Mkuu wa jeshi aponea kifo Somalia

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
140528111919_somalia_mkuu_wa_jeshi_512x288_bbc_nocredit.jpg

Jenerali Dahir anaendesha moja ya magari yenye uwezo mkubwa wa kudhibiti mashambulizi

Mkuu wa jeshi la Somalia ameponea chupuchupu kuuawa mjini Mogadishu.
Hili ndilo shambulio la punde zaidi katika msururu wa mashambulio dhidi ya viongozi wa serikali na rasilimali za serikali nchini humo.

Gari lake Jenerali Dahir Aden Elmim lilirushiwa bomu katika barabara kuu karibu na afisi za wizara ya ulinzi mjini Mogadishu.
Aliponea kwa sababu yeye huendesha mojawepo ya magari machache yaliyo na uwezo wa kudhibiti shambulio la risasi, ambayo yametengewa viongozi wakuu wa serikali hiyo.
Hakuna yeyote aliyedai kuhusika na shambulio hilo kufikia sasa japo inafahamika kuwa kundi la Al shabaab limekuwa likifanya mashambulio ya mara kwa mara mjini Mogadishu.
Mwishoni mwa juma, watu 15 waliuawa katika shambulio lililolenga jengo la bunge la Somalia. Wengine wengi walijeruhiwa wakiwemo wabunge 3. mia

Chanzo:bbc
 
We mleta mada na bbc kiswahili gani hiki. Ameponea kifo??kiswahili cha wapi hiki. Kwa hiyo ametumia kifo kupona?
 
140528111919_somalia_mkuu_wa_jeshi_512x288_bbc_nocredit.jpg

Jenerali Dahir anaendesha moja ya magari yenye uwezo mkubwa wa kudhibiti mashambulizi

Mkuu wa jeshi la Somalia ameponea chupuchupu kuuawa mjini Mogadishu.

Hili ndilo shambulio la punde zaidi katika msururu wa mashambulio dhidi ya viongozi wa serikali na rasilimali za serikali nchini humo.

  • Gari lake Jenerali Dahir Aden Elmim lilirushiwa bomu katika barabara kuu karibu na afisi za wizara ya ulinzi mjini Mogadishu.
Aliponea kwa sababu yeye huendesha mojawepo ya magari machache yaliyo na uwezo wa

kudhibiti shambulio la risasi, ambayo yametengewa viongozi wakuu wa serikali hiyo.
Hakuna yeyote aliyedai kuhusika na shambulio hilo kufikia sasa japo inafahamika kuwa kundi la Al

shabaab limekuwa likifanya mashambulio ya mara kwa mara mjini Mogadishu.
Mwishoni mwa juma, watu 15 waliuawa katika shambulio lililolenga jengo la bunge la Somalia. Wengine wengi walijeruhiwa wakiwemo wabunge 3.

Chanzo: BBC
 
Back
Top Bottom