Mkuu Rrondo kwa hili la matamshi naomba niwe upande wa watangazaji

Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
2,330
4,151
RRONDO ndugu yangu kitu cha kwanza katika lugha ni lazima ujue alama kuu zinazoitambukisha lugha fulani ni lahaja na lafudhi

Lahaja ni namna ya utamkaji wa maneno na lafudhi ni namna uongewaji wa hayo maneno unawasilishwa
Sasa katika hili watangazaji wetu wa kiswahili wako sahihu asilimia 100% pale wanapotumia lahaja na lafudhi ya kiswahili kutamta majina ya watu wa mataifa mengine maaba hii inawarahisishia ufikiwaji wa taarifa wale wenyeji wa lugha fulani kwa ufanisi. Mimi huwa huwa nakerekwa sana na mtangazaji anatangaza kiswahili halafu Rojo anaitamka Roho ni ujinga mtupu, hiyo roho ni lahaja ya kihispania, unaposema eti mtangazaji atamke Gerit Beli badala ya Garethi Bale hapo unalazimisha tuizoee tamadani nyingine kwa ulazima kwenye lugha yetu

Kama umewahi fatilia wachambuzi wa kifaransa na kiarabu huwa wana namna yao ya utamkaji tofauti na waingereza, kwa mfano wafaransa hutamka Pierre ( Piaa) ila waingereza ( Pieri) na waarabu au waturuki hutamka (Piere) kama sisi huku bongo tunavyotamka Piere.

Kwa hiyo mimi ninaona wako sawa kabisa kwa muktadha wa lugha yetu kutamka kwa lahaja yetu, kama ni Van Dijk sisi tutamke (van dijiki) badala ya van daik

Kwa hiyo ukitakitaka tulamizishe kutamka kama wazungu huu utakuwa ni uboya na hakutakuwa na maana ya kujivuni lugha yetu ya kiswahili
Tena ilibidi hata Lacazette tutamke Lachazete badala ya lakazeti
Ronaldo=Ronaldo badala ya (Ronado)
Arthur=Arturi badala ya (Adha)
Maguire=Maguire badala ya (Magwaya)
Bailly=Baili badala ya (Beil)
Carvajal=Charvajali badala ya (Kavahal)
Harry Kane=Hari Kane badala ya (Heri Keni)
Kieran Trippier=Kierani Tripieri badala ya (Kiran Tripia)

https://www.jamiiforums.com/threads...zi-majina-maneno-fulani-yanatamkwaje.1582412/
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom