Mkuu haya yana baraka zako kweli? Badilisha wasaidizi wako

Lakasa chika7

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
454
1,264
Mkuu hii Nchi yetu yote. Katika maisha usitake kupendwa na watu wote. Hata Bwana Yesu na Mtume Muhammad kuna watu waliwapinga na hadi Leo kuna baadhi ya watu hawaamini nguvu zao. Katika maisha ya siasa hasa za vyama vingi lazima ukubali kupingwa. Haiwezekani kila MTU awe CCM. Hilo halitawezekana hadi kiama kinafika.

Sisi wafrika nahisi kuna MTU katuloga aisee. Na aliyetuloga amekufa.
Haiwezekani umekuwa mkubwa wa Nchi badala ya kupambana uletee maendeleo kwa hizo few resources ulizonazo wewe unapambana na watani wako kisiasa. Hapana lazma mstari uchorwe wa mwisho.

Tunaona watani wako wa kisiasa mara hotel zao zimevunjwa, ukumbi za starehe wengine kijani wenzako lakini wanasulubiwe kwakuwa hawakuwa kambi yako. Eti ameajiri wageni, mara fukuza kwenye pango.

Wengine tunajua uchaguzi umeisha kumbe wengine bado mpo kwenye Kampeni.

Bado mimi ninaimani na wewe sana, hata wasaidizi wako wawili wakuu VP na PM. Nina amini haya yanatokea bila baraka zako, naamini hivyo huwezi wewe kuwatuma wasaidizi wako chini wafanye harassment kwa wafanyabiashara ambao hawakuungi mkono.

Mkuu watoe wote wasaidizi ambao wana suppress upinzani. Wanakuharibia wewe unachukiwa sana mtaani. Mvuto wako umepungua sana. Hawa wakina Mbowe ni watanzania kama wewe waache wafanya biashara zao km wengine. Msuguane kwenye siasa tu tena kwa hoja siyo kwenye social & economic ya MTU.

Tafuta legacy ya kimaendeleo ..Leo hata ukiondoka tuseme mzee wetu alifanya hili na lile. Isifikie hatua watu waombee muda wako uishe.

Kuwadhoofisha kiuchumi watani wako haiondoi dhana ya mabadiliko iliyoingia kwa Watanzania. Watanzania waliowengi wanaamini ukiitoa Ccm Nchi itapata maendeleo, kazi yako km mkuu prove them wrong, na wajue kuwa maendeleo yataletwa na CCM.

KUNA WATU WANASEMA UNAUTHUBUTU SANA BUT UNATHUBUTU KWENYE WRONG DECISIONS.
Badilisha wasaidizi wako, wengi wapo kinafki sana..ngoja ustaafu utawasikia wakikunanga km wanavyomnanga bwana yule wa msoga wakati nao walikuwa serikalini.

Au tumeingia kwa haraka kwenye mfumo wa vyama vingi.

Kwa visasi hatutofika.

Nakumbuka kauli ya bwana yule wa msoga 'Nataka nikistaafu nikumbukwe kama bwana Maendeleo'
 
wewe ndio unamchukia mh rais..sisi tunampenda sana

wapinzani wenyewe hawa wasio na hoja wana faida gani
 
Hayo mambo yana baraka zake na yeye Ni mtu wa visasi na ndo maana hata kuna baadhi ya maeneo hapa nchini hatoweza kukanyaga kamwe mpaka mwisho wa uongozi wake na hili lilidhihirika mkoa wa Kagera mpaka alipoambiwa na chama. Lakini Kuna maeneo kuyatembelea na kutatua kero zao ni kugusa tu hasa yale ya kina Ngosha.
 
Mkuu hii Nchi yetu yote. Katika maisha usitake kupendwa na watu wote. Hata Bwana Yesu na Mtume Muhammad kuna watu waliwapinga na hadi Leo kuna baadhi ya watu hawaamini nguvu zao. Katika maisha ya siasa hasa za vyama vingi lazima ukubali kupingwa. Haiwezekani kila MTU awe CCM. Hilo halitawezekana hadi kiama kinafika.

Sisi wafrika nahisi kuna MTU katuloga aisee. Na aliyetuloga amekufa.
Haiwezekani umekuwa mkubwa wa Nchi badala ya kupambana uletee maendeleo kwa hizo few resources ulizonazo wewe unapambana na watani wako kisiasa. Hapana lazma mstari uchorwe wa mwisho.

Tunaona watani wako wa kisiasa mara hotel zao zimevunjwa, ukumbi za starehe wengine kijani wenzako lakini wanasulubiwe kwakuwa hawakuwa kambi yako. Eti ameajiri wageni, mara fukuza kwenye pango.

Wengine tunajua uchaguzi umeisha kumbe wengine bado mpo kwenye Kampeni.

Bado mimi ninaimani na wewe sana, hata wasaidizi wako wawili wakuu VP na PM. Nina amini haya yanatokea bila baraka zako, naamini hivyo huwezi wewe kuwatuma wasaidizi wako chini wafanye harassment kwa wafanyabiashara ambao hawakuungi mkono.

Mkuu watoe wote wasaidizi ambao wana suppress upinzani. Wanakuharibia wewe unachukiwa sana mtaani. Mvuto wako umepungua sana. Hawa wakina Mbowe ni watanzania kama wewe waache wafanya biashara zao km wengine. Msuguane kwenye siasa tu tena kwa hoja siyo kwenye social & economic ya MTU.

Tafuta legacy ya kimaendeleo ..Leo hata ukiondoka tuseme mzee wetu alifanya hili na lile. Isifikie hatua watu waombee muda wako uishe.

Kuwadhoofisha kiuchumi watani wako haiondoi dhana ya mabadiliko iliyoingia kwa Watanzania. Watanzania waliowengi wanaamini ukiitoa Ccm Nchi itapata maendeleo, kazi yako km mkuu prove them wrong, na wajue kuwa maendeleo yataletwa na CCM.

KUNA WATU WANASEMA UNAUTHUBUTU SANA BUT UNATHUBUTU KWENYE WRONG DECISIONS.
Badilisha wasaidizi wako, wengi wapo kinafki sana..ngoja ustaafu utawasikia wakikunanga km wanavyomnanga bwana yule wa msoga wakati nao walikuwa serikalini.

Au tumeingia kwa haraka kwenye mfumo wa vyama vingi.

Kwa visasi hatutofika.

Nakumbuka kauli ya bwana yule wa msoga 'Nataka nikistaafu nikumbukwe kama bwana Maendeleo'

Umeongea ukweli kabisa lakini wakija Kijani hapa watakutukana mpaka ukome.

Any way kwa kawaida Chuki na visasi hazijengi taifa lolote lile. Muda msingi Serikali inaweza namna gani ya kumdhoofisha Mbowe na Lissu badala ya kuwapa namna gani ya kuleta Maendeleo kwa Watanzania.

Waliohujumu uchumi wa Tanzania ni wanachama na Viongozi walio ndani ya CCM ambao ameapa hata wagusa.Wanaoguswa Ni Wapinzani ambao wengi wao wamepata utajiri kupitia wazazi wao enzi za ukoloni.

Wivu na Chuki vinatupeleka pabaya sana.Mwisho wa siku hakutakiwa Taifa moja tena.

Nilitegemea Viongozi wa dini watusemee kwenye hili lakini hata wao wanachangia kwa sababu ya kuongeza hata Upuuzi.

Unapongeza madawa ya kulevya wakati hakuna hata MTU aliyekamatwa anayeuza na kusafirisha madawa hayo.Wanaokamatwa ni wale walio tofauti na wao.

Siku wanachama wa CCM watakapokuja kushtuka kwamba chote hicho ni jioni macho basi wengi tutakuwa tumeumia
 
Sidhani kama anapotoshwa na wasaidizi wake...

Yeye amejifanya kuwa "Alfa na Omega",hataki kushauriwa wala kuhojiwa,hataki discussion kwe Yale anayotaka kuyafanya,hivyo basis kwa kuwa wasaidizi wake(wengi kama sio wote) ni wachumia tumbo wanaogopa kwenda kinyume naye.
 
wewe ndio unamchukia mh rais..sisi tunampenda sana

wapinzani wenyewe hawa wasio na hoja wana faida gani

Haya nyie wenye hoja mmeshafanya nini??Mpaka sasa mmeongeza ajira au mmepunguza ajira na kuongeza waliokuwa na kazi mtaani kwa kufanya Chuki na visasi kwa wasio wachagua??

Niambie mpaka sasa alichofanya Mwenyekiti wa CCM ni kipi??Sana anachofanya ni kunyanyasa Wapinzani tu.Miaka.mitano atajibu nini??Kajenga Uwanja wa ndege Chato, duka la.madawa Chato,Jengo la TRA Chato,Barabara zote Chato,ambulance Chato yaani kila kitu ni Chato Chato Chato.Miaka mitano Unajua Chato Chato.
 
  • Thanks
Reactions: 999

kwani chato ipo JAMAICA ?
 
Tafakuli : linganisheni maendeleo ya wilaya CHATO na jirani zao BIHARAMULO.

MIMI nabaki hapa hapa
 
Wakati chato ilikuwa ndani ya wilaya ya Biharamulo kabla haijawa wilaya.. Na umeme unaotumika chato unatoka kwenyw Generator lililopo Biharamulo
 
Kuna watu hudhani ukiwa Chadema ndo uko kwenye chama kinachojali wananchi wake

Kuna wengine kila wakati hudhani ccm ina nia njema juu yao

Ushauri tu: usiwekeze moyo wako juu ya chama fulani utaumia pale utakapoona ulichotegemea kifanywe na chama chako bado hakifanyiki
 
wewe ndio unamchukia mh rais..sisi tunampenda sana

wapinzani wenyewe hawa wasio na hoja wana faida gani
Hata Kama nchi nzima isingekuwa na mpinzani kwa hali ilivyo wewe binafsi ulitakiwa kuwa mpinzani, sasa unapigana na wapinzani? Hujielewi!
 
Back
Top Bottom