Mkutano wa wana MMU kwa ajili ya kujumuika

Simplicity.

JF-Expert Member
Dec 19, 2013
2,636
1,661
Ndugu wapendwa,

Naandaa mkutano wa wanaMMU, lengo ni kukutana kimwili (physically) kwa ajili ya kujamiana (kusocialize).

Naamini mkutano huo utatoa fursa ya kufahamiana, kubadilishana mawazo, kushirikiana na hata kuanzisha mahusiano, urafiki na mapenzi imara zaidi.

Katika mkutano huo hakutakuwa na kujuana kwa majina yetu ya JF, ila kama mtu una wasiwasi wa kuwepo mamluki, unaweza tu kumwuuliza maswali machache kuhusiana na MMU, mfano, hebu mwelezee lara 1 wa MMU kwa sentensi moja, au malizia hili jina maarufu la mwana MMU: miss ******, n.k., Nasisitiza kuwa hakutakuwa na kufahamiana majina yetu ya humu (mimi mwandaaji hamtanifahamu pia).

Kipekee nataka kuitumia fursa hii kupata mchumba. Tupeane ushauri wa mahali pa kukutania (ukumbi), Tarehe, muda n.k. Kutakuwa na vinywaji na bites ambazo mimi nitagharimia 100% ya kila kitu, vitu vingine mtajinunulia wenyewe. Baada ya kuridhia huu mkutano na kukubaliana taratibu zingine, nitamwomba mwana MMU mmoja maarufu, aanzishe thread ya kukusanya idadi ya watakaohudhuria.

Karibu kwa maoni.
 
Mkutano uwe dar, sehemu nzuri ni Mensuma makumbusho, au milenium tower au kijiji cha makumbusho
 
Nyie wa mkoani karibuni pia, tutafanya Dar kwanza. Kama kutakuwa na mikutano ya mikoani, tutawajuza.
 
Good idea. Mkuu fanya mchakato tukutane,hata contribution tutatoa,ila iwe jumamosi,na hasa mwisho wa mwezi,kwa maslahi ya wengi.
 
Ndugu wapendwa,

Naandaa mkutano wa wanaMMU, lengo ni kukutana kimwili (physically) kwa ajili ya kujumuika (kusocialize).

Naamini mkutano huo utatoa fursa ya kufahamiana, kubadilishana mawazo, kushirikiana na hata kuanzisha mahusiano, urafiki na mapenzi imara zaidi.

Katika mkutano huo hakutakuwa na kujuana kwa majina yetu ya JF, ila kama mtu una wasiwasi wa kuwepo mamluki, unaweza tu kumwuuliza maswali machache kuhusiana na MMU, mfano, hebu mwelezee lara 1 wa MMU kwa sentensi moja, au malizia hili jina maarufu la mwana MMU: miss ******, n.k., Nasisitiza kuwa hakutakuwa na kufahamiana majina yetu ya humu (mimi mwandaaji hamtanifahamu pia).

Kipekee nataka kuitumia fursa hii kupata mchumba . Tupeane ushauri wa mahali pa kukutania (ukumbi), Tarehe, muda n.k. Kutakuwa na vinywaji na bites ambazo mimi nitagharimia 100% ya kila kitu, vitu vingine mtajinunulia wenyewe. Baada ya kuridhia huu mkutano na kukubaliana taratibu zingine, nitamwomba mwana MMU mmoja maarufu, aanzishe thread ya kukusanya idadi ya watakaohudhuria.

Karibu kwa maoni.

Ehh kumbe ndo dhamira yako basi tumekuelewa,kama unapesa sana kwanini usitoe msaada kwa wenye uhitaji eg yatima nk.
 
Kwani mimi kunufaika kwa kutafuta mchumba ni vibaya? Acha wivu, unajuaje kama nitaibuka na dada yako! Wewe jamaa, utaniheshimu kwa kuniita shem, ala.
 
Back
Top Bottom