Mkuu wa Majeshi ampongeza Shein

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange, amemtumia salamu za pongezi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa tena na wananchi wa Zanzibar kushika wadhifa huo kwa muhula wa pili cha madaraka.

Salamu hizo zilizotumwa na Jenerali Mwamunyange kwa niaba ya Maofisa, Askari na Watumishi wa Umma wanaofanya kazi katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), zilieleza kuwa ushindi wa kishindo wa Dk Shein alioupata unadhihirisha kuwa wananchi wa Zanzibar wameridhishwa na uongozi wake makini na mahiri aliouonesha katika muhula wake wa kwanza wa uongozi wake.

Salamu hizo ziliendelea kueleza kuwa historia ya Dk Shein ya uaminifu, maadili mema na uzalendo aliouonesha katika utumishi wake wa muda mrefu katika nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika kabla hajawa Rais wa Zanzibar imewapa wananchi imani kubwa kuhusu uongozi wake.

“Mheshimiwa Rais, hapana shaka kuwa katika muhula huu wa pili wa uongozi wako, Zanzibar itashuhudia mafanikio makubwa zaidi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, sambamba na kuendelea kuwepo kwa hali ya amani na utulivu kwa wananchi wote,” ilieleza sehemu ya salamu hizo.

Aidha, salamu hizo za pongezi zilieleza kuwa JWTZ inamhakikishia Dk Shein kuwa itaendelea na utiifu, uadilifu na uaminifu mkubwa kwake kama ilivyo desturi ya majeshi nchini. Wakati huo huo, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Zanzibar, Abood Jumbe Mwinyi, naye amemtumia salamu za pongezi Dk Shein kwa ushindi wa kishindo alioupata katika marudio ya uchaguzi wa Zanzibar.

Kwa niaba yake na familia ya Mzee Jumbe, salamu hizo zilitoa pongezi kwa Dk Shein pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ushindi huo na kueleza furaha yake ya moyoni mwake kwa kuona jinsi alivyokiwakilisha chama cha CCM na kukipatia ushindi ambao ulitegemewa.

Nao uongozi na wanachama wa ‘Veteran Young Pioneer Association Zanzibar’ umetoa salamu za pongezi kwa Dk Shein kutokana na ushindi wa kishindo alioupata wa kura 299,982 sawa na asilimia 91.4 katika Uchaguzi Mkuu wa Marudio uliofanyika hivi karibuni.
 
Hii habari imezidi chumviiiiiiiiiiiii , hata hailiki tena , Huyo Jumbe muda mrefu hajui kiingiacho wala kitokacho , hii leo atoe pongezi kwa Shein ,TAIRENI

HEKO CCM NA USALAMA WA TAIFA LA WAVAMIZI
 
Mbona mijasho inawatoka sana ndugu zetu. Hivi Mkuu wa majeshi mbona hakutuma salamu za Pongezi Magufuli aliposhinda, kwa Shein kimetokea nini? IGP naye Mkuu wa Usalama wa Taifa na Magereza na wao watatoa pongezi zao? Lakini swali la misingi ili iweje au wanataka kuonesha nini?
 
Unajuaje kama hakutuma salamu za pongezi kwa JPM?
 
Siku zote kwenye mashindano mshindani akiwa hana mshindani lazma awe mshindi kwa sababu asiyekubali kushindwa siku zote si mshindani.

Umeshindishwa ushindi hujashinda ukawa mshindi...!.
 
Mbona mijasho inawatoka sana ndugu zetu. Hivi Mkuu wa majeshi mbona hakutuma salamu za Pongezi Magufuli aliposhinda, kwa Shein kimetokea nini? IGP naye Mkuu wa Usalama wa Taifa na Magereza na wao watatoa pongezi zao? Lakini swali la misingi ili iweje au wanataka kuonesha nini?
CDF mtu kubwa yule usimlinganishe na igp.
 
Mbona mijasho inawatoka sana ndugu zetu. Hivi Mkuu wa majeshi mbona hakutuma salamu za Pongezi Magufuli aliposhinda, kwa Shein kimetokea nini? IGP naye Mkuu wa Usalama wa Taifa na Magereza na wao watatoa pongezi zao? Lakini swali la misingi ili iweje au wanataka kuonesha nini?

Chama cha mapinduzi CCM walishakula haramu na dunia nzima inajua, wajikaze vivyo hivyo ila historia ita wahukumu wote walio wafanyia uhuni wananchi wa Zanzibar....
 
mkuu wa majeshi ni kati ya watendaji weledi kabisa katika jeshi letu. nampongeza na kutambua mchango wake katika taifa.
 
Back
Top Bottom