Mkuu Serengeti: Mkuu wa shule anaendekeza Rushwa ya ngono

chamilo nicolous

JF-Expert Member
Mar 10, 2016
1,991
1,364
Uovu huu ungeendelea hadi lini?
Binafsi nawapongeza TAKUKURU DODOMA, kwa kazi nzuri mliyofanya. Mungu awabariki!

Niweke kumbukumbu sawa,:-
Vitendo vya mapenzi kati ya walimu na wanafunzi katika Shule ya Serengeti vimekuwepo kwa muda sasa.

Mwaka 2015/2016 vitendo hivi vilishamiri kwa kasi sana, baadhi ya wazazi na walimu hawakufurahishwa. Mbaya zaidi kabineti ya mkuu wa shule ndiyo ilikuwa inahusika. Ilifika sehemu wakimpa mwanafunzi mimba wanampa ruhusa ya ugonjwa, anatoka shule anaenda mahali anajiweka sawa anarudi.

Mwaka 2016/2017 aliyekuwa makamu mkuu wa shule alinogewa na penzi la mwanafunzi kiasi cha kuleta ugomvi wa kifamilia, kitu kilichopelekea mwanafamilia mmoja kuchukua kisu na kuvamia bweni akitaka amudhuru huyo mwanafunzi.

Na ikiwa mwanafunzi akiambiwa swala la kumfanya mpenzi akakataa, anatishiwa kupewa adhabu aidha anasakamwa sana, hivyo wengine wanakubali yaishe.

HEKO KWA TAKUKURU DODOMA: tunaomba Mamlaka husika mlifuatiliye kwa ukaribu, siyo yeye tu, anarafiki zake anafanyakazi nao, nao wanafanyanyasa wanafunzi kingono.
 
Dah! Hiyo hatuiti rushwa ila ni TEACHING ALLOWANCE jamani mtuache walimu na sisi kwenye kitengo chetu. Mbona wenzetu kwenye vitengo vingine wamehalalishiwa rushwa na bos kwa kusema ni hela ya kung'arishia viatu. Utani tu jamani.
 
Hii ya kuwaandama watoto wa kike na kuwapa pressure bila sababu Kwa kisingizio eti mwalimu anadhibiti nidhamu,ni janga sana kwenye baadhi ya taasisi za elimu.

Ninaamini ipo mifumo inayochochea hali hii kuwepo.Na walimu wanaofanya hivi wanajua kichaka cha kujificha.

Natoa wito kwa mawaziri wanaosimamia taasisi za elimu,wakae chini na kuangalia changamoto hii.Wamekuwa kimya sana


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku za mwizi arobaini, ni ngumu sana kumshawishi MTU kuwa wewe si mwizi ikiwa umekamatwa unaiba
 
Back
Top Bottom