Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo akabidhiwa barua ya shukrani kutoka kwa Baba Mtakatifu

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,052
24,442
Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, amekabidhiwa barua ya shukrani kutoka kwa Baba Mtakatifu wa Kanisa Katoliki duniani kutokana na mchango wake uliotukuka kwa ofisi ya Mashirika ya Kipapa nchini (Pms).

Hafla hiyo ya kumkabidhi barua hiyo imefanyika katika makao makuu ya Baraza la Maaskofu Tanzania, kurasini Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam.
IMG_8604.jpg

IMG_8605.jpg

IMG_8606.jpg

IMG_8607.jpg
 
Hilo ndio kanisa linajua jinsi ya kwenda sawa na mamlaka zote za duniani na mbinguni bila kuharibu kokote, mana mamlaka zote zinatoka kwake
 
Kitu gani aliyofanya?

Kama usipohusisha siasa, huyu jamaa anamchango mkubwa sana kwenye kanisa!
Vipo vitabu vingi sana vinavyohusu masuala ya kikanisa alivyoviandika na pia ni mdau mkubwa sana katika kusaidia mashirika mbalimbali ya kipapa na kitume...
Kwa wakazi wa segerea wanamfahamu vyema namna anavyojitoa kanisani!
Kwa Papa kumpa barua hiyo ya shukrani siyo jambo lelemama! Si rahisi kwa mtu kufanya kazi ya kawaida kisha akakubalika na mamlaka za juu Vatican na kupelekea kupongezwa!
 
Correct kabisa hata hom Masanza kafanya mengi sana Mungu ambariki zaidi.
 
Back
Top Bottom