Mkuu wa Mkoa Morogoro aagiza kukamatwa mwalimu aliyepokea mshahara bila kufanya kazi

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Stephen Kebwe ameamuru kukamatwa kwa Mwalimu Hamisi Salumu Mkoleme kwa tuhuma za kulipwa mishahara ya mwaka mmoja na nusu bila kufanya kazi katika kituo chake alichopangiwa baada ya uhamisho kutoka mkoa wa Tanga kwenda mkoa wa Morogoro, bila kuripoti katika kituo alichopangiwa.

Akizungumza na walimu waliofika katika ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Mvomero ili kuhakikiwa Mkuu huyo wa Mkoa wa Morogoro Dokta Kebwe Stephen Kebwe ameitaka kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Mvomero kusimamia kwa ukamilifu zoezi hilo ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wenyewe kutoa ushirikiano katika zoezi hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa amesema wameamua kuchukua hatua za kupitia upya orodha aliyokabidhiwa na Halmashauri ili kujiridhisha na kwamba iwapo itabainika mwalimu yeyote amefanya kosa kama hilo, hatua kali zitachukuliwa.
 
Hivi ni lini hawa wakuu wa mikoa watakuwa bize na shughuli za maendeleo, maana shughuli ya kudili watumishi hewa ni endelevu (iwe kwenye ratiba kila baada ya muda fulani wanahakiki upya) so waachane nalo waangalie mambo mengine ya msingi yatakayo boresha maisha ya wananchi kwa ujumla.
 
Wewe nyumbu tulia dawa ikuingie,
Kuziba mianya ya upotevu Wa mapato ni shughuli ya maendeleo pia.
 
Wewe nyumbu tulia dawa ikuingie,
Kuziba mianya ya upotevu Wa mapato ni shughuli ya maendeleo pia.
Hivi hamuwezi ku- reply kwakutumia hekima na kuja na hoja za kujenga Taifa , mnafikiri kila member wa JF mwana CCM na CDM. Najua mnapenda sana sifa kuliko kupewa ushauri ambao mtu mwenye hekima atausoma na kuutafakari. Sorry najua mmnapenda hadithi hizi "serikali imeshushwa kutoka mbinguni na imepakwa mafuta na muumba hakuna zaidi yao, na mahakama ya fisadi ndio nyumba yakudumu ya Edo" - hapo umefurahi?
 
Kupambana na ufisadi ndio msingi /foundation ya maendeleo.

Nchi zote zilizoendelea zilifanikiwa sana kupiga vita rushwa na ufisadi.

Kwa hiyo nyinyi nyumbu mnapopinga wala rushwa na mafisadi wasipelekwe mahakamani ,mnasikitisha sana.

Mlaaniwe kabisa
 
Back
Top Bottom