Mkuu wa mkoa Shinyanga imulike Don Bosco-Didia, inarudisha wanafunzi nyumbani wamalize ada ya mwaka mzima ilhali wanatakiwa kulipa ya mhula wa kwanza

tatamajuva

Member
Sep 11, 2019
74
83
Hii ni habari ya kusikitisha Sana kwa uongozi wa Don bosco-didia Shinyanga ukiongozwa na fr OMONDI ambaye ni mkenya kurudisha wanafunzi baada ya kumaliza likizo ya pasaka April 2022.

Kwa taarifa ni kwamba wazazi ambao watoto wao wamerudishwa nyumbani na hivyo kukosa masomo wamelipa Ada yote ya muhula wa Kwanza na hivyo wanaeubiri kumaliza muhula wa pili.

Aidha, fr huyo amekuwa akileta usumbufu mkubwa kwa wanafunzi kwa kusema kwavile yeye ni mkenya na kwao utaratibu wa kulipa Ada nusu muhula haupo ila ni hapa Nchini Tanzania tu.

Sababu nyengine anayowaelekeza wanafunzi hao ni kwamba muhula wa Kwanza utakuwa na likizo ndefu kutokana na sensa hivyo anahitaji walipe Ada yote.

Hii ni ukiukaji wa taratibu za uendeshaji shule zisizo za serikali kulazimisha ada yote ilipwe mwaka mzima.
 
Hii ni habari ya kusikitisha Sana kwa uongozi wa Don bosco-didia Shinyanga ukiongozwa na fr OMONDI ambaye ni mkenya kurudisha wanafunzi baada ya kumaliza likizo ya pasaka April 2022.

Kwa taarifa ni kwamba wazazi ambao watoto wao wamerudishwa nyumbani na hivyo kukosa masomo wamelipa Ada yote ya muhula wa Kwanza na hivyo wanaeubiri kumaliza muhula wa pili.

Aidha, fr huyo amekuwa akileta usumbufu mkubwa kwa wanafunzi kwa kusema kwavile yeye ni mkenya na kwao utaratibu wa kulipa Ada nusu muhula haupo ila ni hapa Nchini Tanzania tu.
 
Hii ni habari ya kusikitisha Sana kwa uongozi wa Don bosco-didia Shinyanga ukiongozwa na fr OMONDI ambaye ni mkenya kurudisha wanafunzi baada ya kumaliza likizo ya pasaka April 2022...
hicho si ni chuo binafsi? halafu wewe unawapangia utaratibu wa kulipa. Umerogwa na nani wewe toa mwanao mpeleke vyo vya serikali teana wametangaza nafasi bure
 
Hii ni habari ya kusikitisha Sana kwa uongozi wa Don bosco-didia Shinyanga ukiongozwa na fr OMONDI ambaye ni mkenya kurudisha wanafunzi baada ya kumaliza likizo ya pasaka April 2022...
...Kama kwao Kenya Hawafanyi Karo Nusu Nusu, SI aende huko? Akija hapa ni lazima afuate Sheria
Wazazi changamkeni!
 
Elimu ni bure mnapeleka watoto kufanya nini uko wakati pesa yako ya kuunga unga, kama kipato chako kidogo acheni sumbua watoto
 
Lipa Ada, wacha blah blah, lipa Ada!
Private institutions hizo, Ada wanategemea kuendesha chuo, wakufunzi walipweje, Ka wewe hulipi Ada, umejipangia
 
Back
Top Bottom