Mkuu wa Idara ya Utafiti Wizara ya Elimu asimamishwa kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa Idara ya Utafiti Wizara ya Elimu asimamishwa kazi

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kapotolo, Sep 14, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imemsimamisha kazi na itamchukulia hatua za kinidhamu Mkuu wa Idara ya Utafiti, Tathmini na Huduma za Kompyuta, Joseph Mbowe baada ya uchunguzi kubaini kuwapo kwa dosari katika ukokotoaji wa alama za mitihani ya somo la Islamic Knowledge katika kompyuta.

  Aidha, Wizara hiyo imeagiza Necta kukokotoa upya alama za mitihani ya wanafunzi wa kidato cha sita ya somo hilo waliofelishwa kwa bahati mbaya mwaka huu kutokana na dosari hiyo na tayari matokeo ya alama hizo yametolewa.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo na Ufundi, Philip Mulugo alisema Mei 28, mwaka huu, Wizara ilipokea malalamiko kutoka Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu, dhidi ya matokeo ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka huu katika somo hilo.

  Source: Habari leo
   
 2. fugees

  fugees JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 2,587
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Poa na safi kwa kuwawajibisha vilaza! Lakini isiwe kwa idala tu iwe hata kwa kamuhanda na wenzie wote!
   
 3. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Muslims' power,wanaposema kuwa wanafelishwa kwa sababu ya dini yao usiwabeze,unapaswa kuwasikiliza.
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  mtihani wa islamic
   
 5. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  waisilamu huwa hawasemi uongo kwetu uongo ni mwiko hilo ni somo la dini tu je vipi masomo mengine huwenda huwa wanayachakachuwa sana leo Allah amewadhalilisha wanaona haya kwa kuwadhulumu waisilamu tunataka NDALICHAKO na mfumo mzima ubomolewe maana kile ndio kichaka cha kuwachinjia waisilamu
   
 6. nkyalomkonza

  nkyalomkonza JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 1,165
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wamemtoa kafara tu. Sidhani kama ni yeye anaehusika. Kumbuka matokeo ya mtihani hayaandaliwi na mtu mmoja, bali ni Board ya NECTa. Mbona wao hawakuliona hilo?. Huyo jamaa ni Mbuzi wa kafara.
   
 7. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu rekebisha title ni Mkuu wa Idara ya Utafiti NECTA na sio Wizara ya Elimu .
   
 8. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,382
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Nchi isiyo na dini kwa nini inasimamia na kusahihisha mitihani ya dini? Serikali ifute kabisa mitihani ya dini, kama watu wanataka kujua wanaielewa kwa kiasi gani dini yao basi dini husika ziwatungie mitihani huko kwenye Sunday school, kipaimara sijui na madrasa. Ni upuuzi serikali inayojidai haina dini kusimamia mitihani ya dini
   
 9. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tatizo sio kusahihisha mtihani ndugu inabidi uelewe.

  Tatizo lilikuwa kwenye mfumo wa kompyuta. Mitihani ikishafanywa matokeo yanaingizwa kwenye system kutegemeana na namba za mtahiniwa sasa system ikawa haijaelekezwa vizuri kukokotoa wastani kwa paper 1, paper 2 na paper 3.
   
 10. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tulishatangaziwa miezi kadhaa iliyopita kwamba mkuu huyo wa idara alisimamishwa kazi kupisha uchunguzi. Sasa naibu waziri anapotangaza matokeo ya kamati ya uchunguzi kisha anasema hatua imechukuliwa kwa kumsimamisha kazi mkuu huyo huyo wa idara (ambae teyari amesimamishwa siku nyingi) nashindwa kuelewa. Nilidhani ama baada ya kusoma report ya uchunguzi wangetangaza kurudishwa kazini kwake au KUFUKUZWA na sio kusimamishwa tena. Kiini macho kwa kweli.
   
 11. u

  upendom Member

  #11
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wewe pepombili huwezi kujenga hoja,kaimbe taarab ndo fani yako .
   
 12. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #12
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yatajiri mengi kabla ya uamuzi wangu 2015.
   
 13. nkyalomkonza

  nkyalomkonza JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 1,165
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Baada ya System matokeo hupitiwa na Board mbona hawakuliona hilo tatizo?
   
 14. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  nilivyoisoma ile taarifa ni wazi huyu mtu wa IT inawezekana hakufahamu kilichokuwa kinaendelea na hana makosa.
  Walisema kuwa kawaida zilikuwa 'paper' tatu lakini wakiabadilisha na kuwa 'paper' mbili. Kwa kawaida system za computer na hasa DATABASE zinakuwa na commands zake zinazoziwezesha kuprocess data automatically. Kwa maani hiyo system ilikokotoa kwa kwa wastani wa tatu badala ya mbili ambayo haikuwepo kabla. Hivyo ni wazi mtu wa IT anafanya kazi kwa kutegemea data na commands zake na wala hakai kisikiliza 'siasa' za NECTA zinaendaje.

  Sasa kama Baraza liligundua baada ya Bw. Mbowe na vijana wake wa IT kufanya kazi zao ni kwa nini walaumiwe. Maana nimeona kwenye taarifa kuwa baada ya hili tatizo kubainika waliwataarifu walimu wa Islamic Knowledge na walilielewa suala zima na kulishukuru Baraza. Kwa maana hiyo suala za kuita hii hujuma liko mbali sana na nadhani jibu sahihi ni kuita 'uzembe'

  Mwenye maoni tofauti na haya naomba anipe mwanga zaidi
   
 15. zethumb

  zethumb JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 606
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  halafu kinachonishangaza ni kwamba, waislamu mnadai Ndalichako (JEMBE LA MATHEMATICS TZ YOTE) afukuzwe baraza, awekwe nani? waislamu kila kitu ni kutumia nguvu tu na reasoning ndogo kwamba kitu kimefanyika kwa sababu si mwenzetu, mnawaita...."makafiri".... jaribuni kubuni njia za kufikisha ujumbe pasina UDINI! nyie mnakalia mmefelishwa ISLAMIC KNOWLEDGE, hiyo inakusaidia nini katka maisha?, utakuwa docta. accountant, lawyer, physician, chemist kwa islamic knowledge? mgesema mmefelishwa HISABATI ningewaona wa maana lakin islamic knowledge?, islamic knowlege na christianity ni masomo tu ya kufanya wanafunzi wajue imani na misingi ya maisha na hata ukifeli na kufaulu masomo mengine hakuna mbaya! mnachekesha kweli, eti mnaandama hamtaki sensa na waliokatwa waachwe then.... NDALICHAKO UNAFUATA.... kama hamna utaratibu kabisa!
   
 16. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #16
  Sep 14, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  I think you have a point. Kama hatutaki kuhesabu watu kwa misingi ya dini zao kwa sababu "hatuna mpngo wa kuwajengea nyumba za ibada", kwanini tuwatahini ufahamu wa dini zao?
   
 17. nyotanjema

  nyotanjema Senior Member

  #17
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  katika hili wanapashwa kuwajibika wahusika ila tuondoe dhana ya kuwa upande mmoja unaonewa hii haiingii akilini kama wewe ni kilaza uwe mkristu au muislamu form 6 utafeli tu hata hiyo form 4. kwa nn hatupimi uwezo wa al muntazir, feza boys,marian ,st francis, mzumbe,kibaha n.k then tukaja na majibu sahihi sio haya ya kuambiwa kwenye vipaza sauti au vijiwe vya kahawa.Hili jambo halihitaji siasa narudia tena KAMA WEWE HUSOMI USITEGEMEE KUFAULU. Mbona tunapotosha wasiosoma??? hata waliosoma nao wanapotosha?? Misingi ya kufaulu kwa mwanafunzi ni jitihada binafsi katika masomo.
   
 18. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Nilidhani Baraza la Mitihani (NECTA) ndio lingewajibika. Inakuwaje awajibishwe mtu kutoka wizarani? Je hayo matokeo yaliidhinishwa na kusainiwa na nani? Hakujua anachosaini? Huyo ndiye aliyestahili kuwajibishwa na si vinginevyo. Tuache kuonea dagaa wakati waharibifu ni samaki na wanafahamika.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...