Alwaz
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,080
- 10,741
Mkuu wa majeshi wa Nigeria Lt Gen Tukur Yusuf Buratai amesema magaidi nchini humo wataendelea kuwepo hata baada ya miaka 20 ijayo.
Maelezo hayo ameyatoa kwenye ukurasa wake wa twitter baada ya kutokwa kwa mauwaji ya watu 43 yanayosemekana yalitekelezwa na Bokoharam. Maoni yake hayo yamekuja sambamba na wito wa baadhi ya wanasiasa wanaotaka Luteni huyo avuliwe madaraka kwa kushindwa kumaliza tatizo la matendo ya kigaidi.
Mkuu huyo wa majeshi bila kutoa ufafanuzi amesema kuna kutokufahamika kuliko wazi kwa maana ya ugaidi na mambo yanayofungamana nayo. Akazidi kusema kuwa ipo haja ya kuchukua hatua za pamoja na uwajibikaji ulio mpana.
Wakati huo huo polisi wa nchi hiyo wamelazimika kuwafanyia paredi wahalifu waliowashika baada ya kuzuka sokomoko kweny mitandao ya kijamii kwa kutoridhishwa na picha iliyotolewa awali na jeshi hilo ambapo watu wengi walitilia shaka picha hiyo wakisema ilikuwa na ishara za kutengenezwa.
Hii ni mwendelezo wa malalamiko ya wananchi wa nchi hiyo kwa askari na kutilia shaka baadhi ya matukio yanayotokea nchini humo. Hata hivyo haijulikani iwapo paredi hiyo iliwahusisha wahalifu wale wale waliotiliwa shaka na wananchi au ni watuhumiwa wengine katika kuzima sintofahamu za wananchi hao juu ya utendaji wa jeshi hilo.