Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,500
- 9,279
Jumuiya ya nchi za kiarabu inatilia shaka nafasi ya Marekani kama mpatanishi katika mzozo wa mashariki ya kati.
Uamuzi wa Marekani kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel "unazusha suala kuhusiana na mchango wake na jukumu lake katika kuimarisha utulivu na amani katika eneo hilo, amesema hayo katibu mkuu wa jumuia ya nchi za kiarabu, Ahmed Abu Gheith, katika mkutano wa dharura wa jumuia hiyo mjini Cairo.
Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa jumuia ya nchi za kiarabu wameitolea wito Marekani ibatilishe uamuzi huo.Tangazo la rais wa Marekani Donald Trump "linavunja vibaya sana sheria za kimataifa".Wamesema mawaziri wa nchi za nje wa jumuia ya nchi za kiarabu.
DW