Mkuu wa Majeshi na Ulinzi (JWTZ) Venance Mabeyo, aahirisha ziara ya Kibiti

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,483
54,846
Mkuu wa Majeshi na Ulinzi (JWTZ) kaahirisha ziara ya Kibiti. Alikuwa akaongee na Wakazi wa Kibiti Pwani. Mkuu wa Majeshi Venance Mabeyo, ameahirisha Ziara hiyo saa chache kabla ya kuanza. Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Bwana Gullamuhusein Kifu amesema, Mkuu wa Majeshi hataweza kuja tena kwani kapata uzuru.

Ziara hii ilikuwa inakuja siku moja baada ya Askari wawili kupigwa risasi. Pwani: Askari Wawili wa Usalama Barabarani wauawa kwa kupigwa risasi Kibiti.

Kwa taarifa iliyotolewa leo Asubuhi, ilisema kuwa leo Mkuu wa Majeshi angeenda kibiti na kuongea na Wakazi wa huko. Mkuu wa Majeshi na Ulinzi (JWTZ) kuwasili wilaya ya Kibiti Leo

Hata Mkuu wa Polisi Simon Sirro alishawahi kufanya ziara kama hii na kuongea na Wazee wa huko.

My TAKE;

Nalaani mauaji yanayoendelea Kibiti. Tanzania ni kisiwa cha amani. Hawa jamaa wa Kibiti wanataka kututilia Mchanga kitumbua chetu cha Amani. Bado naamini Amani inaletwa na Sisi wananchi sio vyama vyetu. Tushirikiane kufichua wahalifu hawa. Mauaji yanayoendelea Pwani; Toa Maoni, Ushauri na Mapendekezo ya nini kifanyike ili kuyatokomeza
 
aisee huko sio kwa kwenda kichwa kichwa.

bila shaka wazee wa intelligence walinusa kitu...wakamwambia asiende.

halafu wale viongozi/makada wenye midomo mirefu ya kuropoka maneno ya vitisho wasipelekwe kabisa huko.

mtu kama daudi bashite huko asipelekwe kabisa...ataropoka mchana halafu wale majamaa watajibu jioni.
 
Ukute Intelligencia imenasa kuwa hali isingekuwa nzuri

Ila sidhani kama ilikuwa sahihi yeye kutaka enda kule...
Kule ni siasa ndio sababu ya mauaji
 
Ukute Intelligencia imenasa kuwa hali isingekuwa nzuri

Ila sidhani kama ilikuwa sahihi yeye kutaka enda kule...
Kule ni siasa ndio sababu ya mauaji


Unamaanisha tatizo ni vyama vyetu vya siasa hivi uchwara ndiyo chanzo !?
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom