Mkuu wa Mkoa mteule wa Dar, Karibu utekeleza haya yaliyomshinda bwana yule mtumbuliwa, usidandie usichotumwa na bosi ,tunataka maendeleo ya dhati

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Karibu mkuu wetu mpya , karibu kwa bashasha, tutakuunga mkono katika kazi zako ili ututendee haki kwa walichokutuma utufanyie.

Katika hotuba za K.M. ndg HP na KM Bashiru kuna jumbe mbali mbali kama maono ya kina yakilenga kuwaasa vijana kutomaliza kazi walizotumwa badala yake kudandia kazi za siasa wakati wenye kazi zao wapo.

Kwanza Dar kuna matatiizo mengi haihitaji shule kuyajua. Ni ya muda mrefu hayajatatuliwa.

Mpangilio wa machinga: wafanyabiashara hawa mbali na kupendwa Serikali imeshindwa kuwaweka kwenye mpangilio sahihi.
Wamejaza sehemu isiyoruhusiwa had I kwenye mwendokasi na transformation

Huduma ya Usafi; hii imefeli kabisa, kwenye vituo vyote vichafu.

Sehemu zilizotengwa kufanyia michezo bado kuna magereji.

Maduka mengi bado wanauza bidhaa feki.

Machangudoa sehemu nyingi wanazidi kupanua wigo ya kusurubu wa kwale.

Vyuma vilivyowekwa kama urembo vimeibwa , mifuniko ya maji taka pia.

Miti iliyopandwa kwa mbwembwe yote imekauka.

Mashulee, machinjo, hospital zote za Dar bado hazijakamilika kwa wakati.

Hii yote ni kwa sababu za kuacha ulichotumwa kuwainua wananchi na kudadia usiyotumwa ASA ya kisiasa na mengine ya kijinsia yasiyotatulika bila nguvu za kimahakama.

Hima fuata maelekezo ya bosi wako kama alivyokueleza kwenye hotuba yake.

Maendeleo hayana vyama fanya kazi bila upendeleo. Tunakutakia huduma njema. Karibu dar bila ya mihemuko ya kisiasa.
 
Jamaaa ni jembe aje huku tutampa kula zetu maana kigamboni inachangamoto nyingi sana hasa maji shule za msingi ni chache maana watu wanahamia wengi sana pia hata mabarabara ni mabovu sana
 
Jamaaa ni jembe aje huku tutampa kula zetu maana kigamboni inachangamoto nyingi sana hasa maji shule za msingi ni chache maana watu wanahamia wengi sana pia hata mabarabara ni mabovu sana
Huyu awezi kitu, ameshindwa Kumaliza hospital ya kibamba, ya bunju machinjio ya vingunguti
 
Huyu jamaa sawa ana mapungufu yake ila tumpe kigamboni tuone maana kigamboni ni wilaya mpya kwa sasa huyu tukimpa ni mtu anafuatilia sana anaweza akaharakisha maendeleo labda nae aje atuangushe
Hu kama Mwananzila was Tabora tuuu
 
kama anataka kuongoza mkoa huu kwa mafanikio basi lazima ajifunze kuwa mkali/makemeo ya haraka, na awe na uwezo wa kuchukua hatua kwa haraka na kwa wakati, lkn kubwa zaidi anapaswa kusimamia miradi yote kwa karibu zaidi maana wapigaji wapo wanazengea .
 
Tunaomba muongeze Ussuri unaofaa hili atutendee haki. Hili jiji liliachwa pasipo mpangilio kwa muda
 
Huyu jamaa sawa ana mapungufu yake ila tumpe kigamboni tuone maana kigamboni ni wilaya mpya kwa sasa huyu tukimpa ni mtu anafuatilia sana anaweza akaharakisha maendeleo labda nae aje atuangushe

Kajikumbushe kazi na majukumu ya mbunge.
 
Tatua usafiri wa mwendokasi haufai na haukidhi mahitaji na wingi wa wananchi.

Eneo la mbweni kuna mafuriko ya jabu mpaka barabara hazipitiki tunashindwa kuelewa fedha za Dmdp zimeshindwa kujenga miundombinu ya mifreji mikubwa ,mitaro pamoja na barabara haswa maeneo ya malindi, teta na ubungo.
 
Kweli haya ndio matatizo. Nakumbuka kuna hela ilitolewa kuamisha madimbwi chasimba na ddawasco ikaliwa chini ya makonda akiwa mkuu was wilaya
 
Jamaaa ni jembe aje huku tutampa kula zetu maana kigamboni inachangamoto nyingi sana hasa maji shule za msingi ni chache maana watu wanahamia wengi sana pia hata mabarabara ni mabovu sana
Atajenga na kutekeleza hayo kwa pesa zake za mfukoni?
Kuna kumpa tu "kula" pia kuna kumpa "kura!"
 
Back
Top Bottom