Mkuu wa Majeshi na Ulinzi (JWTZ) kwenda Wilaya ya Kibiti Leo

Ila hao ni suala la mda. Njia zote za mawasiliano kutoka na kuingia maeneo hayo nadhani zimeshadhibitiwa kwa hiyo watashindwa kuendelea na logistics zao wataishiwa. Tatizo ni kwamba wataondoka na uhai wa watu kadhaa mpaka wafikie huko. Mwisho wao umekaribia hao wahuni
 
Mmmmh! Najaribu kuifikiria kesho au keshokutwa nini kitajili kwa askari/viongozi wa serikali za mitaa waliopo huko.

Kila la heri afande CDF!
 
Pongezi sana CDF lakini sidhani kama Kibiti wana hitaji CDF. Nikisema hivyo si maanishi kuwa namzuia kwenda popote TZ. Kama mkuu wa jeshi anaruhusiwa kwenda popote na wakati wowote. Lakini, nachelea kusema, huu haukuwa wakati muafaka kwenda Kibiti.
Twendeni Kibiti tukitumia diplomasia zaidi. Tukae, kwanza tuutangaze msamaha kwa waliofanya upumbavu huu, halafu tutake kujua wanataka nini. Haya sio ya CDF. Akiisha enda huyo, inamaana ametangaza vita!! Najiuliza, na naomba msamaha kama nikikosea, Ametangaza vita na nani?? Ni kikundi gani kimejitangaza?? ISIS au Al Shabab au nani sasa?? Hawa ni watu waoga mno mno. Ukiwatishia waoga watazidi kujificha na kutenda gizani (Kushtukiza). Sasa utajua ni nani atakutwa na hiyo risasi leo?? Hebu jamani tutumie hekima na maarifa mengi zaidi. Kusema tutumie diplomasia sio kwamba tumewaogopa. Hatumwogopi tusiye mjua.
 
Usalama utakuepo kwa muda atakaokuepo hapo tuu angetuma vijana kujua tatizo nini maana anaenda kuongea na walengwa katika mauaji huku wauaji wakiwa katika maandaki kama kandahar inatakiwa akili ya ziada sana na si vitisho huko...
 
Alienda Sirro akapiga Mkwara alipotoka tu wakauwa.
Ameenda Amiri Jeshi na bado yupo wamepiga Askari.sasa akienda Mabeyo sijui nini kitafata
 
Wapeleke Wanajeshi kule wapite pori kwa Pori yani tuone kama tutasikia Vifo
Sidhani kama wapo msituni, yasemekana wapo mingoni mwa raia humo humo na wakipiga tukio wanaendelea na shughuli zao za kila siku kama kawaida na jamii inawajaua. Huenda ndio maana wakubwa hawa vyombo vya ulinzi na Usalama wanajaribu sana kuzungumza na wananchi kwa sababau wanaamini wananchi wanawajua. Kwa namna moja au nyingine wananchi wanajiona kama wako attached na hao wahuni na haijawahi mwananchi wa kawaida kuuawa. Wanaona kama wako upande wa kutetea haki zao baada ya kinachodaiwa manyanyaso ya mda mrefu kutoka kwa dola( sijui polisi, mgambo, maliasili n.k).
 
Comrade Saint Ivuga
Sote tunahitaji kumaliza hili tatizo
Tupatie ufumbuzi kwa namna unavyoona inafaa zaidi
Kiongozi wangu. Heshima yako.

Ili kupata solution ya tatizo lolote lazima speculation na ili utatue tatizo lazima ufahamu kuwa ni tatizo gani?

Mara zote vita na mauaji hutokea baada ya uonevu au ubabe.

Na ili vita iishe au ugomvi uishe ni lazima mmoja wapo awe mjinga akubali yaishe.

Naendelea ku type......


Issue ya kibiti ina picha mbili..
Kwanza kuna mashehe wale waliokamatwa..

Wale wasipoachiwa basi mauaji yataendelea bila kukoma.

Wale mashehe waulizwe wanataka nini na waachiwe bila pingamizi lolote.

Kundi lingine ni hawa jamaa ambao wapo kwenye system.

Namaanisha wajeda..

Hakuna wasiwasi kabisa kuwa hii vita inafanywa na trained people.
Imagine mtu mmoja anawalaza askari polisi saba tena wamejikoki wapo kwenye doria?

Huyu sio mtanzania wa kawaida ni mtu mwenye mafunzo ya hali ya juu sana.

Here we approaching the wrong groups,

Wazee wetu waislamu wa kibiti wanakamatwa, wanapigwa wanateswa.

Imagine shehe anatoa wapi mafunzo ya kutumia sniper?

Watu wanadunguliwa kwa sniper..

Data ambazo ninazo kutoka kabisa jikoni ni kuwa hawa jamaa wapo kwenye system wanajuana.

Jeshi la tanzania na ujanja wake wote washindwe kuwadhibuti magaidi wa kitanzania? Tangu lini?

Hapo ni jeshi against government.

Wamalizane wenyewe kiustarabu. Wasimuumize rais kichwa.
Magufuli ana kazi nyingi sana.

Hapo inatakiwa weledi wa mkuu wa majshi amalizane na vijana wake kwa maongezi.
Akitumia nguvu atawashinda lakini itamchukua muda sana na damu nyingi sana zitakuwa zimeshapotea.
Huu ni mtazamo wa Saint Ivuga na sio mtizamo wa [HASHTAG]#jamiiforums[/HASHTAG].
 
Alienda Sirro akapiga Mkwara alipotoka tu wakauwa.
Ameenda Amiri Jeshi na bado yupo wamepiga Askari.sasa akienda Mabeyo sijui nini kitafata
Kwa kuwa akili hawana hapo ndipo wataingia mtegoni. Maana hata vyombo vishawajua hiyo trend Ila kama wasipofanya tukio wakatulia kimya threat level ya hawa jamaa itabidi iongezwe
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom