Mkuu Nape, gari unaloendesha matairi yametoboka. Huta fika kwa mziba pancha.

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Dereva makini kabla ya kuanza safari yake ni lazima ahakikishe usalama na uzima wa gari analoendesha. Gari analojaribu kusafiri nalo huyu kijana mwenzetu Nape (CCM) Linahitaji marekebisho makubwa, jambo baya zaidi. Safari ameshaianza, hana utingo, hana spana, jeki wala tairi la akiba. Tayari matairi yametoboka, anajaribu kwenda kasi ili awahi kufika kwa mziba pancha kabla upepo haujaisha. Mkuu jipange upya kwa safari, safari ni ndefu. Anzia gereji kwanza kwa wataalamu, warekebishe gari lako unalolipenda sana (CCM) Ndipo uanze safari, vinginevyo siku moja utakuja sema unategewa misumari njiani kumbe tairi za gari lako ndiyo kipara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom