Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,608
Binafsi nadhani "mkuu" kabisa anaingilika na anashaurika vizuri tu.
Tatizo lipo kwenye mazoea ya ushauri waliyonayo washauri kwa maana ya wale wanaoteuliwa kumsaidia kwenye wizara mbalimbali.
Mshauri anapozoea kushauri kisiasa kwa nia ya kumpamba yule anayemshauri basi upo uwezekano wa kujikuta anaishi kama mpambe badala ya mshauri kwa maana ya msaidizi mkuu wa utekelezaji wa sera na mambo nyeti ya kitaifa.
Nimegundua kuwa "mkuu" anapenda zaidi substance kwenye ushauri wa mtu zaidi ya blah blah za kisiasa, hataki upambe anataka ushauri ili na yeye aweze kutoa maagizo kutokana na upana wa ushauri anaopewa.
Anaweza kuwa na udhaifu kwa maana ya wakati mwingine uwepo wa jazba, lakini anasikiliza zaidi ujazo wa hoja ya mtoa hoja na sio tabia ya kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa.
Wasaidizi wake wanao mtihani wa kujifunza kuwa na tabia ya kujiamini wakati wanapowakilisha hoja, wengi ndio zile shahada za uzamivu hivyo ni lazima waijue sanaa wa uwakilishaji wa hoja zao.
Mshauri wa "mkuu" kabisa ambaye unaamini katika uwezo wako na elimu yako kwanini ushindwe kuwa na ushawishi wakati unawakilisha hoja zako?.
Naamini washauri watakuwa wameshajifunza kitu fulani ndani ya huu mwaka wa kwanza wa awamu ya tano.