Mkuu wa kituo cha polisi mbaroni kwa ujambazi

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Mkuu wa kituo cha polisi mbaroni kwa ujambazi

2007-10-26 09:29:16
Na Renatus Masuguliko, PST Chato


Polisi Mkoani Kagera inamshikilia Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Bwanga, Wilayani Chato kwa tuhuma za kushiriki katika tukio la ujambazi wa kutumia silaha lililotokea wilayani humo hivi karibuni.

Wakati hilo likiendelea, watu wanaoaminika kuwa majambazi yameteka nyara mabasi matatu na kufanikiwa kuondoka na mali chache huku basi moja likipinduka katika harakati za kuyakimbia majambazi hayo.

Katika tukio la mkuu wa kituo kukamatwa, imeelezwa kuwa kunafutia wanananchi wilayani hapa wakiwemo?baadhi ya abiria?kumtambua kwamba alikuwa miongoni mwa watu wanaodaiwa kuwa majambazi katika eneo la tukio.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kagera, Bw. Abdallah Msika alithibitisha kwa njia ya simu jana kushikiliwa kwa mkuu huyo wa kituo na kumtaja kwa jina la Koplo Rajabu.

Hata hivyo, hakutaja ni lini alikamatwa kwa mahojiano lakini alisema hatua hiyo ilichukuliwa baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi.

`Kwa kuzingatia utaratibu wa jeshi baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakiwemo waliokumbwa na tukio la uvamizi wa kutumia silaha lililotokea katika kijiji cha Mkungo Kata ya Busaka, wakidai kumtambua kuwepo kwenye tukio tulimkamata na tunaendelea kumhoji toka wiki iliyopita,` alisema Kamanda Msika.

`Tunataka kujua ukweli, kwani katika moja ya matukio yanayodaiwa kuwa alishiriki, sisi tunajua kuwa hakuwepo katika eneo hilo bali alikuwa wilayani Ngara kwenye operesheni maalum, lakini bado tunajiuliza kwa vipi wananchi wamtaje?` aliongeza.

Alisema kinachofanyika sasa ni kuwashirikisha wananchhi waliotoa taarifa hizo na uongozi wa polisi wilayani Ngara alikokuwa kwenye shughuli maalum kufahamu kwa kina ilikuwaje akahusishwa na kuonekana eneo la tukio.

`Kwa sasa ni mapema mno kusema kwa kina kuhusiana na tukio la kukamatwa kwake lakini nitatoa taarifa kwa vyombo vya habari baada ya uchunguzi kukamilka... Nisingependa kumhusisha moja kwa moja kuwa amekamatwa kwa kushiriki ujambazi,` alisisitiza Kamanda Msika.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka wilayani humo, mkuu huyo wa kituo anatuhumiwa kuhusika kushirikiana na majambazi walioteka magari kadhaa katika kijiji cha Mkungo likiwemo gari la hospitali.

Habari hizo zilidai kuwa kiongozi? huyo na baadhi ya watu waliokuwa wakisafiri na moja ya gari lililotekwa na majambazi hao, yaliyokuwa na silaha, walimfahamu bayana mkuu huyo na walilazimika kuwajulisa baadhi ya viongozi katika maeneo jirani.

Ilidaiwa kuwa wananchi hao walikusanyika huku wakiwa wameshatoa taarifa katika kituo cha polisi cha Buselesele na Chato ambapo walifanikiwa kuweka mawe barabarani ili kuyazuia magari yasipite.

Wakati wakiwa katika harakati hizo, gari lililokuwa likitumiwa na majambazi hao akiwemo mkuu huyo wa polisi, lilifika na mkuu huyo kuteremka haraka na kuwaambia wananchi hao kuwa lile gari lilikuwa la walinda amani hivyo waliruhusu lipite.

Wananchi hao waliliruhusu baada ya amri hiyo, lakini baada ya muda mfupi kupita? gari la polisi lilifika katika eneo hilo likilifukuza gari hilo la majambazi na walipoambiwa kuwa limekwishapita, polisi walilazimika kuwafuatilia bila mafanikio.

Wananchi hao walidai kuwa? walilaghaiwa na ofisa huyo wa polisi baada ya kudanganya kuwa gari hilo llilikuwa na watu wema na kuliruhusu kupita hatua iliyosababisha watoe taarifa kwa mara ya pili kwa mamlaka husika na hatua kuanza kuchukuliwa.

Wakati huohuo, majambanzi sita waliokuwa na bunduki zinazosadikiwa kuwa ni SMG wameteka mabasi matatu ya abiria katika pori la Samina na Chibingo, wilayani Geita mkoani Mwanza na kufanikiwa kupora kiasi kidogo cha fedha toka kwa abiria.

Uporaji huo umekuja baada ya basi la abiria kupinduka wakati lilipokuwa katika harakati za kujinasua kutoka mtego wa majambazi hayo kwa kurudi nyuma bila ya mafanikio.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Bw. Zellothe Stephen, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa njia simu.
Alisema Mkuu wa Polisi wilayani humo alikuwa amekwisha fika katika eneo la tukio kufanya operesheni kabambe ya kuwasaka watuhumiwa hao.

Katika tukio hilo miongoni mwa waliotekwa wamo madiwani wawili wa kata za Chigunga, Bw. Peter Lutakwa na Antony Mutalonzwa wa Nyakagomba na askari polisi mmoja aiyekuwepo kwenye safari ya kawaida kikazi kutoka kituo cha Butundwe, kwenda Geita mjini.

Askari huyo aliyekuwa maevaa kiraia ndiye anadaiwa aliyemtia moyo dereva huyo kujinasua kwenye mtego kabla ya gari kumshinda kwa hofu na kupinduka.

Abiria wamedai kuwa majambazi hayo yalisikia yakiomba pesa kwa kiswahili chenye lafudhi ya Rwanda na Burundi.

Majambazi hayo waliokuwa wamepanga magogo barabarani, walisababisha moja ya mabasi yaliyokuwa yametangulia kupinduka na abiria 15 kujeruhiwa vibaya.

Tukio lilitokea eneo hilo jana asubuhi ambapo majambazi hayo yanayodaiwa kuwa yalikuwa na bunduki mbili aina ya SMG yaliweka magogo barabarani ili kuyazuia magari yote yasipite katika eneo hilo kwa lengo la kukusanya fedha toka kwa abiria hao, wengi wakiwa wafanyabiashara.

Mabasi hayo yaliyotekwa na majambazi hayo ni yale yaliyokuwa yakitokea katika tarafa ya Butundwe katika kata za Bukondo na Katoro kwenye barabara kuu iendayo wilayani Chato yenye namba za usajili T.692 , mali ya Muba, T.444 AJM na lenye namba T437 AJ `Usiogope kazi` lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyetambuliwa kwa jina moja la Faraj, ambalo ndilo lililoanza kutekwa na kupata ajali.

Baadhi ya abiria walijeruhiwa kutokana na kubanwa na viti na kuangukiwa na viti vya basi hilo na ndipo majambazi hao walifika na kuanza kuwaamuru walale chali huku yakiwataka watoe pesa ambapo baadhi yao waliwapa fedha hizo kabla hayajatokomea mbali baada ya kusikia ngurumo ya gari.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Cassian Kabuche, alisema kuwa majeruhi 15 ndio waliofikishwa hapo na kupewa matibabu ambapo wanne kati yao wamelezwa wodi namba nane na saba kutokana na hali zao kuwa si za kuridhisha.

SOURCE: Nipashe
 
NO wonder wananchi wanaamua kutoa wahalifu wao vituoni.
Tangu lini Jambazi anaweza kumshughulikia Jambazi mwenzie? au hata mbakaji?

IGP, kabla hujawapiga risasi wananchi, wapige kwanza vijana wako.
 
NO wonder wananchi wanaamua kutoa wahalifu wao vituoni.
Tangu lini Jambazi anaweza kumshughulikia Jambazi mwenzie? au hata mbakaji?

IGP, kabla hujawapiga risasi wananchi, wapige kwanza vijana wako.
Reply With Quote

Nakuunga mkono Hume. Kumbe wananchi wanapowatoa watu mahabusu na kuwaadhibu huenda hizi zikawa ndio sababu zenyewe. Sasa kama askari ambaye tunamuamini kwa kutulindia mali zetu na maisha yetu ndio anashiriki katika unyang'anyi, sisi tufanyeje?
 
Ya
Mkuu wa kituo cha Polisi Koplo Rajab!
Yaani kwa akili zako unafikiri vituo vyote vya polisi hata vidogo wakuu wa polisi Lazima wawe ma ASP kama jambo hujui ni vema kukaa kimya kuliko kujifanya unashangaaa Fanya utafti.
 
Habari ya mwaka 2007....RPC akiwa Mzee Msika....miaka zaidi ya 10 sasa ndio inaletwa leo??? Acheni zenuu jamaniii!!!!
Humu habari zipo tangu Forum ianzishwe ambazo hazijafutwa.
Ukipost kwenye uzi husika, uzi unapanda juu miongoni mwa nyuzi zinazojadiliwa muda huo
 
Najua mkuu sasa alieilepandishaa ndio hakueleza kuwa ni zamani na si sasa......inakanganyaaaa
Humu habari zipo tangu Forum ianzishwe ambazo hazijafutwa.
Ukipost kwenye uzi husika, uzi unapanda juu miongoni mwa nyuzi zinazojadiliwa muda huo
 
Najua mkuu sasa alieilepandishaa ndio hakueleza kuwa ni zamani na si sasa......inakanganyaaaa
Kweli,
Hata mimi mwenyewe nilipoona kichwa cha habari nikawahi kuifungua nilidhani ni ya sasa
 
Habari ya mwaka 2007....RPC akiwa Mzee Msika....miaka zaidi ya 10 sasa ndio inaletwa leo??? Acheni zenuu jamaniii!!!!

Duh
Unachekesha sana na jicheke kwa uliyoandika kama vile mshindi kumbe pwaaaaaaa... Inaonyesha unasomaga bila hata kuangalia imerushwa lini... jionee aibu hujui ya forums.. natumaini leo umejifunza.
 
Duh
Unachekesha sana na jicheke kwa uliyoandika kama vile mshindi kumbe pwaaaaaaa... Inaonyesha unasomaga bila hata kuangalia imerushwa lini... jionee aibu hujui ya forums.. natumaini leo umejifunza.
Kesho nakutoleaa posa weye

Ova
 
Back
Top Bottom