Mkuu wa mkoa Paul Makonda, na sisi wakazi wa Mpigi Magoe tunaomba utukumbuke, barabara yetu ni mbaya haswa

Avictown

Member
Jan 16, 2018
99
125
Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, kwanza nakupongeza kwa juhudi kubwa ulizonazo katika kumsaidia Mheshimiwa Rais wetu kipenzi Dr. John Pombe Magufuli.

Leo naomba kuja kwako na ombi moja la barabara ya kutokea mbezi mwisho kupitia mbezi high school mpaka Mpigi Magoe. Barabara hii ni kati ya barabara zenye magari mengi katika jiji la Dar es Salaam lakini pia ikiwa na urefu wa takribani kilometer 11 toka mbezi hadi mpigi magoe.

Ukiangalia urefu wa barabara utaona ni jinsi gani wakazi wa huku tunavyopata shida. Wenye magari inafikia kipindi hawaweki magari yao barabarani hivyo kutufanya sisi wananchi wako kwenda makazini kwa mbinde sana. Lakini pia, vijana pale mbezi wametugeuza mitaji yao kwa kutuibia pale tunapokuwa tunagombania magari ya kwenda huko.

Tunakuomba mkuu wetu wa mkoa na sisi pia utuombee kwa Mheshimiwa rais ili atukumbuke kama walivyokumbukwa wananchi wa Goba na Madale. Kama kuna jambo wananchi wa huku wanajutia ni kuendekeza kuchagua watu wasioonekana kabisa kuwatetea wananchi. Lakini mwaka kesho Mungu akipenda wananchi wameahidi hawatafanya makosa kwa kuendelea kuchagua vibaya.

Ni matumaini yangu kuwa Mheshimiwa Mkuu wa mkoa utasoma hapa na utanipatia majibu.

Ni mimi mwananchi wako wa Dar es Salaam
 
harder king

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
3,910
2,000
Hizi mambo za kuandikiwa asome hajazoea subiri akiwa mbele ya waandishi wa habari umwambie!
 
stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
12,155
2,000
Kuna kipindi niliwahi kuishi hiyo mitaa,naijua sana hiyo barabara,na ukiwa na kigari chako cha binafsi utajuta hata kwanini uliamua kuishi huko,kingine ni kuwa hata kama ikitokea wakapitisha Tingatinga huwa haichukui muda kuharibika kwani magari kwenye hiyo njia ni mengi sana...
 
Avictown

Member
Jan 16, 2018
99
125
Kamuombeni John Mnyika mliempa kura zenu awe mbunge wenu mkaacha kumpa wa CCM
Mkuu, Mnyika alishinda lkn si kwamba wa CCM hakupata kura. Maana yake ni kwamba, hata wa CCM pia hii tabu ya barabara inahusu. Usiongee bila kufikiria.
 
mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
29,299
2,000
Kamuombeni John Mnyika mliempa kura zenu awe mbunge wenu mkaacha kumpa wa CCM
Na kodi muwe mnakata kwa wana CCM tu,kwa wapinzani msijipendekeze kuwakata kodi ili wajijengee barabara zao wenyewe.
 
Avictown

Member
Jan 16, 2018
99
125
Kuna kipindi niliwahi kuishi hiyo mitaa,naijua sana hiyo barabara,na ukiwa na kigari chako cha binafsi utajuta hata kwanini uliamua kuishi huko,kingine ni kuwa hata kama ikitokea wakapitisha Tingatinga huwa haichukui muda kuharibika kwani magari kwenye hiyo njia ni mengi sana...
Kwa kweli ni changamoto sana. Wenye magari ya abiria (daladala) huwa wanayaondoa magari yao kuepusha spare za mara kwa mara. Hapo ndo kilio cha kusaga meno kwa wananchi kinapoanziaga. Make unaendaje kazini bila usafiri?
 
ChizzoDrama

JF-Expert Member
Sep 29, 2019
1,249
2,000
Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, kwanza nakupongeza kwa juhudi kubwa ulizonazo katika kumsaidia Mheshimiwa Rais wetu kipenzi Dr. John Pombe Magufuli.

Leo naomba kuja kwako na ombi moja la barabara ya kutokea mbezi mwisho kupitia mbezi high school mpaka Mpigi Magoe. Barabara hii ni kati ya barabara zenye magari mengi katika jiji la Dar es Salaam lakini pia ikiwa na urefu wa takribani kilometer 11 toka mbezi hadi mpigi magoe.

Ukiangalia urefu wa barabara utaona ni jinsi gani wakazi wa huku tunavyopata shida. Wenye magari inafikia kipindi hawaweki magari yao barabarani hivyo kutufanya sisi wananchi wako kwenda makazini kwa mbinde sana. Lakini pia, vijana pale mbezi wametugeuza mitaji yao kwa kutuibia pale tunapokuwa tunagombania magari ya kwenda huko.

Tunakuomba mkuu wetu wa mkoa na sisi pia utuombee kwa Mheshimiwa rais ili atukumbuke kama walivyokumbukwa wananchi wa Goba na Madale. Kama kuna jambo wananchi wa huku wanajutia ni kuendekeza kuchagua watu wasioonekana kabisa kuwatetea wananchi. Lakini mwaka kesho Mungu akipenda wananchi wameahidi hawatafanya makosa kwa kuendelea kuchagua vibaya.

Ni matumaini yangu kuwa Mheshimiwa Mkuu wa mkoa utasoma hapa na utanipatia majibu.

Ni mimi mwananchi wako wa Dar es Salaam
pongezi kwa makonda anafanya kazi kubwa
 
BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,505

Kwaniii HUKO n DAR ES SALAAM??
 
Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
15,427
2,000
Kamuombeni John Mnyika mliempa kura zenu awe mbunge wenu mkaacha kumpa wa CCM
Hapa umekosea mkuu,hii ni Tz ya watu wote,eneo kuwepo na Mbunge wa chama A au B haimaanishi wanakosa haki ya kuhudumiwa,umecomment bila kufikiria maana mpiji kuna wanaCCM pia
 
Pakawa

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
6,752
2,000
Uchaguzi unakaribia wataanza na kelele oh tutawajengea barabara oh hospitali clinic shule nk kwani halmashauri kazi yao nini mipango miji nk
Barabara zijengwe kwani ni pesa yetu msitulaghai wachumia tumbo. Mji unajengwa kiholela barabara hazipitiki Changanyikeni Makongo juu Goba barabara miaka nenda rudi
 
msafwa93

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,674
2,000
Mkuu wa mkoa anaijua DSM yake yote, hivyo nilivyomwandikia yeye amepajua tayari.

Makalio kweli wewe, Sasa kama nia ni mkuu wa mkoa pekee si ungemuandikia email, au Dm kule instagram, au si uende ofisini kwake.?

Una uhakika gani yupo humu au aliwahi kusema anaingiaga humu kwani.?
 
Avictown

Member
Jan 16, 2018
99
125
Makalio kweli wewe, Sasa kama nia ni mkuu wa mkoa pekee si ungemuandikia email, au Dm kule instagram, au si uende ofisini kwake.?

Una uhakika gani yupo humu au aliwahi kusema anaingiaga humu kwani.?
Daaaa, sasa matusi ya nini mkuu? Ndo ulivyofundishwa na wazazi wako? Umekosa adabu wewe. Mimi nakuacha, lakini hutatoka humu duniani bila kupata adhabu yako ya matusi kwa watu usiowafahamu. Endelea tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom