jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Mkuu Boliva, nakubaliana kuhusu nia njema ya mwalimu, lakini implementations na implications za hiyo policy turned out to be undesirable!Boliva said:Niliwahi kuwa na mjadala mkali na rafiki yangu mmoja mchaga, alikuwa akidai Nyerere aliwabagu wachaga na wahaya na hakufurahishwa na utetezi wangu kuwa alichofanya Nyerere kilikuwa sahihi. Bado nasimama pale pale Nyerere hakuwabagua wachaga na wahaya labda na wanyakyusa. Alikuwa na lengo zuri kutengeneza mazingara yenye usawa kwa makabila yote.
Huwezi ukafix one problem at the expense of creating even a bigger one.
Unaposema alikuwa na lengo la kutengeneza mazingira yenye usawa, basi ni sawa tu na kusema alichosema mkuu huyu wa mkoa ni sahihi.
Je usawa unaletwa kwa kuwawezesha wananchi walio nyuma kimaendeleo ama ni kuwapachika tu kwasababu unataka usawa?
Kwanini mbinu zilizowapatia kabila moja maendeleo zistumike kuwasaidia wengine badala ya kusema eti wako wengi na wana maendeleo ama wamesoma hivyo hawafai? Hiyo ndo namna nzuri na nia njema ya kuleta maendeleo na usawa?
Je kitendo alichofanya mwalimu hakiwezi kutafsiriwa kuwa na yeye aliamini makabila hayo makubwa ni wabaguzi?
Mkuu kwa taarifa yako hata wizara ya elimu imetumika sana ku hold different standards based on the same assumptions.
Na pia anapofanya hivyo, ie kujaribu ku "spread" maendeleo kwa kuwanyima hawa nafasi na kuwapatia hawa zaidi, ana uhakika kuwa makabila madogo si wabaguzi? Je watu wata ajiriwa based on their merits and qualifications? Ama tu viongozi watahakikisha kuwa si kabila flani? Is that the way to fix this problem for real?
Mimi ninaamini kabisa kuwa nia ya mwalimu yawezekana ilikuwa nzuri, lakini huu utekelezaji siyo kabisa, yani implications/outcomes zake si nzuri hata kidogo, ndo uko utakuta unqualified people nk
Katiba ndo inatakiwa itulinde na si vibaraka wa central government ambao wanapelekwa mikoani na wilayani kulinda maslahi ya mtop alie magogoni, ni kama vile masharti ya rungu la urais yalitakiwa yabadilishwe mara baada ya mwalimu kuondoka kwasababu si kweli kwamba kila mtu atalitumia rungu hilo kwa nia njema.
Huyu aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ametokea kufundwa namna ya kubagua na mara nyingi hawa viongozi wanaoteuliwa na rais huwa wanapelekwa kwa malengo maalum.
Hata kama wakijificha, vitendo na kauli zao vitawaumbua.