Mkuu wa Mkoa Tabora atoa mwezi mmoja kiwanda cha maziwa kilichofungiwa kijirekebishe

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Mkuu wa Mkoa Tabora Bw. Aggrey Mwanri ametoa mwezi mmoja kwa mmiliki wa kiwanda cha Maziwa cha Tabora kuhakikisha anarekebisha kasoro zilizosababisha kufungwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa mwaka 2016 la sivyo Serikali itakichukua na kumpa mtu mwingine ili akiendeshe.

Bw. Mwanri alitoa agizo hilo jana mjini Tabora baada ya kutembelea Kiwanda ili kujionea mazingira yaliyosababisha kisimamishwe.

Alisema kuwa mara baada ya kipindi cha mwezi kukamilika na kama Mmiliki wake atakuwa ajarekebisha mapungufu aliyoelekezwa na TFDA ayafanyie kazi itabidi apelike mapendekezo katika Wizara inayohusika na Viwanda ili kikabidhiwe kwa mwekezaji mwingine.

Mkuu wa Mkoa huyo aliongeza sanjari na kumwagiza alerebishe kasoro pia alimtaka apelike Mkataba wa Ununuzi wa Kiwanda hicho ili kuona kama anazingatia masharti aliyopewa wakati akikinua mwaka 1998.

Kwa upande wa Meneja wa Kanda ya Magharibi wa TFDA Dkt.Edgar Mahundi alisema kuwa walipofanya ukaguzi katika kiwanda hicho walikuta maziwa yakizalishwa katika mazingira ambayo ni hatari kwa afya ya watumiaji.


upload_2017-8-15_13-38-7.jpeg
 
Duh hivi wakirudisha kiwanda huwa wanachukua pia na installations ambazo mwenye kiwanda kaweka?
 
Ni cha serikali au binafsi, kama cha serikali OK, kama siyo hivyo, maana kwa spidi hii basi kesho tutaambiwa kuwa kama mke hapati mimba watamchukua na kumpa mwanamume mwingine!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ni cha serikali au binafsi, kama cha serikali OK, kama siyo hivyo, maana kwa spidi hii basi kesho tutaambiwa kuwa kama mke hapati mimba watamchukua na kumpa mwanamume mwingine!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Teh! Teh!' Teh ,umenichekesha sana
 
Back
Top Bottom