Mkuu mpya Mkoa wa Dar es Salaam ni mfano mzuri wa kuigwa kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya

Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
14,210
13,723
Nimefarijika sana pale nilipomsikia mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam alipokuwa anajitambulisha na kuongea na wazee wa mkoa. Huyu mteule anaonekana kutokana na maneno yake kuwa ni mtu wa busara na mwenye maono ya uongozi; amegundua kuwa wazee ni hazina kubwa kwa kiongozi yeyote yule kwani wameishi na wameona mengi; ushauri wao ni muhimu katika kufanikisha maendeleo ya mahala popote pale hivyo wana nafasi ya pekee katika jamii.

Bahati mbaya sana kuwa wateule wengi sana wa Rais wa siku hizi hasa vijana hawathamini mchango wa wazee katika mafanikio ya nchi hii. Hawatambui kuwa bila mchango wa hawa wazee wasingefika hapo walipo; hapo walipo wamesimama juu ya mabega ya hawa wazee hivyo hawana budi kuwapa heshima yao wanayostahili.

Rais Magufuli anawaonesha mfano kwa kuwaheshimu watangulizi wake na ndio maana hawaachi katika shuhuli muhimu za nchi na pia kupata ushauri kutoka kwao. Sio hivyo kwa wengi wa MaRC na MaDC wake kwani wao hawana heshima kabisa kwa wazee bali hata MaRC na MaDC waliostaafu hawapati heshima wanayostahili wanapokuwa na shida katika ofisi zao.

Haipendezi kuona Mkuu wa Mkoa mstaafu amekaa kwenye mstali akingojea kumuona kijana DC ofisini kwake! Hii inatokea sana kwa Hawa vijana wa siku hizi wanaodhani wamefika hapo kwa nguvu zao wenyewe.

Mkuu wa mkoa wa Dar katika maongezi yake na wazee amewaagiza wasaidizi wake hapo katika mkoa wake kuwa hawana budi kuwaheshimu wazee sio wale waliokuwa na wadhifa tu hapo nyuma bali wazee wote kwani hao ni hazina ya nchi.

Ingependeza sana kama mfano huu wa agizo la huyu mkuu wa mkoa wa DAR lingetolewa kwa MaRC na Ma DC wote nchi nzima na hasa hasa Hawa MaDC vijana. Unfortunately, hawasomi historia ya nchi hii na ndio maana haishangazi kuwa hawawajui wale waliowatangulia ingawa juhudi zimefanywa kuwaorodhesha kwenye mabango katika ofisi zao!
 
Kuna DC wake wanaeshea domicile anaweza kuwa rc muda wowote mkoani hapo baada ya Kune kuteuliwa ubunge na wizara juu
 
Back
Top Bottom