Mkuu wa Mkoa Mtwara atunukiwa Nishani na Papa Benedict XVII

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,724
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Kanali(Mst) Joseph Simbakalia ametunukiwa Nishani na Papa Benedict XVI baada ya kuteuliwa na Kanisa Katoliki Tanzania kuwa ndiye Mlei bora kabisa kwa mwaka huu 2011!

Hongera Mh.Mlei J.Simbakalia...Naamini kabisa kuwa hujapendelewa na mtu, bali utendaji na uumini wako safi. Mungu akusimamie.

Chanzo: Askofu mkuu wa Jimbo la Tabora, Paul Ruzoka, wakati akitoa matangazo baada ya Misa kuu ya Krismas iliyofanyika kitaifa mkoani Tabora.
 
Bwana Pakajim,

Mimi pia nimesikia, lakini jina ni hilo kweli na zawadi ni ya Gregori Mkuu... lakini je, si Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kweli? Vyovyote vile, lakini Nishani hii imeenda kwa Mlei huyo.

Sasa niulize SIFA ZAKE NI ZIPI?
 
Hongera zake. Ila kumbukumbu zinaonesha huyu hajawahi kuwa mkuu wa mkoa wa tabora. Mara ya mwisho nadhani alikuwa mkuu wa mkoa wa kigoma. Anyway mkoa siyo issue sana
 
Bwana Pakajim, Mimi pia nimesikia, lakini jina ni hilo kweli na zawadi ni ya Gregori Mkuu... lakini je, si Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kweli? Vyovyote vile, lakini Nishani hii imeenda kwa Mlei huyo. Sasa niulize SIFA ZAKE NI ZIPI?
Sielewi una maanisha sifa za upande gani. Lakini kwa hii nishani aliyopewa na Pope sifa kuu ni kuishi maisha yanayokubalika kwa mlei. Mlei ni mkristu yeyote, tofauti na wale wenye daraja maalum katika ngazi za kanisa katoliki., au kwa ufupi ni mkristo wa kawaida.

Hivyo naamini sifa yake mojawapo ni kuwa anaishi kwa uaminifu na usahihi maisha yale ambayo yanampasa muumini wa kawaida.
 
hongera zake!!kwa tanzania ya leo kumpata mtu mwenye cheo kuishi kwa maadili ya dini ni very rare.
 
hongera zake!!kwa tanzania ya leo kumpata mtu mwenye cheo kuishi kwa maadili ya dini ni very rare.

Utafiti wao juu ya waliomteua una walakini; huyu bwana alituibia sana mali zetu alipokuwa NDC, pamoja na kujiuzia nyumba kwa bei ya kutupa!!
 
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Kanali(Mst) Joseph Simbakalia ametunukiwa Nishani na Papa Benedict XVI baada ya kuteuliwa na Kanisa Katoliki Tanzania kuwa ndiye Mlei bora kabisa kwa mwaka huu 2011!

Hongera Mh.Mlei J.Simbakalia...Naamini kabisa kuwa hujapendelewa na mtu, bali utendaji na uumini wako safi. Mungu akusimamie.

Chanzo: Askofu mkuu wa Jimbo la Tabora, Paul Ruzoka, wakati akitoa matangazo baada ya Misa kuu ya Krismas iliyofanyika kitaifa mkoani Tabora.

To me,there is something behinde hidden.
 
Utafiti wao juu ya waliomteua una walakini; huyu bwana alituibia sana mali zetu alipokuwa NDC, pamoja na kujiuzia nyumba kwa bei ya kutupa!!
Bulesi,
Aliiba specifically nini akiwa NDC?...au ndo generalization ya mtu akiwa kiongozi mwandamizi?
Suala la kununua nyumba halikuwa conceived na yeye personally, bali ilikuwa ndio sera ya wakati huo wa Mkapa.
 
Jamaa aliingia mikataba hewa na kampuni ya South Africa ili kuzalisha umeme wa makaa ya mawe huko mchuchuma; fedha nyingi zilitumika but nothing came out of it!! Sawa hiyo ilikuwa policy ya kununua nyumba enzi ya Mkapa lakini sio kwa bei sawa na bure tena sehemu maarufu.
 
Hana harufu ya ufisadi kama wanasiasa wengine? Au waliomteua waliangalia tu cheo cha uzee wa kanisa (ulei) na mahudhurio ya kanisani tu, bila kugeuza upande wa pili wa shilingi?
Kama hana harufu za ufisadi basi nampongeza.
 
Jamaa aliingia mikataba hewa na kampuni ya South Africa ili kuzalisha umeme wa makaa ya mawe huko mchuchuma; fedha nyingi zilitumika but nothing came out of it!! Sawa hiyo ilikuwa policy ya kununua nyumba enzi ya Mkapa lakini sio kwa bei sawa na bure tena sehemu maarufu.
Naomba nisahihishwe iwapo naelewa ndivyo sivyo!

Hivi Mkuu wa Mkoa ana jeuri ya kusaini mkataba mkubwa namna hiyo na Wawekezaji?...Au hata kama by then alikuwa Mkurugenzi, i dont think that he had guts to do so!
Labda unipe ufafanuzi broda!

Kuhusu sual la bei ya nyumba, unawezaniambia ni nani aliyenunua nyumba zile kwa bei ya juu, kwa maana ya bei ya soko?, regardless ya eneo ilipo nyumba?
 
Amepeleka mchango wa fedha kiasi gani kanisani..that is criteria
Acha ndoto weye?
Ni Wakristo wengi mno wakatoliki wamebarikiwa na fedha na vyeo kumzidi sana yeye kwa mbali, bado unaiamini kauli yako?
 
Acha ndoto weye?
Ni Wakristo wengi mno wakatoliki wamebarikiwa na fedha na vyeo kumzidi sana yeye kwa mbali, bado unaiamini kauli yako?

Yeye amewazidi kwa kiasi alichotoa kanisani.. mchango wa fedha ni criteria hasa pesa za umma alizopeleka kanisani...
 
Nampa ongera.huyu jamaa upande dini hasa rc amejitoa sana kushiriki arambee za ujenzi wa shule za sekondari zinazoendeshwa na rc.mwaka juz nikiwa kasulu alifanikisha ujenzi wa sekondary ya st. Francis.ameudhuria arambee pale,aliwai kutwambia atajitoa ili shule hiyo iwe mfano.nilikuwa kwenye kamat ya ujenz na alifanyakaz kubwa sana, michango yake ya mawazo ilisaidia.waha tu wagumu kutoa michango.mh ruzoka ni askofu mkuu,maana yake anasimamia dayosisi ya kigoma na tabora.nafikiri ata mageuz kupata mabunge wanne wa upinzani ni yeye.huyu hataki unafiki.kati ya wakuu wa mikoa walio wahi kukaa kgma waha wamemkubali sana.
 
Back
Top Bottom