Mkuu wa Kaya sasa ni wakati wa kubadili gia angani

MGANGA MCHAWI

Senior Member
Oct 15, 2015
199
393
Nikikumbuka mbwembwe za mwanzo za uongozi wa serikali ya awamu ya tano nakua siamini kinachoendelea. Yako wapi yale matamko ya mawaziri?
Ziara za kushtukiza zimeenda wapi?

Yule DC alievaa nguo za mgambo na kutembelea hosipitali bado yupo?
Hivi lile agizo la mkuu wa kaya kutaka taasisi zote zinazodaiwa na NHC zilipe malimbikizo yao ndani ya mwezi m1 na kama wakishindwa watolewe nje vitu vyao kama yule wa Hai lilitekelezwa?

Ni dhairi kuwa mbinu ulizokuwa unatumia mwanzo zimeshafeli na sasa ni wakati muafaka wa kubadilisha.Nchi haihitaji kutumia nguvu ili iende bali kutumia busara na kusimamia sheria na kanuni tulizojiwekea.Ni wakati wa kuanza kuwaamini wateule wako kabla hujachelewa.Acha dhana ya kwamba bila ww basi kazi haziendi.

Anza kutumia mfumo wa piramidi katika uongozi. Hivi mkuu unahisi kuna haja ya ww kwenda kutembelea mradi uliosimama kwa kukosa fedha na kutoa tamko likatekelezwa? Waziri husika yupo wap? Waziri mkuu yupo wap? Vp kwa miradi inayotekelezwa mbali ambapo huwez kufka? Mkuu tengeneza mfumo utakaoweza kufanya kazi hata kama ww haupo.

Hivi unajua kwanini saiv mawaziri wako wapo kimya? Ulishajiulza hilo swali? Dharau, vitisho, kebehi, majigambo sio njia nzuri za kuongoza.Ukishampa mtu mamlaka muamini kuwa anaweza akateleza majukumu yake na kitu cha kufanya ni kuangalia tu anafata taratibu na kanuni zinazomuongoza. Na kama ikitokea amekosea usitumie mwanya huo kupata sifa kwa kutoa maagizo na maelekezo kwa dharau na vitisho.

Hivi mkuu unakumbuka ulivotofautiana katika maamuz kpnd kle ni waziri kuhusu kubomoa jengo la tanesco pale ubungo?Nani alikutsha au kukudharau kuanzia waziri mkuu hata Rais?Nani alikwambia kama hutaki kufata maamuzi yao uache kazi.Njia yako ya uongoz inawavunja moyo wateule wako.

Walianza kwa spidi kubwa sana ila saiv wote kimya.Hizi ni dalili mbaya katika uongozi na ni vigumu kugundua kwa sababu mtu mzima hanuni kwa mashavu bali moyoni.

Sasa ni wakati wa kubadilsha njia za uongozi toka kwenye "ONE MAN ARMY" hadi kwenye "TEAM WORK" Anza kusukuma maendeleo kwenye wizara, Wizara zitasukuma mikoani, Mikoa itasukuma wilayani, wilaya itasukuma kwenye kata, kata zitasukuma kwenye vijiji, mitaa na vitongoji.Hiyo ndio njia nzuri za kuongoza.

Kiongozi mzuri ni yule ambaye ana uwezo wa kutambua raslimali alizokua nazo na kuzitumia kwa manufaa mapana ya nchi.Raslimali ni pamoja na watu.Anza kutumia wataalamu uliokuwa nao.Umeteua watu makini na wenye uwezo mkubwa sana ila tatizo umeshindwa kuwatumia.Watumie ipasavyo.Ni aibu kwa kiongoz wa kaya kushangaa wateule wako hawajakuletea majina ili uteue kamishina wa kupambana na madawa ya kulevya.

Pia ni aibu kusema kuwa walimficha waziri mkuu kuwa yeye ni mwenyekiti wa kumati ya kupambana na madawa ya kulevya.Nani alikuficha? Kwa manufaa ya nani? Ni aibu kusema kuwa umeamua kwenda mwenyewe kutembelea mradi mana ungeomba taarifa wamekudanganya. Hivi kweli upo serious mkuu wa kaya? Yani kweli unaamini pamoja na vitisho vyako vyote bado kuna wateule wanaweza kukidanganya? Umewachagua wanini kama huwaamini?

Ni hayo tu mkuu kwa leo.
TAFAKARI, CHUKUA HATUA.
 
Ni wakati wa kuanza kuwaamini wateule wako kabla hujachelewa.Acha dhana ya kwamba bila ww basi kazi haziendi.

Mkuu tengeneza mfumo utakaoweza kufanya kazi hata kama ww haupo.

Ukishampa mtu mamlaka muamini kuwa anaweza akateleza majukumu yake na kitu cha kufanya ni kuangalia tu anafata taratibu na kanuni zinazomuongoza. Na kama ikitokea amekosea usitumie mwanya huo kupata sifa kwa kutoa maagizo na maelekezo kwa dharau na vitisho.

Ndio nini hichi ulichochangia?
Anamshangaa mtoa mada ya kiushauri. Wakati huo mfumo anaoushauri tayari ulishafeli. Ubadhirifu wa mali ya umma, uzembe, rushwa, nk nk, madudu mengi ya kuchefua. Huyu kaingia na staili yake anayoamini ninaweza ikatuondolea kero. Akitaka kushauri, basi ajikite na "aidia" mpya itakayotoa dira ya mafanikio katika kuondoa kero, siyo kushauri kuturejesha katika mawazo yaliyofeli ya awamu zilizopita. Pia raia tuwe na kiasi.
 
Akifuata taratibu vyema hakuna shida atafanikisha kila alitakalo lakini akiendelee kuamini yeye ndiye muweza wa yote hakika miaka mitano itaisha na hakuna kilicho fanyika.
 
Sidhani alicho kiandika kwa mtu mwenye akili timamu kabisa asiye na dosari yeyote kwenye ubongo wake atapinga , hadi nakushangaa
Sasa kama maisha yamekuwa yale yale - Na maisha yale yale yalikuwa mazuri tu then tatizo na mijilawama hii ya kila kukicha ni ya kazi gani - Hivi mna akili timamu kweli ?
 
Anamshangaa mtoa mada ya kiushauri. Wakati huo mfumo anaoushauri tayari ulishafeli. Ubadhirifu wa mali ya umma, uzembe, rushwa, nk nk, madudu mengi ya kuchefua. Huyu kaingia na staili yake anayoamini ninaweza ikatuondolea kero. Akitaka kushauri, basi ajikite na "aidia" mpya itakayotoa dira ya mafanikio katika kuondoa kero, siyo kushauri kuturejesha katika mawazo yaliyofeli ya awamu zilizopita. Pia raia tuwe na kiasi.
System haukufeli ila ilifelishwa.walichokosea utawala uliopita ni kutochukua hatua kwa viongozi waandamizi ambao aliwaamni.Ukisoma vizuri nilochoandika nmesema lazi yake itakua ni kuhakikisha wateule wake wanafata kanuni na taratibu zinazowaongoza.
 
Sasa kama maisha yamekuwa yale yale - Na maisha yale yale yalikuwa mazuri tu then tatizo na mijilawama hii ya kila kukicha ni ya kazi gani - Hivi mna akili timamu kweli ?
Hapana maisha hayajawa yaleyale mkuu maisha yamekuwa mabaya zaid ya yale kila kitu kimesimama maisha hayaeleweki, serikali ndio hiyo hadi mkuu wa mkoa anamuamrisha spika wa bunge, majanga yakitokea ndio hivyo wenye majanga wajitwishe mizigo yao ,watumish nao hakuna walilotendewa jema tangu upya wa serikali yao zaid ya kadhia za kila mara , na wahisani ndio hao tena wanakuja wanatoa ahadi wakienda ndio wameenda jumla, unadhani kuna mfanano na serikali za kale mkuu? Kwani hayo yalikuwepo mkuu, kulalamika ni lazima walalamike maana wanakutana na maajabu wasiyo wahi yatarajia.
 
Back
Top Bottom