Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,265
- 105,431
Tuliondoa jeshi katika siasa.Wanapoteuliwa huwa tunasikia wamestaafu jeshini. Jana nimeona kwenye TV mkuu wa mkoa wa mpya mmoja akiwa amevaa sare za jeshi la wananchi kwenye shughuli zake za ukuu wa mkoa. Je hiyo ni sawa? Kama hajastaafu jeshini anatumikaje kwenye shughuli za kisiasa akiwa na cheo chake cha jeshini na sare zake? Ni kueleweshwa tu wakuu
Wanajeshi waliokuwa na nafasi za kisiasa kina Kikwete, Makamba Sr, Chiligati, Mkuchika wakastaafu jeshini na kuendelea na siasa kama wanajeshi wastaafu.
Magufuli karudisha siasa jeshini. Wanajeshi wanateuliwa vyeo vya kisiasa bila kustaafu.
Kuna siku wengine watakitaka kile cheo kikubwa kabisa cha kisiasa, urais, kwa kupindua nchi, watakichukua.
Ushawaambia kufanya siasa ni sawa. Siku ukijisahau kuwakaripia karipia hadharani wanakupindua tu.
Hamna jinsi hapo.
Hizi kanuni nyingine kama "civilian control of the military" zina maana sana. Magufuli amazivunja bila weledi.