Mkuu wa kituo cha Polisi Usa Riva apata Ajali mbaya na kufariki dunia

Diplomatic Imunnity

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,183
1,250
Jamani mwenye taarifa kamali juu ya huyu mhe kupata ajali akamilishe taarifa hii


MKUU wa Kituo cha Polisi (OCS) Holili katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Musa Sinde, amekufa papo hapo, baada ya gari alilokuwa akisafiria, kugongana na gari la Kampuni ya vinywaji baridi Bonite.


Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela,alisema ajali hiyo ilitokea Disemba 8, 2014, majira ya saa 7:30 mchana katika eneo la Kia, upande wa mkoa wa Arusha.


Kwa Mujibu wa Kamanda Kamwela, ajali hiyo ilihusisha Gari aina ya Rav4 lenye namba za usajili T. 395 BMK, iliyokuwa ikiendeshwa na marehemu, na Gari la Bonitte lenye namba za usajili T 352 AUJ, lililokuwa limebeba vinywaji na kusababisha kifo cha mkuu huyo papo hapo.


Kamanda Kamwela, ameeleza kuwa Mkuu huyo wa kituo alikuwa akitokea Moshi kuelekea mkoani Arusha, na kwamba mpaka sasa jeshi hilo halijaweza kufahamu gari la kampuni ya Bonite lilikuwa likielekea wapi.


"Ajali hiyo ilisababisha kifo cha mkuu huyo wa kituo hapohapo, na kwa sasa jeshi la polisi tunaendelea na uchunguzi, ili kuweza kubaini chanzo cha ajali hiyo, kwani mpaka sasa hatujaweza kubaini chanzo wala mazingira halisi ya tukio hilo"alieleza Kamanda.


Hata hivyo amesema kuwa, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyoko mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, kusubiri taratibu za mazishi.
 

Muwazi

JF-Expert Member
May 16, 2014
355
225
Jamani mwenye taarifa kamali juu ya huyu mhe kupata ajali akamilishe taarifa hii
Unasema "NEWS ALERT" Kumbe huna hata taarifa inayoeleweka. Hivi kwa nini watu mnakurupuka hivi? Kama huna uhakika ungesema "TETESI" Ili mwenye uhakika ama taarifa kamili atujulishe. Nyie ndo wachawi na wapotoshaji humu muache tabia hiyo shame on you. Fuatilia utupe taarifa iliyokamilika.
 

mkupuo

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,279
2,000
Yani yeye ni kamanda halafu anakufa kwa ajali mbaya! Mana yake nini jambo hili? Maisha ya abiria wasio makamanda yapo hatarini zaidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom