Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, tusaidie kuondoa kelele za muziki wa bar karibu na makazi ya watu

JBITUNGO

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
1,356
608
Imekuwa ni kawaida sana katika mitaa mingi hapa Dar es Salaam kuanzisha Bar zinazopiga muziki kwa sauti ya juu. Mimi sio mtalaamu wa sauti lakini kitendo cha "mabaa" yaliyo karibu na makaazi ya watu kupiga muziki kwa sauti kubwa bila kujari usumbufu wanaosababisha HAIKUBALIKI.

Naomba kuchukua fursa hii kumuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja idara ya afya katika kata zetu kuingilia kati. Makele na miungurumo ya muziki ni kero mno.

Nafahamu watu wa "mabar" wanatumia njia ya kupiga muziki wa sauti kubwa kama njia ya kuwavuta wateja wao. Lakini wanashindwa kufahamu kwamba muziki wa sauti kubwa ni kero kubwa kwenye makaazi ya watu wanaozunguka. Kama mwenye bar anataka kupiga muziki kwa sauti kubwa ni jukumu lake kutengeneza utaratibu wa kuhakikisha sauti ya muziki wake haiwi kero kwa majirani zake.

Nimechukua njia hii ya kufikisha ujumbe kwa idara zinazohusika kwa sababu wananchi wengi wanashindwa kulalamika kwa kuongopa nguvu za wenye "mabar".

Kama njia ya dharura, nichukue fursa hii kumuomba IGP Sirro kutumia vijana wake wa patrols kuwachukulia hatua mabar yote yanayopiga muziki kwa sauti kubwa kwenye makaazi ya watu.
 
Fuata protocal anzia kwa balozi wako, panda mpaka kwa mwenyekiti wa mtaa alafu ndiyo usonge mbele zaidi.
 
Hii kitu inasumbua sana hasa ukiwa na mgonjwa nyumbani na pia agusie jambo la matumizi na uuzwaji wa Shisha.

Shisha inauzwa kwa kasi sana hapo mjini.

Kama lilikuwa agizo la serikali basi msimamo ubaki vile vile.

Kama lilikuwa agizo la aliyepita basi aweke wazi pia.
 
Back
Top Bottom