Mkuu wa Majeshi kaufanyia nini mziki wa Tanzania?

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Wakuu salamu

Husika na Title ya huu uzi.

Tuzo za muziki za Tanzania zinatolewa usiku huu ikiwa ni miaka 7 imepita bila uwepo wa Tuzo hizi nchini Tanzania, tuzo za mwaka huu zinatolewa kwenye Ukumbi wa JNICC Dar es salaam na tayari zimeanza kutolewa ambapo Watu watano wa kwanza kupewa tuzo ya heshima ni Rais Samia, Mkuu wa Majeshi Mabeyo, Marehemu Ruge Mutahaba, Marehemu Bibi Kidude na Mwimbaji Diamond Platnumz.

KWA MUJIBU WA BASATA

Mh. Rais Samia ameupiga mwingi sana, miaka 7 ya Tuzo kukosekana ametenga zaidi ya bilioni 1.5 kwa ajili ya Wasanii na tasnia hii na sasa zinafanyika tena Serikali ikigharamia tukio hili kwa zaidi ya 90%

Tuzo kwa Marehemu Ruge: “Tuzo hii inatolewa kwa sababu Marehemu Ruge alianzisha na kuibua vipaji mbalimbali kwa Wasanii, atakumbukwa sana kwa mchango wake mkubwa kwenye muziki wa Tanzania hivyo Baraza limeamua kumpa Tuzo ya heshima”

Tuzo nyingine ya heshima imekwenda kwa Diamond Platnumz "Tuzo hii inatolewa kwake kwa sababu ni Msanii ambaye alileta mabadiliko katika tasnia kwa kuongeza thamani ya muziki hasa katika dhana ya sanaa ni biashara, Diamond ameonesha kwa vitendo na kwa kuwekeza zaidi kwenye matumizi ya digitali, kujibrand na kuseti viwango vya malipo vyenye tija katika kazi zake lakini kubwa zaidi kuuza muziki nje ya Tanzania"

Bi kidude hakuna asiyejua mchango wake katika ku push taarabu ya Tanzania kwenda kimataifa,huyu hakika anastahili.

Mkuu wa majeshi,hapa mwenye maelezo naomba anifafanulie
 
kila kikosi cha jeshi (jkt) kina kikudi cha ngoma na kwaya..... matukio ya kitafa kwa kiasi kikubwa hupambambwa na vikosi hivi bila wananchi kujua
brass bands kwa majeshi yote, ikiwemo chuo cha kujifunza vyombo vya mziki CCP na tpdf pia kipo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom