DodomaTZ
Member
- May 20, 2022
- 71
- 107
Miezi minne tangu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel aagize wanawake, vijana na wenye ulemavu waliotokomea na Shilingi bilioni 4.9 za mikopo ya halmashauri kuzirejesha tayari shiingi bilioni 1.45 zimerejeshwa na vikundi hivyo.
Gabriel alitoa agizo hilo Aprili 25 mwaka huu huku akisema Sh4.9 bilioni ziliyodaiwa kutojulikana ilipo ni sehemu ya Sh8.9 bilioni zilizotolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika halmashauri nane za mkoa huo.
Gabriel amewaambia waandishi wa habari kuwa kurejeshwa kwa fedha hizo kumechangiwa na ufuatiliaji uliofanywa na kamati aliyoiunda kufuatilia suala hilo na utoaji wa elimu kwa wanufaika juu ya faida za kukopa na kurejesha fedha hizo.
Amesema kasi ya urejeshaji wa fedha hizo inaridhisha na kuwataka wasimamizi wa ukopeshaji kutorudia makosa ya ukiukwaji wa kanuni, sheria na taratibu za utoaji fedha hizo katika mwaka huu wa fedha ili walengwa mahususi ndiyo wanufaike.
"Ni mapinduzi makubwa na mwelekeo chanya kwamba vikundi vimeanza kurejesha baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa zaidi ya miaka mitatu, twende kwa kina tusirudie makosa fedha hizi ziende kwa makundi yaliyokusudiwa," amesema Gabriel.
Ameongeza; "Kuna vikundi vimeitwa lakini havikufika tunavipa muda kuanzia wiki ijayo nitaanza kukutana na vikundi ambavyo havijaanza kabisa kurejesha ili kuhakikisha fedha zote za marejesho zinarudi na kuingia kwenye mzunguko ili kuikomboa jamii yetu na kuleta matokeo chanya,"
Pia amevitaka vikundi ambavyo vilihama Mkoa wa Mwanza vikiwa vimeshakopa fedha hizo kuzirejesha mara moja huku kamati zikipaswa kuendelea kufuatilia maboresho ili masharti na kanuni yazingatiwe fedha hizo zilete matokeo chanya.
Baada ya kurejeshwa kwa kiasi hicho cha fedha mkoa huo unakuwa na kiasi cha shilingi bilioni 2.37 ambazo ziko tayari kwa kukopeshwa ambapo vijana na vikundi vyenye ndoto na malengo vimetakiwa kujitokeza kuandaa maandiko mradi kupata fedha hizo ziwaletee mapinduzi na siyo kuishia kuzitafuna.