Mkuu wa Mkoa Rukwa: Nataka tuwachome wahalifu, tumechoma sana nyavu ila uvuvi haramu bado unaendelea

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058
Kamishna Mstaafu Zelote amesema hayo wakati akijiandaa kushiriki zoezi la kuteketeza zana haramu zilizokamatwa kupitia doria katika vijiji vya Kabwe, Isaba, Chongokatete, Mandakerenge, Kolwe, Lupata na Kisenga katika wilaya ya Nkasi Mkoani humo, zoezi lililofanyika katika mwalo wa kijiji cha Kirando.



"Kukamata na kuchoma nyavu haitoshi kwa sababu hii inaungua tu, nataka tuwachome wahalifu kwa kutumia sheria. Nimechoma sana nyavu hizi na huu mtindo bado unaendelea, hii haina tija, kila tukichoma madhara yanatokea mazingira yanaharibika. Sasa tuseme basi, ningependa kusikia mhalifu kakamatwa kapelekwa Mahakamani na kupewa adhabu," amesema Kamishna Mstaafu Zelote.

Mhe. Zelote amewaasa watumishi wa idara ya uvuvi ambao wapo chini ya wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini kuachana na kupokea rushwa, kwani jambo hilo linaonekana kukwamisha juhudi za serikali katika kulinda rasilimali zake kwa ajili ya faida ya kizazi hiki na kijacho.

Mhe. Zelote amesema kuwa wananchi bado wanahitaji kuendelea kupatiwa elimu juu ya umuhimu wa kutunza rasilimali na kujulishwa kwamba rasilimali hizo ni za watanzania wote ili waweze kuachana na tabia ya kuvua samaki kwa kutumia zana zisizokubalika.

Kutokana na doria hiyo iliyofanywa na kikosi cha usimamizi wa rasilimali za uvuvi Kijiji cha Kipili kwa kushirikiana na polisi pamoja na kikosi cha jeshi la wanamaji wote wa kipili kuanzia Juni hadi Septemba 2017 waliweza kukamata nyavu zisizokidhi viwango vya serikali zenye thamani ya shilingi milioni 57.6.

Miongoni mwa nyavu zilizokamatwa ni nyavu 32 za Makira (gilinets) zenye thamani ya shilingi milioni 38.4, nyavu za dagaa zenye macho chini ya 8 mm zenye thamani ya shilingi milioni 16.5 na makokoro ya vyandarua yenye thamani ya shilingi milioni 2.7.

Msikilize hapa chini Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akizungumzia zaidi sakata hilo la wavuvi haramu.

Chanzo: EATV
 
Mhh mbona naona kama ametumia lugha nzuri tu kisheria.. Maana naona hapo amesema anataka kuwachoma wahalifu kisheria.. kuchoma hapo imekuwa kama kivumishi.. ila maana yake kubwa ni kufikishwa mahakamani kukiwa na ushahidi wa kutosha ili wahukumiwe kisheria..
 
nyavu.jpg
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafi Zelote Stephen ameionya idara ya uvuvi iliyo chini ya wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini kuhakikisha wanawachukulia hatua wale wote wanaokamatwa na zana haramu za uvuvi na kutangaza hukumu zao na si kuishia kwenye kuchoma zana zao tu.

Ameyasema hayo wakati akijiandaa kushiriki zoezi la kuteketeza zana haramu zilizokamatwa kupitia doria katika vijiji vya Kabwe, Isaba, Chongokatete, mandakerenge, kolwe, lupata na kisenga katika wilaya ya Nkasi Mkoani humo. zoezi lililofanyika katika mwalo wa kijiji cha Kirando.

“Kukamata na kuchoma haitoshi, kwasababu hii inaungua tu, nataka tuwachome wahalifu kwa kutumia sheria, nimechoma sana nyavu hizi na huu mtindo bado unaendelea, hii haina tija, kila tukichoma madhara yanatokea, mazingira yanaharibika, sasa tuseme basi, ningependa kusikia mhalifu kakamatwa kapelekwa mahakamani na kupewa adhabu,” Amesema

Katika kuhakikisha wahalifu hao wanapatika Mh. Zelote amewaasa watumishi wa idara hiyo kuachana na kupokea rushwa, jambo ambalo linaonekana kukwamisha juhudi za serikali katika kulinda rasilimali zake kwaajili ya faida ya kizazi hiki na kijacho.

Amesisitiza kuwa wananchi bado wanahitaji kuendelea kupatiwa elimu juu ya umuhimu wa rasilimali hizo na wajulishwe kuwa rasilimali hizo ni za watanzania wote na hatimae kuacha tabia kuvua samaki hao kwa zana zisizokubalika na sheria za serikali.

Mh. Zelote aliishauri idara hiyo kuwa panapokuwa na zoezi hilo linalofanyika mbele ya wananchi wahakikishe kunakuwa na nyavu halali zinazokidhi viwango vya serikali na kuwaelimisha wananchi tofauti iliyopo ili wasiojua nao wapate kufahamu matakwa ya serikali katika kuhifadhi mazingira.

Kutokana na doria hiyo iliyofanywa na kikosi cha usimamizi wa rasilimali za uvuvi Kijiji cha Kipili kwa kushirikiana na polisi pakmoja na kikosi cha jeshi la wanamaji wote wa kipili kuanzia Juni hadi September 2017 waliweza kukamatanyavu zisizokidhi viwango vya serikali zenye thamani ya shilingi milioni 57.6.

Miongoni mwa nyavu zilizokamatwa ni nyavu 32 za Makira (gilinets) zenye thamani ya shilingi milioni 38.4, nyavu za dagaa zenye macho chini ya 8mm zenye thamani ya shilingi milioni 16.5 na makokoro ya vyandarua yenye thamani ya shilingi milioni 2.7.

Awali akisoma taarifa hiyo fupi ya uteketezaji wa zana haramu za uvuvi kwa mgeni rasmi Afisa mfawidhi idara ya uvuvi kanda ya Rukwa Juma Makongoro alitaja kuwa kuna manufaa mengi yanayopatikana kutokana na rasilimali hiyo ikiwa ni pamoja na watu kujipatia ajira, kitoweo, fedha za kigeni na kuingizia serikali kodi ambayo hutumika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Michuzijr
 
Back
Top Bottom