Tetesi: Mkuu wa jeshi la Magereza nchini huenda akatumbuliwa

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939
Wana JF,

Kutokana na safari ya kikazi alioifanya Mh Rais katika magereza jana Ukonga na kubaini yafuatayo;

1. Askari magereza kununua sare za jeshi lao kwa watu binafsi
2. Jeshi la magereza kushirikisha watu binafsi katika ujenzi, hali hii ilimchukiza Mh Rais.

Aidha kutokana na machukizo hayo ni dhahiri Mh Rais atatengua uteuzi wa Mkuu wa jeshi la Magereza nchini Kamishna Jenerali John Casmir Minja.
 
Tenda hizo , na yeye aliukuta huu utaratibu . Makampuni yaliyokuwa yatapata tenda kilio kwao . Nimekumbuka uniform za wafanyakazi wa Air Tanzania zilikuwa zinashonwa nje ya nchi , wakati shirika lilikuwa na ndege moja tu . Ila kusema kweli watu walikula sana pesa ya umma .
 
Naamini atamvumilia kidogo maana magereza wanasahaulika sana! Alipowapa zile 10b maana yake afukie mashimo mambo yakae sawa! Kama umri umesogea sogea atamvumilia amalize astaafu zake! Nina mashaka na Mangu.....kama atamaliza mwaka huu!
 
Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama siyo wa kutumbuliwa hivi hivi kama vibaraka wa CCM kwenye ngazi za Mkoa na Wilaya.

Nakuambia,hawezi Kutumbuliwa.

Iliwezekana na DCI sembuse huyo wa magereza tu
 
Wana Jf
Kutokana na safari ya kikazi alioifanya Mh Rais katika magereza jana ukonga na kubaini yafuatayo
1. Askari magereza kununua sare za jeshi lao kwa watu binafsi
2. Jeshi la magereza kushirikisha watu binafsi katika ujenzi, hali hii ilimchukiza Mh Rais,Aidha kutokana na machukizo hayo ni dhahiri Mh Rais atatengua uteuzi wa Mkuu wa jeshi la Magereza nchini Kamishna Jenerali John Casmir Minja.
Hili mbona liko wazi. Si unajua jinsi rais wenu anavyokurupukaga?
 
Naamini atamvumilia kidogo maana magereza wanasahaulika sana! Alipowapa zile 10b maana yake afukie mashimo mambo yakae sawa! Kama umri umesogea sogea atamvumilia amalize astaafu zake! Nina mashaka na
Mangu.....kama atamaliza mwaka huu!

IGP Mangu amefanyaje tena? Lete habari mkuu
 
Wana Jf
Kutokana na safari ya kikazi alioifanya Mh Rais katika magereza jana ukonga na kubaini yafuatayo
1. Askari magereza kununua sare za jeshi lao kwa watu binafsi
2. Jeshi la magereza kushirikisha watu binafsi katika ujenzi, hali hii ilimchukiza Mh Rais,Aidha kutokana na machukizo hayo ni dhahiri Mh Rais atatengua uteuzi wa Mkuu wa jeshi la Magereza nchini Kamishna Jenerali John Casmir Minja.

Askar hawanunui sare kwny Maduka Binafsi bali wananunua vitambaa kwny Maduka binafsi na wanaenda kujishonea binafsi sasa uamuzi wa Rais kusema Maduka binafsi yakabidhi Mara moja hizo sare maana yake ni kuwapora Vitambaa hivyo, Kisheria ni kosa kuvaa sare za Majeshi yetu lakin si kosa wala dhambi kuvaa shati au Suruali inayofanana rangi na sare za Majeshi yetu isipokuwa sare za Jwtz, sasa tangazo Hilo kwa lugha nyingine tumepiga Marufuku kuuza vitambaa vya aina hiyo so badala ya kuwapora Wenye Maduka binafsi itumike busara wavinunue ili kupunguza hasara kwa Wafanyabiashara wetu ambao kila kukicha Hali inazidi kwenda halijojo!

Duka la Khimji pale Mnazi mmoja lilifunguliwa Miaka mingi sana kabla ya Watoa Amri hawajaja mjini anaweza kuwa Mhanga wa Kwanza!
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom