Mkuu wa majeshi Gen V. Mabeyo kuwafunda vijana kuhusu ndoa siku ya Valentine

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,461
2,000
Askofu mkuu wa jimbo katoliki Dodoma Edwin Ngonyani anawalika watu wote hasa vijana katika misa takatifu ambayo pia mkuu wa majeshi ya Tanzania Gen Venans Mabeyo atakuwa mtoa neno na aakofu mwalikwa Beatus Kinyaiya watatoa somo .

Gen mabeyo ambaye hutambulika kama mtu wa dini na imani sana atatoa neno la kuwaasa vijana juu ya umuhumu wa doa katika misa itakayoanza mapema saa 9 mpaka saa mbili usiku.

Ibada hii itafanyika katika kanisa ukumbi wa kanisa la Mt. Paulo wa msalaba msalato jijini Dodoma amabapo pia askofu Edwin Ngonyani askofu mwenyeji atakuwepo

Kama ndoa yako inamatatizo na inamapungufu njoo na mkeo mpate somo kutoka kwa kamanda huyu mweledi


USSR


IMG-20210207-WA0042.jpg
 

Huliza

JF-Expert Member
May 5, 2017
330
1,000
Askofu mkuu wa jimbo katoliki Dodoma Edwin Ngonyani anawalika watu wote hasa vijana katika misa takatifu ambayo pia mkuu wa majeshi ya Tanzania Gen Venans Mabeyo atakuwa mtoa neno na aakofu mwalikwa Beatus Kinyaiya watatoa somo...]
Hivi kwenye ndoa kuna uzoefu?

Mimi najua kila mtu anabeba zigo lake mwenyewe

Wengine walibeba sura halafu zinawasumbua

Wengine walibeba wowo au makalio yanawatokea puani

Wengine walioa vimbaumbau sura ngumu miguu kama chaga wanaishi kwa furaha na amani tele na ndoa zipo imara

Wengine walio miguu ya bia wana raha na amani

Tatizo ndoa kila mtu anabeba tatizo lake hakuna uzoefu
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
6,521
2,000
Hizo ndoa nani aliwatuma muoane nyie wakristu? naona kama mmeshakosea kuanzia mwanzo ila chakushangaza mnaenda kujadili muendelezo wa makosa yenu, mnaenda ku-develop kosa, haya mambo ya ulimwengu huu ni shida sana.
 

ofisa

JF-Expert Member
May 15, 2011
2,881
2,000
Umeona sasa hii nchi ilipofikia
Jamani mbona marehemu rais wa burundi alikuwa mcheza mpira na mapenzi yake hakuyafucha.
Huyu ana mapenzi na malezi ya vijana.na ndiyo kazi kubwa ya kiongozi kuhakikisha vijana wanakuwa na mtazamo positive ili watulie.
 

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
9,337
2,000
Askofu mkuu wa jimbo katoliki Dodoma Edwin Ngonyani anawalika watu wote hasa vijana katika misa takatifu ambayo pia mkuu wa majeshi ya Tanzania Gen Venans Mabeyo atakuwa mtoa neno na aakofu mwalikwa Beatus Kinyaiya watatoa somo...
General ajikite kulinda mipaka, ufundaji awaachie makasisi!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom