Mkuu wa Mkoa Paul Makonda ahudhuria Ibada KKKT Kimara; hataruhusu Dar kuwa lango la Madawa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Heshima kwenu wakuu,
Screenshot from 2017-03-05 10-36-22.png

Karibu kwenye Ibada ianyoendelea hapa Kimara. Ibada ni nzuri sana na utukufu wa Mungu umetamalaki. Mkuu wa mkoa wa Dar kaungana na sisi kwenye hii ibada, ameguswa na ibada hadi kuishiwa nguvu za kusimama na kuamua kukaa na kuanza kumlilia Mungu aliye hai.
Screenshot from 2017-03-05 10-34-05.png

Tunaamin leo atatoa neno na kujibu mashambulizi yanayoelekezwa kwake. Nakemea hila za shetani zishindwe kwa jina la Yesu. Mungu atazidi kumpigania kwani hakuna mkamilifu hata Mmoja duniani.

======

Update;

======

Ntatoa Update kwa Ufupi kile Mkuu wa Mkoa anachosema...

=> Hata nikiwa Mkuu wa mkoa kwa siku moja inatosha, kuwa mkuu wa mkoa sio tatizo, tatizo ni naikamilishaje kazi ya Mungu aliyonipa hapa Duniani.

=> Hapa tupo kwenye vita, Vita tuliyonayo sio ya ulimwengu wa Mwili bali ulimwengu wa roho, vita hii haipiganwi kienyeji, vita hii inatakiwa uwe umekaa sawa sawa. Hii kitu watu hawawezi kunielewa.

=>Akili zake Mungu ukizitazama katika akili za kibinadamu huwezi kuzielewa.

=>Rais wangu Magufuli anacho hangaika ni kuhakikisha hakuna mtoto hata mmoja, hawezi kutoa elimu bure kuanzia shule ya Msingi hadi sekondari, Hawezi weka sheria bodi ya Mikopo kuwawezesha watoto wasoma kwa mkopo wa kodi ya serikali halafu watoto wakaendelea kuwa wavuta bangi na kutumia madawa ya kulevya, rais gani atakaye vumilia hilo?, Mzazi gani mwenye akili timamu atakaye chekelea hilo? Kiongozi gania mwenye ufahamu wa kimungu atakaye furahia hilo?

=>Basi leo eti wanapambana na Makonda, wamesahau hii vita ni kwa jili ya bwana, kama hawajui wamuulize Gidion atawapa stori. Hata jeshi lao lilivyozidi kuwa kubwa Mungu akamwambia embu sikiliza bwana, hili jeshi unalokwenda nayo sina uhakika nayo ebu wapeleke kwenye ule mto wanye maji tuone wanakunywaje, watakaokunywa tofauti tutawaweka pembeni nataka watu wachache ntakaokwenda nao watakao simama upande wangu, Mungu hahitaji watu wengi. Akiamua kazi yake hata Punda ataitekeleza.

=>Vita tuliyonayo wapendwa katika bwana ni kati ya mauti na uzima, Vita tuliyonayo ni kati ya haki na dhuruma, vita tuliyonayo ni kuhakikisha kumtoa mtoto wa mtu fulani kwenye makucha ya shetani na hii kazi Yesu kashaifanya. Nikukubmushe? kutaka kukumbuka kaifanya wapi soma alikuja kufanya nini. Na alieleza shetani ni baba wa uongo anafitinisha, anachonganisha, anaharibu, anateketeza na anaua. Lakini Yesu alikuja kurejesha kilichopotea mahala panapositahili kuwa. Ndo kazi anayoifanya rais Magufuli ndo kazi tunayoifanya wasaidizi wake. kurejesha kilichokuwa kimepotezwa kimetekwa.

=> Sijui kama watu wanafahamu, unakuta watu wamejichoma sindano moja watu ishirini, wengine matumbo yao yameharibika kwani wamebeba madawa mpaka wamepasuka wengine wamekufa. Tanzania kupitia dar ndo ilikuwa ni Mlango wa madawa ya kulevya. Ndo maana lugha inakuwa ni ngumu sana watu wengine kuelewa. Tusiumizwe na maneno ya watu hizo ni dalili tu ya kwamba kazi tunazozifanya katika ulimwengu wa roho zinalipa.

=> Hakuna aliye mcha Mungu anayeweza kuacha kusimama katika hili ambalo rais wetu ametuelekeza akabaki kupia kelele hizi ndogo ndogo.

=> Wameenda sasa wameshafika mbali, hata Mke wangu wanamshambulia, wanasema sio raia.

=> Mkoa wangu unachangia 17% na hakuna mkoa mwingine unaokusanya 17% Tanzania na 80% ya mapato yanayokusanywa TRA yatoka Dar. Dar ndo lango la uchumi. Lakini watu wanataka dar iwe lango la kusambaza dawa za kulevya. Uchumi wa kuua ndugu zetu na kuwangaamiza.

=> Mcha Mungu gani anaweza akakaa kwenye mkoa kama huyu halafu akaruhusu eti madawa yapite halafu aendelee kujiita anamtumikia Mungu. Mcha Mungu gania anaweza kuruhusu Maovu yaendelee kutawala katika mkoa wake halafu aendelee kujiita mcha Mungu?

=> Nikasema nikimuona, sitakaa kimya, wala sitaruhusu chombo kikatize katika anga la utawala nililopewa. Biblia inasema nimeketishwa katika naye kwenye ulimwengu wa roho, ninafanya kazi kutoka kwenye kile kiti. Soma Waefeso. (Waefeso 1:20-21 Kwahiyo, sisi pia tumeketishwa mahali alipoketishwa yeye, katikaulimwengu wa roho, juu sana kuliko falme na mamlaka za giza; ilituweze kuvunja na kuharibu kazi za shetani duniani.)

=> Wakati ndo sasa wa kutangaza jina lipitalo majina yote nalo ni jina la Yesu. Ntasimama hadi dakika ya Meisho na ntasimama kuhakikisha jina lipitalomajina yote jina yesu Kristo mwana aliyehai linahimidiwa.

makonda+chozi_1.jpg
 
Back
Top Bottom