Mkuu wa Majeshi na Ulinzi (JWTZ) kwenda Wilaya ya Kibiti Leo

Evans-Arsenal

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
868
1,385
Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, General Venance Mabeyo leo atawasili katika wilaya ya Kibiti, Pwani na kuzungumza na watu wa maeneo hayo.

a274044abaca3fd7cb554f2b68edee19.jpg


General Venance Mabeyo atapata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Kibiti, katika shule ya secondary Kibiti

UPDATES;

Mkuu wa Majeshi na Ulinzi (JWTZ) kaahirisha ziara ya Kibiti mkoani pwani. Zaidi soma=> Mkuu wa Majeshi na Ulinzi (JWTZ) Venance Mabeyo, aahirisha ziara ya Kibiti
 
Huko Kibiti viongozi wanatakiwa kwenda kukaa pamoja na wananchi hata muda wiki moja kuongea nayo kusikiliza kero zao na kuzifanyia kazi kwa haraka sana. Nadhani inaweza kusaidia kupunguza hayo matukio ya mauaji yanayoendelea lugha za kibabe na vitisho haziwezi kumaliza tatizo hilo.Busara na hekima zinahitajika sana katika kumaliza jambo hili kuliko nguvu .
 
Nakumbuka miaka ya tisini mwalimu mmoja alitufundisha kuwa polisi wako trained kuzuia ghasia na uhalifu lakini JW mafunzo mengi yanawaelekeza kummaliza adui hivyo akatutahadharisha kuwa ukiwaona usilete mzaha.
Tatizo la hawa jamaa wa Kibiti ni adui ambao ni invisible!
 
Kuna haja ya kujifunza kitu katika hili binadamu akichoka hubadilika na kuwa mnyama hatari kuliko hata simba ni muda wa viongozi kujitathimini hofu yangu vugu vugu hili likisambaa mikoa mingine itakuwaje maana hata nchi zilizoingia kwenye machafuka mambo yalianza taratibu badae kufikia pabaya zaidi
 
Ni Vizuri
Akawauliza nini madai yao. Maana lazima watakuwa na madai yanayowafanya wafanye mauaji hayo.
Huenda wanamahitaji ambayo yanaweza kutejekezwa na serikali au viongozi wa serikali za mitaa.
Kundi lolote la kigaidi huwa lina madai flani.
Hata kwa kuyasikia tu madai yao itakuwa ni moja ya njia ya kupata ufumbuzi wa tatizo.

Zingatia mkuu.
 
Vita ya kibiti inafanywa na wajeda. Wana biashara zao za kuuza mikaa ambazo zimepigwa marufuku.

Issue ni mkaa na mbao na KIKUBWA ni VIPUSA..

Kwenye kusafirisha mbao na mkaa wanafanya na biashara zao za pembe za ndovu.
Nina uhakika 100% na ninachokisema.

Serikali ilivyoanza kuwabana hawa jamaa ndio wakaanza kuleta noma kwa sababu ni biashara kubwa sana na yenye pesa na ina watu ambao wapo ndani ya system.

Wengine wapo hadi ikulu. Hutaki kuniamini acha.
Hii vita ngumu sana ni kama vita ya marekani na elchapo kings of drugs marekani kila wakipeleka mission ina fail. Kumbe white house elchapo alikuwa na watu wake.
Na madawa yalikuwa yanaingia kama kawaida.
Mwisho wa siku us akawarudisha wanajeshi wake home akajipanga upya.

Hii biashara ya pembe za ndovu sio ya kitoto ni kama madawa.


In short kwenye system wanajuana wote
.

Kumbuka hii post ni msimamo wa Saint Ivuga na sio msimamo wa [HASHTAG]#jamiiforums[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom