Mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika(AU) unaendelea mjini Addis Ababa. Rais wa Tanzania amejifungia nyumbani

Wanabodi nawasalimu


Tanzania ilikuwa baba wa demokrasia,utu wema,kisiwa cha amani na utulivu mpaka ikawa kimbilio la walioteseka na majanga mbalimbali nchini kwao lakini leo sina hakika kama bado tunayo sifa hiyo.
Hapo pichani ni Mhe.uhuru kenyatta rais wa kenya akijadiliana na mhe.raila amollo odinga(Mpinzani wake mkuu)ambaye ni afisa maalum wa umoja wa afrika aliyepata nafasi hiyo baada ya kupendekezwa na kenyatta mwenyewe.
Wenzetu wamepiga hatua ndefu mbele huku sisi tukipiga sarakasi kwa mbio za relay kurudi nyuma miaka ya 1970.
Sifa moja tuliyo nayo ni kupigana risasi na kuwekana ndani kwa kesi bandia.

Nimeangaza angaza kama nitamuona mtukufu wetu mhe.John Magufuli kikaoni lakini nimeambulia patupu sijui anaumwa miaka mitatu mfululizo au ni ile aleji ya kutosafiri ndiyo inaendelea hata kwenda kuungana na wakuu wa nchi wenzake duniani inakuwa shida?

Jamani hata wawekezaji kama kina dangote hawakuja wenyewe au kushawishiwa na mabalozi,makamu wa rais au waziri mkuu,wanahitaji kuonana au kuhakikishiwa mazingira bora na mkuu wa nchi na hasa kwenye mataifa yetu yasiyotabirika kwenye nyanja ya haki za binadamu,utawala wa sheria,demokrasia na uhuru wa kiuchumu.

Kikwete alifanya kazi ya ziada kuwaleta na kuwahakikishia mazingira bora na rafiki kikodi,kiusalama na kimalighafi na ndiyo maana baada ya kuondoka ikulu sidhani kama kuna uwekezaji mkubwa kutoka nje kwa wafanyabiashara umekuja nchini zaidi ya kuhangaika na hawa kina Mo wanaopitia mkono wa chuma na kuhamisha mitaji nje ya nchi kunusuru mitaji na usalama wao.

Serikali ya viwanda imeota mbawa na haisikiki tena abadan,labda uwe na roho ngumu kama ya mwendawazimu kuunadi uchumi wa viwanda na tanzania mpya ya Magufuli.
Huwezi kutengeneza kitu kinachohitaji kanuni kwa kuigiza au kuwakusanya viongozi wa dini ikulu na airport kuwaaminisha wananchi kuwa uchumi uko imara tena viwanda vimejengwa zaidi ya 3500 toka mwaka 2016-2019.
Watakuja kwenye nyumba za ibada kuhubiri porojo na maagizo ya ikulu lakini watapuuzwa kwa sababu watu wanataka wapate neno la Mungu huko na siasa kwa wanasiasa.

Watu wanaona,wanajua na wanaelewa na wakinyamaza si kwamba wamekukubalia,wanakaa kimya kuepusha shari.
Najua kuna watu watabeza safari za lazima za rais kama hizi za A.U,U.N nk.
Shida siyo wao kubeza bali ni kwa kiasi gani wanauelewa mpana kuhusu safari hizi na ushawishi wa rais kiuchumi,kibiashara na kidiplomasia.
Sidhani kama dunia ilikuwa inamfahamu mtu anayeitwa mhe.rais John Pombe Magufuli kabla ya mhe.sana Tundu Lissu kupigwa risasi na kumtambulisha duniani.

Jamani nawasilisha mimi nilikuwa nawaza kuhusu mikutano ya kimataifa na umuhimu wa mkuu wa nchi kuwepo kwa maslahi mapana ya taifa na afya yake kiuchumi na kidiplomasia.
Kama mtasema siyo muhimu basi aendelee kujifungia halafu tutajua huko mbeleni kama baba wa familia anawezaje kujifungia na kapu la fedha chumbani akitumia bila kuingiza kama zitadumu.
Ukitaka Kula sana lazima ukubali kuliwa kidogo lakini kama unahisi wenzako hawastahili kula vyako basi watakutenga na utaishi mpweke kama shetani na ukipata janga utalia mwenyewe.

Ni mimi mzalendo wa kweli wa taifa Deus Mkombozi Kira.



NB: Picture upload failed
We ni mseng kweli hizo jumuiya mlizojiunga zimewasaidia nini hasa cha maana zaidi ya kuwatia umaskini?nenda basi wewe kamuwakilishe kama kuna umuhimu,mmekuwa na akili mbichi kila kukicha masimango kwa rais tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka sasa AU haina maana ni maonyesho ya mitindo ya mavazi na umwinyi! Muulize Mr Julius Malema wa EFF South Africa atakueleza vizuri. Sioni kama inafaa raisi wetu ambaye yuko bise kulinyoosha taifa lililo kuwa linakwenda kombo anapaswa kupoteza muda kwenda kwenye hicho chombo. Afadhali awatume wengine. Nchi ikinyooka wawekezaji wa maana watakuja, siyo wale wanaotaka kutuibia - tumeibiwa saaaaana! Inatosha.
Tumeibiwa sanaaaaa chini ya chama hiki hiki cha ccm.Hakuna jipya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Anataka avunje masharti ya mganga la kwanza Hakuna kusafiri nnje hasa kupanda ndege ,la pili Hakuna kuona maiti ,la Tatu Hakuna kumgusa Bashite ,sasa ICC inanukia sijui ataendaje ,atakeasitake lazima akwee pipa au aende kwa mguu .
Ninyi kama ni malaya basi ni jamvi la wageni mwanzo mlidai kikwete anasafiri sana leo mnasema magufuri hasafiri,mnanataka kulala na nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu uingie madarakani mwaka wa nne sasa umetembelea nchi tatu tu tena ndani ya jumuia yako. Kwanini hausafiri zaidi ya hapo? Tatizo ni nini? Uzalendo?, Lugha?, Kutekwa?, Kupinduliwa?

Mwanzo tulikupongeza kwa kutambua kuwa unabana matumizi kumbe ulikuwa unatafuta UNIQUE MEANS ya kupora hazina ya walipa kodi. Matumizi yasiyoeleweka ndani ya miaka mitatu yanaweza funika gharama za Baba mkubwa Vasco Dagama za kusafiri nje ya nchi yake kwa miaka kumi.

Baba, upinzani wa Upinzani ni mdogo sana ila wewe unauona mkubwa. Kuna upinzani ndani ya chama chako ambao wewe unauona ni mdogo, ila huo ni mkubwa sana na ndio utakaokuondoa kwenye kiti hicho kikuu kuliko vyote nchini. Huu una wafanyabiashara wakubwa, wastaafu mbalimbali na wateule wako. Wanakupimia target tu. Kumbuka kale kagesi hakakuletwa sehemu husika na upinzani wa nje bali wa ndani. Nikuombe tu umshike vizuri kaka wa taifa kwa umbea wake.

Hutapata msamaha wa Mungu kanisani huku nyuma ya pazia unawapangia maovu raia wako. Vilio vya yatima, wajane, ndugu, jamaa na wanaoishi maisha magumu havitakuacha salama.

Teuzi za mara kwa mara za watu wachache wenye maisha yao mazuri zingeweza kuajiri maelfu ya raia ambao wangelipwa mshahara kwa mwezi sawa na posho ya siku moja ya kikao cha mbunge.

Mgabe hakusafiri siku ya kupinduliwa, yote yalimkuta akiwa nchini mwake. Yajayo yanafikirisha.
 
hiyo ni kesi ya uhaini kuipindua serikali iliyochaguliwa na wananchi
 
Tangu uingie madarakani mwaka wa nne sasa umetembelea nchi tatu tu tena ndani ya jumuia yako. Kwanini hausafiri zaidi ya hapo? Tatizo ni nini? Uzalendo?, Lugha?, Kutekwa?, Kupinduliwa?

Mwanzo tulikupongeza kwa kutambua kuwa unabana matumizi kumbe ulikuwa unatafuta UNIQUE MEANS ya kupora hazina ya walipa kodi. Matumizi yasiyoeleweka ndani ya miaka mitatu yanaweza funika gharama za Baba mkubwa Vasco Dagama za kusafiri nje ya nchi yake kwa miaka kumi.

Baba, upinzani wa Upinzani ni mdogo sana ila wewe unauona mkubwa. Kuna upinzani ndani ya chama chako ambao wewe unauona ni mdogo, ila huo ni mkubwa sana na ndio utakaokuondoa kwenye kiti hicho kikuu kuliko vyote nchini. Huu una wafanyabiashara wakubwa, wastaafu mbalimbali na wateule wako. Wanakupimia target tu.

Hutapata msamaha wa Mungu kanisani huku nyuma ya pazia unawapangia maovu raia wako. Vilio vya yatima, wajane, ndugu, jamaa na wanaoishi maisha magumu havitakuacha salama.

Teuzi za mara kwa mara za watu wachache wenye maisha yao mazuri zingeweza kuajiri maelfu ya raia ambao wangelipwa mshahara kwa mwezi sawa na posho ya siku moja ya kikao cha mbunge.

Mgabe hakusafiri siku ya kupinduliwa, yote yalimkuta akiwa nchini mwake. Yajayo yanafikirisha.
Kwanza kabisa nikuhakikishie hakuna wakumpindua Mh.rais na hayupo na hata tokea kamwe katoka ardhi hii ya tanganyika na sababu kuu ni kwamba hakuna sababu yeyote ya msingi ya kufanya hivyo dhidi ya Mh rais wetu

Nikushauri achana na stori zako za vijiwe vya wavuta bange na wavuta ugoro mnapotoshana huko

Taifa linasonga mbele na litasonga mbele chini ya jemedari DR JOHN MAGUFULI.......over
 
hiyo ni kesi ya uhaini kuipindua serikali iliyochaguliwa na wananchi
Mkuu watu hawaogopi kufa sembuse kesi ya Uhaini? Hivi mtu anayetaka kupindua nchi utamtishia kwa kesi ya uhaini. Japo siungi mkono mambo ya kuponduana lakini utakua hauko serious kumtishia mtu kwa hilo. Akina Hanspope walifungwa kwa kesi hiyo mbona wanakula bata kama kawa na wamefanikiwa kimaisha kuliko kondoo wa enzi hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kabisa nikuhakikishie hakuna wakumpindua Mh.rais na hayupo na hata tokea kamwe katoka ardhi hii ya tanganyika na sababu kuu ni kwamba hakuna sababu yeyote ya msingi ya kufanya hivyo dhidi ya Mh rais wetu

Nikushauri achana na stori zako za vijiwe vya wavuta bange na wavuta ugoro mnapotoshana huko

Taifa linasonga mbele na litasonga mbele chini ya jemedari DR JOHN MAGUFULI.......over
Nyerere kipenzi cha watu lakini halikoswa kupinduliwa mara nane unalijua hilo?
 
Maybe the fear of flying? Who knows
Mbona yapo na yanatibika?

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Sio lazima Mh. Rais aende, katuma mwakilishi..!! Na yuko Addis, ww unawashwawashwa kama washawasha nn?
Wee utaonekana hauna akili kama kutuma mwakilishi ni sahihi kwa nini huwa hawatumii wawakilishi kwenda uwanja wa ndege? Hata kwenda kuzindua kiwanda cha sukari pia?? Mbona hawatumii wawakilishi kwenda kuzindua uzio? Mbona hawatumii wawakilishi kwenda kwenda kupokea ma mwendokasi?? Vitu vingine utumie akili. Yaani anaweza kwenda kwenye mambo ya kipuuzi lakini anashindwa kwenda kwenye vikao muhimu huu ni ujinga kama ujinga mingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom