Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,519
- 217,785
Waliokuwa Wagombea ubunge wa Chadema kwenye ule uchaguzi hewa wa 2020 , wamefunguka leo chanzo cha wao kuzuiwa kuingia ndani ya gereza la Ukonga kumuona Mwenyekiti wao Freeman Mbowe, katika siku halali na muda muafaka wa kuona Mahabusu.
Wamefunguka yote haya katika Mkutano wao na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Chama hicho huko Kinondoni, Mkoani Dar es Salaam.
Kisingizio cha Corona kilichotolewa na Mkuu wa gereza hilo kimepuuzwa vikali na wadau kwa madai kwamba hakuna corona popote duniani inayobagua watu kutokana itikadi ya siasa, kwamba wazuiliwe Chadema waliopata chanjo na huku wakiwa na tahadhari zote za corona, ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa na Sanitizer za kutosha, lakini watu wengine tena waliokimbia chanjo na wasiochukua tahadhari yoyote waruhusiwe, Maajabu!
Bali inafahamika kwamba Mkuu huyo wa Gereza aliamua kuwazuia Chadema ili apeleke Ushawishi kwa Mamlaka za uteuzi za CCM ili apandishwe cheo zaidi, hii ni kutokana na uzoefu wa miaka mingi wa viongozi wa serikali ya CCM kuwapandisha vyeo wale wote wanaojitolea kuwatesa Viongozi na wanachama wa Chadema nchi nzima.
Video hii hapa.
View attachment 1986460
Pia soma: Msemaji wa Magegereza aanika Sababu Makada wa Chadema kuzuiwa kumuona Mbowe