoja na viongozi wenzangu tuzipatie ufumbuzi wa pamoja Kwenye kikao kile kuna Mwalimu alichelewa na alionekana amekunywa kidogo.

Nikamuuliza, Mwalimu kwanini umechelewa kwenye kikao changu? Akaniambia "Mkuu, usinizingue maana mimi nimeshachoka na maisha." Nikamwambia "huna adabu" na kumuagiza OCD amuweke ndani saa 24.

Kama ilivyo kawaida, kesho yake nikaagiza aletwe ofisini ili nimsikilize, akumbuka Mpendwa Mwalimu aliniambia yafuatayo "Mkuu, nihurumie mtumishi wako.

Jana wakati napata wito wako nilikuwa nimemfumania Mke wangu amelala na mwanaume mwingine kwenye kitanda chetu nyumbani.

Sikuona tena thamani ya maisha na nilitamani kujiua Ili kupotezea nikaona bora nijitundike pombe za kienyeji ili angalau nijisahaurishe matatizo."

"Wakati nipo njwii ndio napokea simu ya wito wako,

"Mkuu, Mimi ni wa kusaidiwa na si kuadhibiwa, naomba msamaha".

Kisa cha pili ni "Nilipokua Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma mwaka 2015/2016,

Anasimulia "Siku moja nilimuagiza Mkurugenzi aniandalie kikao cha ghafla cha watendaji wa vijiji na kata.

Kwenye kikao kile watendaji wawili walichelewa kwa zaidi ya masaa 5, nikaagiza wawekwe ndani masaa 24."

Baada ya saa 24 nikaelekeza waletwe ofisini ili nipate utetezi wao.

Mmoja alikuwa ni mtendaji wa Kijiji cha Sibwesa kwenye kata ya Kalya ambako ni Kilomita 422 kutoka makao makuu ya Wilaya ya Uvinza eneo la Lugufu.

Mtendaji kwenye maelezo yake aliniambia "Mkuu nakiri kupokea wito wako wa dharura, lakini kwa masaa 6 nisingeweza kuwahi kutokana na umbali wa Km 422 kutoka kijiji kwangu na makao makuu."

Akaendelea kujitetea "Kutoka kijijini kwangu ambako ni Barabara ya vumbi lazima nipande pikipiki umbali wa Km kama 30 hivi, halafu nipande Boti kisha nipande basi ndio nipate hiace ya kufika Wilayani."

"Kwa hakika hata sikupewa nauli na gharama si chini ya laki moja ambayo ni karibu nusu ya mshahara wangu.

Lakini kwasababu ya wito wa Mkuu nilitumia gharama zangu binafsi na kukimbazana ili niwe nimetii maagizo yako.

Cha kusikitisha nilipofika tu hata kabla ya kunisikiliza ukaagiza niwekwe ndani saa 24."

Akaniambia, "Mkuu mimi nadhani pale ulinionea na ulitumia mamlaka yako vibaya".

Kisa cha tatu "Nilipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma mwaka 2015/2016 nilielekeza Mkurugenzi aniandalie kikao cha haraka cha watendaji wa kata na vijiji.

Kwenye kikao hicho mtendaji wa kata ya Itebula alichelewa kufika kikaoni na bila ya kumsikiliza nikaelekeza awekwe ndani kwa saa 24 kama ilivyo kawaida kesho yake nikaagiza aletwe ofisini kwangu kwa ajili ya utetezi.

Mtumishi yule alipofika ofisini akaanza kujitetea kwa kuniambia "Mkuu, wakati napata wito wa kikao chako nilikuwa hospitali na Mke wangu.

Mke wangu ni mjamzito na alipata matatizo ya Mimba, muda ule napata wito alikuwa chumba cha upasuaji. Kwa kuheshimu wito wako Mkuu nilimwacha mke wangu hospital nikakimbia kuja kwako.

Nilidhani nikifika utanipa pole na kuona nimeheshimu wito wako, badala yake ukaniweka ndani. Leo nimepata taarifa kuwa hali ya Mke wangu na mtoto aliyeko tumboni ni mbaya zaidi.

Mkuu, tukio hili sitalisahau kwenye maisha yangu na mimi nadhani ulininyanyasa na kunionea kwasababu ya unyonge wangu.

Hakika hapa umetumia ubabe na madaraka yako vibaya".

"Kwa hakika nilitamani kulia. Nilijisikia vibaya sana Nilimuomba radhi mtumishi huyu ikiwa ni pamoja na kumrudishia nauli pamoja na mwenzie wa kijiji cha Sibwesa kata ya Kalya."

Kisa hiki ni cha kweli na kilinifanya niache mchezo wa kuwaweka ndani watumishi. Nikaona haja ya kuwasikiliza watumishi kabla ya kuwahukumu.

Mwalimu Nyerere alitunga kitabu cha "Tujisahihishe" ili kuwakumbusha viongozi umuhimu wa kujikosoa.

Anamaliza kwa kusema "Watumishi wenzetu wa chini yetu ni binadamu na Wana changamoto nyingi kama binadamu wengine."

Busara ni kuwapa fursa ya kujitetea kabla ya kuwahukumu.

Hekima ni kushughulikia changamoto zao kwa kufuata kanuni za utumishi wa Umma.

Kupitia kanuni za Utumishi wa umma watapata wasaa wa kujieleza kabla ya kuchukuliwa hatua za "kinidhamu" na "kisheria".

Usione siku hizi siweki watumishi ndani ukadhani sina Mamlaka.

Tena siku hizi mamlaka ni Makubwa zaidi kuliko siku za nyuma, lakini nimetambua kuwa Elimu haina mwisho na nimekubali kujifunza "Uongozi".

Nimeamua kujikosoa pamoja na kufanyia kazi maoni ya wanao nikosoa.

Sisi viongozi vijana bado ni wanafunzi wa Uongozi Kila siku tunajifunza na kupata uzoefu.

"Hakika uzoefu ni mwalimu mzuri!"
 
Gambo umekuwa muungwana, ni ujasiri mkubwa kukiri mapungufu na kutafuta kujirekebisha. Umetenda vyema sana na big up sana, endelea kubadirika for the better mkuu.

Ni kweli mwanzoni ulizingua kwa sababu ulipaswa kumpa mtu nafasi ya kujitetea lakini maadamu hapa unakiri kuwa ulikuwa unakosea basi endelea kubadirika for the better!
 
Gambo umekuwa muungwana, ni ujasiri mkubwa kukiri mapungufu na kutafuta kujirekebisha. Umetenda vyema sana na big up sana, endelea kubadirika for the better mkuu.
Ni kweli mwanzoni ulizingua kwa sababu ulipaswa kumpa mtu nafasi ya kujitetea lakini maadamu hapa unakiri kuwa ulikuwa unakosea basi endelea kubadirika for the better!
Kufanya kosa siyo kosa, ila kurudia makosa.

RC Gambo amekuwa muungana na ujasiri wa kutamka kuwa alikosea sana kuwaweka ndani watu kwa ajili tu ya "kujimwambafai" na kutokana na Power aliyokuwa,nayo, na hivyo ana-confess kuwa hatarudia tena makosa yake

Huo ni uungwana wa hali ya juu sana.

Inabidi pia amueleze na Bosi wake Jiwe afuate nyayo zake, kwa kuwa yeye anawaona watanzania wote kuwa wajinga na wapumbavu na mwenye, akli katika dunia hii ni yeye peke yake!

Anachosahau yeye ni kuwa hataishi milele hapa duniani, sote tumeumbwa na Mungu na sisi ni wapitaji na wote tutaishia kuudongo na kufukiwa. Full Stop.
 
Kama amekiri kweli alikuwa anakosea kwenye maamuzi yake ni jambo zuri sana. Ila kwa haraka haraka nadhani hayuko kwenye mahusiano mazuri na mamlaka yake ya uteuzi, hivyo utu na akili yake halisi inamrudia kwani anahisi mwisho wa nafasi ya kunyanyasa watu unakaribia.
 
Low of natural justice states clearly that no person shall be convicted without given right to defense. Sharia nayo inayompa mamlaka DC kuweka mtu ndani inaweka masharti kuwa lazima mtu anayewekwa ndani ithibitike kuwa anataka kuhatarisha amani.

Sasa mtumishi huyo kuchelewa kikao cha DC amehatarisha usalama upi?! Sheria inamtaka DC baada ya kumuweka ndani ampeleke mahakamani kwa muda uliotajwa na sheria, sasa unamuita ofisi kwako hapo ndio mahakamani?!

Mimi nasema matendo hayo hayana tafsiri nyingine zaidi ya ulimbukeni wa madaraka. Kumrudishia nauli ndio kitu gani, Utu wake je?!
 
Wajuzi wa mambo embu tusaidieni hapa KM 422 ni kama utoke Dar es Salaam mpaka wapi vileee? Huyu Mrisho Gambo mbona kama anatunga story KM 422 zinapatikana ndani ya mkoa mmoja hapa Tanzania kweli!!! na tena wala sio mkoa ni wilaya.
 
Back
Top Bottom