Mkuu wa Mkoa Tabora amuweka lupango Kaimu Afisa Manunuzi Wilaya ya Sikonge

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Aggrey Mwanri ameagiza kukamatwa na kuwekwa ndani kaimu Afisa Manunuzi Wilaya ya Sikonge, Silvanus Ndilabika kutokana na kuwepo kwa dalili za ufisadi katika ujenzi vituo viwili vya afya.

Mwanri amechukua hatua hizo leo kwenye ziara yake wilayani humo ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya afya mbalimbali ambapo katika ujenzi wa kituo cha afya cha Kitunda imeonekana kuna ufisadi hivyo kupelekea mradi huo kutokamilika kwa wakati.

''Unaona taratibu za manunuzi hazijafuatwa halafu unaongea kwenye kikao changu kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama unaniambia sikiliza unatoa wapi nguvu hiyo hebu mkamateni huyo'', alisema Mwanri.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amewataka watumishi wa umma mkoani humo kuhakikisha wanabaini kasoro za miradi mapema kabla ya kusubiri yeye ndio akabiani hilo.

Mwanri anafanya ziara yake katika wilaya za mkoa huo kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya afya.
 
Kwa hiyo hakutaka ajibu chochote...
Africa bana...watu wanataka waonekane watawala au wafalme
 
Back
Top Bottom