mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,763
- 35,201
Wajuzi watuambie hili la mchanga lina maana gani😥😥😥😥😥
Aendelee kulala salama Maalim Seif Sharif Hamad
===
Katika hali ya kustaajabisha inadaiwa kumeibuka watu ambao wanachukua mchanga katika kaburi la Hayati Maalim Seif. Baadhi ya wakazi wameeleza kuwa mchanga huo unachukuliwa kwa imani tofauti tofauti. Aidha wapo wanaodai kuwa mchanga huo unanukia harufu ya Miski.
Katika kufafanua zaidi tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Bi Salama Mbarouk Khatibu amewaonya watu wanaochukua mchanga huo. Katika hili amesema Watu wanachukua mchanga waendelee kuzuiwa kwa sababu hatujui wanapochukua mchanga huo wanaenda kuufanyia nini.
Naye, RPC wa Kaskazini Pemba Juma Sadi Khamis ameonya kwamba watu wanaokuja kufanya dua wanaruhusiwa isipokuwa hawatakiwi kuchukua mchanga huo. Amesisitiza kuwa mtu akifanya hivyo itakuwa ni kosa.
Pia soma > TANZIA - Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad afariki dunia