Mkuu wa Mkoa ataka Tume ya Uchaguzi ya Chuo ivunjwe

kingfish

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
571
159
Mkuu wa mkoa wa iringa ameagiza wajumbe wa tume ya uchaguzi chuo kikuu cha ruaha(ruco) kujiuzulu.tume hiyo iliundwa ili kusimamia uchaguzi wa serikali ya wanachuo ya ruco utakaofanyika baadaye mwezi huu.wanachuo wameshangazwa na hatua ya mkuu wa mkoa kuingilia mambo ya ndani ya chuo.wanachuo wanadai kuwa tume hiyo iliundwa kwa mujibu wa katiba ya serikali ya wanachuo wa ruaha university college(rusco) na ilipitia michakato muhimu kama vile wajumbe kula kiapo.
Source:radio-ebony,asubuhi hii.
je,mnakubaliana na hatua ya huyu mkuu wa mkoa?
 
Jana principle alifanya kikao na huyo mkuu wa mkoa,na ajaenda hakujulikana.kifupi wanataka kuweka ccm.kweli amechefua
 
Komaeni makamanda, sie huku saut-mwanza tulikomaa mpaka kikaeleweka. Mkuu wa mkoa lini na wapi akahuska na Serikali ya wanachuo? Aende zake akahimize maendeleo,kilimo na pembejeo.
 
Mkuu huyo wa Mkoa tayari anajikaribishia utata wa kisheria hadi hapo hivyo huenda akahitajika kujitokeza mahakamani kutetea msimamo wake huo dhidi ya autonomous body kama hiyo ya RUCO.

Pili, hili lina maana kwamba hivi karibuni kutapatikana VIONGOZI PANDIKIZI kuwaongozeni chuoni hapo kwa matarajio ya kupunguza ushawishi wa CHADEMA na kukifufua uwepo wa Chama Cha Mafisadi, mpende msipende. You guys, watch out for this CCM machinisation on the offing.
 
ni mmoja kati ya wajumbe wa serikali ya wanafunzi??
Iyo Mandate kapata wapi??
Father Mgimwa utajitia aibu ukifanya maamuzi kwa kuendeswaha na kada huyu wa CCM.
Sitashangaa sana Haule akiridhia amri hii ya mkuu wa mkoa kwani ni mtu wa kujipendekeza.
 
kwa nini mkuu wa mkoa anaingilia mambo yasiyomhusu?na uongozi wa RUCO upo kimya tu hautaki kukemea hili swala-au hao wakuu wa ruco nao ni vipandikizi wa wafanyabiashara na wanasiasa?mbona wanaburutwa utazan hawajasoma-kama wasomi na walimu wao wanaweza kuwa infiltrated kiasi hiki,je wale wazee wa vijijini si ndo watawageuza hawa wafanyabiashara na wanasiasa miungu watu
 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa jana alikwenda RUCO (Ruaha University College) na kumwita Mwenyekiti pamoja na wajumbe wengine wa Tume ya kusimamia Uchaguzi wa Serikali ya Wanafunzi (RUCSO) akitaka ivunjwe, kwani imekaa ki- CHADEMA. Lengo lake ni kutaka kuweka kada wa CCM.
 
Mbona ruco asilimia 80 ni chadema, hapo wanatapatapa tuu. Pia tangu lini mkuu wa mkoa akaingilia mambo ya vyuo? Au ndo maagizo mapya kutoka ikulu
 
Naamini ni harakati za kufufua/ kuimarisha chama, japo inaweza kuwa ngumu kutokana na chuki iliyopo dhidi ya CCM.
 
hivi hii nchi inaelekea wapi? Mbona watu wanaingilia mambo yasiyowahusu? Kwani vyuo viko chini ya mkuu wa mkoa? Chuo chenyewe si ni private-? Haya ndo mambo tunayopigia kelele hivi vyeo vya kupewa kwa chupi ndo maana wanahangaika na mamlaka zisizowahusu. Nachukia wanawake wanaopewa vyeo kwa kuwezeshwa!
 
Back
Top Bottom