Mkuu huyu wa wilaya vipi?

Nemesis

JF-Expert Member
Feb 13, 2008
5,460
4,359
Walioandamana kumpinga Dk. Ngasongwa kushitakiwa

na George Maziku

WANANCHI walioandamana wilayani Ulanga, mkoani Morogoro kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kumwacha Dk. Juma Ngasongwa katika uteuzi mpya wa Baraza la Mawaziri alioufanya hivi karibuni, wameingia matatani na wanaweza kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa, Tanzania Daima imegundua.

Katika hali ya kushangaza na inayoashiria kuwa suala hilo lina shinikizo la kisiasa, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Dk. Rajabu Rutengwe na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo Suleiman Magoto, ndio wanaoshika bango la kutaka wananchi hao washitakiwe.

“Tumeamua kuwakamata na kuwafikisha mahakani watu wote walioandamana siku hiyo kwa sababu maandamano yao hayakuwa na kibali,” alisema mkuu huyo wa wilaya alipozungumza na gazeti hili juzi kupitia simu yake ya kiganjani.

Pia mwandishi wa habari wa gazeti lililoripoti kuhusu maandamano hayo (si Tanzania Daima) anatafutwa na viongozi hao wa serikali na CCM ili aunganishwe na wananchi hao kujibu mashitaka yanayowakabili.

Dk. Rutengwe anamlalamikia mwandishi wa gazeti lililoandika habari ya maandamano hayo kwa kile alichodai kuwa kwanza mwandishi hakuwa na kibali cha viongozi wa wilaya hiyo cha kumruhusu kuripoti habari hiyo, pili habari yenyewe ni ya kuchochea chuki.

“Huyu mwandishi kwanza ni mchochezi, anaandika habari za kuchonganisha wananchi na viongozi wao, na isitoshe hakupata kibali chetu kama viongozi wa wilaya kumruhusu kuandika habari hiyo, hayo ni makosa makubwa”, alisisitiza Dk. Rutengwe.

Siku mbili tu baada ya Rais Kikwete kutangaza baraza jipya la mawaziri, kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa, ambapo aliwatupa nje baadhi ya mawaziri waliokuwa katika baraza la kwanza akiwemo Dk. Ngasongwa, gazeti moja la kila siku liliripoti kuwa wananchi wa tarafa za Malinyi na Mtimbira wilayani humo, waliandamana kumpongeza Rais Kikwete kwa kutomteua Dk. Ngasongwa katika baraza hilo.

Naye mwenyekiti wa CCM wilayani humo, aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu ya kiganjani kuwa uongozi wa chama hicho wilayani Ulanga ulikuwa umekasirishwa mno na kitendo cha wananchi hao kuandamana kwa kumkejeli Dk. Ngasongwa, ambaye ni mmoja wa wabunge wawili wa CCM wilayani humo.

“Tumekubaliana na DC ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya yetu kuhakikisha watu wote walioandamana, pamoja na mwandishi aliyeandika habari hiyo wanakamatwa na kufikishwa mahakamani haraka.

“Si uungwana hata kidogo watu kushangilia kuanguka kwa mwenzao. Ngasongwa bado ni mbunge, kitendo cha kuandamana kumpongeza rais na kumkejeli mbunge ni kosa, ni lazima wahusika watuambie wamepata wapi utamaduni huo,” alisisitiza Magoto.

Lakini wananchi walioshiriki maandamano hayo, walipoongea na gazeti hili kwa njia ya simu za kiganjani, kwa nyakati tofauti na kwa sharti la kutotajwa, walisema hawakufanya kosa lolote kwa kuandamana kumpongeza rais wao kwa kuteua baraza zuri la mawaziri.

Pia walisema hawakutenda kosa lolote kwa kuonyesha hisia zao dhidi ya mbunge wao, ambaye walidai hajatekeleza ahadi nyingi alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2005, na kwamba kama watakamatwa na kushitakiwa kwa kitendo hicho basi huo ni udikteta wa hali ya juu.

“Hii ni demokrasia gani? Hivi kweli hata tukitaka kumpongeza rais kwa kazi nzuri lazima tuombe kibali? Huyu DC ni wa kizazi kipi? Mbona anataka kubana uhuru wa binadamu?” alihoji mmoja wa watu walioshiriki maandamano hayo ambaye aliliambia gazeti hili kuwa huenda yeye akawa mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo.

Hata hivyo, baadhi ya watu walioshiriki maandamano hayo wameapa kupambana na kwamba wapo tayari kufunga safari kwenda Dar es Salaam kuonana na Rais Kikwete, ili wamfikishie kilio chao kuhusu manyayaso waliyodai kuyapata kutoka kwa viongozi wao wa wilaya kutokana na kitendo chao cha kuandamana kumuunga mkono.
 
Wakuu kwa kuanzia mi ni hapo tu,

Tangu lini waandishi wakahitaji kibali cha uongozi kuripoti habari? hii ipo kwenye sheria zipi katika nchi yetu? habari zote tunazopata kwenye media huwa zina vibali vya viongozi?

Na hilo la kuwakamata wananchi, wangeandamana kumpongeza Ngasongwa kuchaguliwa kuwa waziri maandamano yao yangekuwa haramu?
 
Asante Lowasa na mtandao . Ngasongwa ni corrupt na mnafiki so anawatumia pia hawa jamaa .
 
Wakuu kwa kuanzia mi ni hapo tu,

Tangu lini waandishi wakahitaji kibali cha uongozi kuripoti habari? hii ipo kwenye sheria zipi katika nchi yetu? habari zote tunazopata kwenye media huwa zina vibali vya viongozi?

Na hilo la kuwakamata wananchi, wangeandamana kumpongeza Ngasongwa kuchaguliwa kuwa waziri maandamano yao yangekuwa haramu?

Wananchi walifurahi na kushangilia, sasa Mkuu wa Wilaya na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya wanataka washtakiwe kwa kosa la kufurahia siku Mbunge wao alipo kosa Uwaziri. Je ni sheria ipi itakayo tumika?.
 
[/COLOR]

wamesha katiwa kao ka mrahaba so wanaendelea kunyonya na kuonyesha kwamba akili zao hazina akili . Mashitaka haya anaye lalamika ni Mkuu wa Wilaya na CCM dhidi ya wapiga kura au ni kitu gani ? Wanajichimbia kaburi sasa maana watu watagoma na hapo JK itabidi aseme ama Pinda aende huko.
 
Walioandamana kumpinga Dk. Ngasongwa kushitakiwa

na George Maziku

WANANCHI walioandamana wilayani Ulanga, mkoani Morogoro kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kumwacha Dk. Juma Ngasongwa katika uteuzi mpya wa Baraza la Mawaziri alioufanya hivi karibuni, wameingia matatani na wanaweza kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa, Tanzania Daima imegundua.

Katika hali ya kushangaza na inayoashiria kuwa suala hilo lina shinikizo la kisiasa, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Dk. Rajabu Rutengwe na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo Suleiman Magoto, ndio wanaoshika bango la kutaka wananchi hao washitakiwe.

“Tumeamua kuwakamata na kuwafikisha mahakani watu wote walioandamana siku hiyo kwa sababu maandamano yao hayakuwa na kibali,” alisema mkuu huyo wa wilaya alipozungumza na gazeti hili juzi kupitia simu yake ya kiganjani.

Pia mwandishi wa habari wa gazeti lililoripoti kuhusu maandamano hayo (si Tanzania Daima) anatafutwa na viongozi hao wa serikali na CCM ili aunganishwe na wananchi hao kujibu mashitaka yanayowakabili.

Dk. Rutengwe anamlalamikia mwandishi wa gazeti lililoandika habari ya maandamano hayo kwa kile alichodai kuwa kwanza mwandishi hakuwa na kibali cha viongozi wa wilaya hiyo cha kumruhusu kuripoti habari hiyo, pili habari yenyewe ni ya kuchochea chuki.

“Huyu mwandishi kwanza ni mchochezi, anaandika habari za kuchonganisha wananchi na viongozi wao, na isitoshe hakupata kibali chetu kama viongozi wa wilaya kumruhusu kuandika habari hiyo, hayo ni makosa makubwa”, alisisitiza Dk. Rutengwe.

Siku mbili tu baada ya Rais Kikwete kutangaza baraza jipya la mawaziri, kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa, ambapo aliwatupa nje baadhi ya mawaziri waliokuwa katika baraza la kwanza akiwemo Dk. Ngasongwa, gazeti moja la kila siku liliripoti kuwa wananchi wa tarafa za Malinyi na Mtimbira wilayani humo, waliandamana kumpongeza Rais Kikwete kwa kutomteua Dk. Ngasongwa katika baraza hilo.

Naye mwenyekiti wa CCM wilayani humo, aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu ya kiganjani kuwa uongozi wa chama hicho wilayani Ulanga ulikuwa umekasirishwa mno na kitendo cha wananchi hao kuandamana kwa kumkejeli Dk. Ngasongwa, ambaye ni mmoja wa wabunge wawili wa CCM wilayani humo.
“Tumekubaliana na DC ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya yetu kuhakikisha watu wote walioandamana, pamoja na mwandishi aliyeandika habari hiyo wanakamatwa na kufikishwa mahakamani haraka.

“Si uungwana hata kidogo watu kushangilia kuanguka kwa mwenzao. Ngasongwa bado ni mbunge, kitendo cha kuandamana kumpongeza rais na kumkejeli mbunge ni kosa, ni lazima wahusika watuambie wamepata wapi utamaduni huo,” alisisitiza Magoto.

Lakini wananchi walioshiriki maandamano hayo, walipoongea na gazeti hili kwa njia ya simu za kiganjani, kwa nyakati tofauti na kwa sharti la kutotajwa, walisema hawakufanya kosa lolote kwa kuandamana kumpongeza rais wao kwa kuteua baraza zuri la mawaziri.

Pia walisema hawakutenda kosa lolote kwa kuonyesha hisia zao dhidi ya mbunge wao, ambaye walidai hajatekeleza ahadi nyingi alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2005, na kwamba kama watakamatwa na kushitakiwa kwa kitendo hicho basi huo ni udikteta wa hali ya juu.

“Hii ni demokrasia gani? Hivi kweli hata tukitaka kumpongeza rais kwa kazi nzuri lazima tuombe kibali? Huyu DC ni wa kizazi kipi? Mbona anataka kubana uhuru wa binadamu?” alihoji mmoja wa watu walioshiriki maandamano hayo ambaye aliliambia gazeti hili kuwa huenda yeye akawa mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo.

Hata hivyo, baadhi ya watu walioshiriki maandamano hayo wameapa kupambana na kwamba wapo tayari kufunga safari kwenda Dar es Salaam kuonana na Rais Kikwete, ili wamfikishie kilio chao kuhusu manyayaso waliyodai kuyapata kutoka kwa viongozi wao wa wilaya kutokana na kitendo chao cha kuandamana kumuunga mkono.

Ukishangaa ya musa utayaona ya filauni. Haya ya filauni ndiyo haya sasa,hivi huyu mkuu wa wilaya ni doctor by proffesional au ni PhD holder? Yale ya Prof.Watson kuhusu akili za watu weusi ndiyo haya sasa,toka lini mwandishi wa habari akaomba kibali cha kutoa habari?Ingekuwa hivyo nafikiri tusingekuwa na magazeti nchi hii.Hapa amechemsha kabisa huyu mkuu,hii ndiyo aina ya viongozi tulionao ambao hupenda kutumia mfumo mfu wa sheria za nchi kukandamiza raia
Na huyu mwenyekiti wa CCM( fikira za mwenyekiti wa chama zidumu),huyu ni aina ya kiongozi ambao wanaendelea kuwakumbatia viongozi ambao hawawatumikii wananchi. Huwezi kuwazuia wananchi kuonyesha hisia zao juu ya kiongozi wao,kama ngasongwa hafanyi kitu,haya ndiyo majibu sahihi. Ndugu mwenyekiti pamoja na mbunge wako,someni alama za nyakati
 
Huyu kalewa madaraka na kudhani yeye ni bora zaidi ya wengine Tanzania .
 
Mods, nadhani thread hii iunganishwe na ile ya 'walioandamana kuhusu Dr. Ngasongwa kushtakiwa.
 
dR.rUTENGWE ANACHOFANYA NI KUENDELEA KUMHARIBIA NGASONGWA MAANA HAKUKUWA NA MAANDAMANO YOYOTE HUKO NA SASA CCM WAMEKOMAA WANAMTAKA ATHIBISHE AU AKANUSHE NA KIBAYA ZAIDI WATU WALITAJWA HUMO MAGAZETINI WAMEMLALAMIKIA KWA KUTUMIA MAJINA YAO KTK KUMCHAFUA NGASONGWA.

HANA NAMNA LAZIMA AANZE KUWATISHA WATU
 
Dr Rutengwe, amechemsha sana, yeye alidhani anajikomba kwa Ngasongwa + CCM. Shida inayoonekana hapo ni kwamba huyu DC ni Doctor. Wasomi kama huyu tunategemea wafanye kazi kwa utalaam na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma (among that ni kutofanya kazi kwa manufaa binafsi au kwa kutarajia kupata zawadi au tuzo).
Hofu nyingine, huenda watendaji wenye tabia hizi wapo wengi.
 
Back
Top Bottom