Mkutano wa Waislam Mnazi mmoja - Kura ya kundi inaleta maana?

hao waislam wameshikwa na mafisadi wa Chama cha mapinduzi,ndio maana kila siku wanajaa ikulu kula daku,unategemea nini kwa watu waliosoma madrasa?
 
Mkandara,

..kuna Waislamu wengi tu wamesoma shule za Kanisa na hawakulazimika kubadili dini.

..pia kama Katoliki walikuwa wanaweka vikwazo wenyeji walikuwa na uwezo wa kujenga shule zao wenyewe.

..kuna maeneo mengi ya Tanganyika ambapo wenyeji walijenga shule nyingi zikiwa za msingi.

..hata vyama vya ushirika kama Nyanza Coorporation na KNCU vilikuwa vinatoa elimu kwa watoto wa wanachama wao.

..maeneo ya kwetu harakati za kudai Uhuru zilianzishwa na vijana ambao baadhi yao walipata elimu ktk shule za Kanisa na za Mkoloni.
Mkuu hata sielewi unachojaribu kusema..

Yaani unaukubali utumwa wa kutawaliwa kwa thamani ya shule za kanisa au?..Mkuu wangu record is clear tunapata Uhuru tuna injinia wawili tu sasa nambie hiyo elimu unayozungumzia ni elimu gani tupate kuisifia.. ZXanzibar walikuwa na wasomi kuliko sisi iweje tuanze kusifia makanisa na misikiti wakati hawa jamaa walikuwa wakifanya biashara na kufuata tawala policies za mkoloni ktk elimu..

Kuwepo kwa shule ili tutawaliwe au. hakuna mtu anazungumzia Waislaam walisoma vipi au wakristu. nazungumzia sisi sote in General.
Ni ujinga na upumbavu mkubwa mzungu au mwarabu anapokuja fungua shule kama biashara tunatumia dini yake kama sababu ya kuhalalisha Udini wetu. That Mzungu au mwarabu hakuoni wewe kama mwenziwe isipokuwa muumini tu wa dini ambaye kwake yeye wewe ni NYANI tu...Leo hii any success ktk elimu nchini tutatoa credit kwa Utawala uliopo madarakani na sii wafanyabiashara kwa dini na rangi zao..

Nitarudia kusema kama kweli walikuwa na nia nzuri tusingekuwa na idadi chache hivyo ya wasomi, kina Nyerere, Fundikira, na wengine wengi tu elimu zao zilikuwa za kukamatia na hatujui wazazi wao walifanya nini ili kuhakikisha watoto wao wanapata elimu.. Kuna wakati huwa nafikira sana hili... wengi walipata misaada ya watu binafsi na sii makanisa wala misikiti at what cost hatujui ila tunapenda tu kusifia makanisa na misikiti..Ndio maana wapo wahindi nchini wanachukua nafasi kubwa sana ktk ujenzi wa nchi yetu (elimu) kuliko jengo la shule lililosimama.
 
Mkandara said:

..sijui kwanini wakati mwingine unajadili hoja kwa hasira kiasi hiki.

..ndiyo, Mwalimu alichukua nchi ikiwa na mainjinia wawili. lakini hiyo haimaanishi kwamba Tanganyika nzima ni hao wawili tu ndiyo walioona shule.

..wakati tunapata uhuru walikuwepo waalimu, wauguzi, mafundi mchundo, mabwana afya etc etc. haimaanishi kwamba tulikuwa tumejitosheleza, hata sasa hivi hatujajitosheleza kwa wasomi, na hata taifa kubwa kama USA halijajitosheleza.

..miaka michache baada ya uhuru serikali ya Tanganyika ilianzisha mpango wa Africanization ambapo Wazungu waliondolewa ktk kazi za utawala serikalini. sasa niambie wazalendo waliojaza nafasi hizo walisoma wapi?

..hakuna anayesema kwamba mazingira ya elimu wakati wa mkoloni yalikuwa perfect. lakini lazima tuwe wakweli kwa kukiri kwamba msingi wa elimu Tanzania uliwekwa na wakoloni.

..vilevile lazima ieleweke kwamba wenyeji/natives walikuwa na uwezo wa kuanzisha shule zao wenyewe. siyo kweli kwamba shule zote zilikuwa za kanisa au misikiti. kulikuwepo shule za serikali na nyingine za wananchi[mfano KNCU,Nyanza Cooperation..]

NB:

..mkoloni hakuwa na nia ya dhati ya kutoa elimu kwa wananchi. lakini ktk mazingira hayo hayo wako wananchi walikuwa na mwamko mkubwa tu wa elimu. suala la mwamko wa elimu tunapaswa kulizingatia tunapoijadili sekta hii.
 
Back
Top Bottom