Mkuu wa Chuo Mandaka TTC ni jipu

Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
9,730
10,811
Mh.Waziri wa Elimu kwa heshima na taadhima mpangie kazi nyingine mkuu huyo wa chuo, ana wanyanyasa watoto wetu.Wanafunzi wameripoti mwanzo wa muhula, hawajapewa magodoro na huduma ya chakula kwakuwa hawajakamilisha malipo mbali mbali.

Wanafunzi wengine wametoka mbali kama Bukoba na Mbeya hawajapokelewa kwa kushindwa kukamilisha malipo. Kiasi kilicholipwa kama hakijalipwa kwa ukamilifu,ni kutokana na hali halisi ya upatikanaji wa fedha nchini. Kwanini wakufunzi hawawapokei wanafunzi na kuwapatia huduma za muhimu!

Wanafunzi kunyimwa magodoro na Chakula ni kinyume na haki za msingi za kibinadamu.
Hatua za haraka zichukuliwe kuwanusuru watoto wetu.Ni uonevu usiokubalika.
 
Back
Top Bottom